Sababu zinazopelekea kuumwa tumbo safarini

Sababu zinazopelekea kuumwa tumbo safarini

jigili

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
350
Reaction score
344
Kwa wale wajuzi wa mambo,

Ni vyakula gani vinasababisha tumbo kuuma na wakati mwingine kuharisha kabisa ukiwa safarini na hasa safari ndefu za magari?

Manake hii kitu huwa ni balaa, ukiwa unasafiri kwenye mabasi ya abiria unaweza umbuka!
 
Mara nyingi ukiwa na hofu ya safari lazima yakukute hayo
 
Usichanganye mayai ya kuchemsha,ndizi za kuiva,karanga,mahindi ya kuchemsha na sambusa lazima uharishe tu.
 
Kwa wale wajuzi wa mambo,

Ni vyakula gani vinasababisha tumbo kuuma na wakati mwingine kuharisha kabisa ukiwa safarini na hasa safari ndefu za magari?

Manake hii kitu huwa ni balaa, ukiwa unasafiri kwenye mabasi ya abiria unaweza umbuka!

Hiyo tunaitaga 'traveller diarrhoea' na ina sababishwa na E.Colli kumbuka kula kula vitu unavyokutana navyo njiani sio nzuri kwa afya kwa sababu hujui vimeendaliwaje usile njiani kabisa kwa usalama wako maana usafi kwa watanzania upo chini sana....kula vitu kama ambavyo viko seal kama biscuit, na the like ni vizuri but zingatia kunawa mikono na sabuni kabla hujaweka chochote mdomoni
 
Binafsi naona ukila vyakula vya mchuzi asilimia kubwa lazima hii hali itakukuta tofauti na vyakula vikavu,hivi ni nadra sana kusababisha matatizo ya kuharisha safarini.
 
Kuna siku nilishuka KIBAHA badala ya Ubungo stand Kisa tumbo nilivipotezea vitu vyote nilivyonunua njiani kama zawadi nikabeba begi tu!
 
Back
Top Bottom