Sababu zipi zilikupelekea ukawa shabiki wa hiyo timu yako ya sasa pale Uingereza?

Nilikuwa napiga sana kazi chafu nikiwa ground enzi hizo na nilikuwa nawaangalia sana Gilberto Silva na Patrick Vieira basi ndio ukawa mwanzo wa kuipenda arsenal hasa lile bato la Roy wa nyumbu na Patrick
Kwa sasa mpo na Jesus
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] nimecheka sana
 
Mimi niliamua tu kwenda tofauti na mzee..
Yeye Liverpool mm Manchester United
Bongo yy Simba mm Yanga [emoji172][emoji169]
 
Mimi ni shabiki wa Man U, sababu iliyonifanya niipende ni Marehemu Mme wangu(Apumzike kwa amani) alikuwa shabiki haswa wa Arsenal pamoja na watoto, kila Arsenal ikishinda mazungumzo yao yote ni kuiponda Man U nikajikuta naanza kuitetea Man U, nilianza kama utani kuwasema Arsenal ikifungwa, mwisho wa siku nikajikuta naanza kuipenda Man U na kuumia inapofungwa. Mpaka leo naishabikia mwanzoni ulikuwa ni mzaha mzaha tu ili nimkere Mme wangu
 
Gazeti la MFANYAKAZI enzi hizo liliandika LIVERPOOL BINGWA wakati mimi sijui hata kusoma kwahiyo marehemu sister alikuwa anatumia kunifundishia kusoma, basi nilitunza lile gazeti hadi nilipojua kusoma, basi kuna wazungu walikuja home miaka hiyo na mimi kizungu sijui ndio nikachukua gazeti nikampa mama awaulize kama wanaijua hiyo timu kumbe wazungu wale ni wadenish ila wakasema wanaijua na wanaipenda, bado sikuitilia maanani hadi Dar esalaam television(DTV) na TVZ walipoanza kurusha ligi ya uingereza ndio nikaikuta liver na mzee Poul Ince wanazikunja na Roy Kean kwahiyo mimi nikawa upande wa giza mwenzangu ince, toka hapo nikawa liver, alivyokuja Michael Owen ndio ikawa kabisaaaa liver dam dam
 
Golini yupo Seaman akiwa backed up na kina Kewon, Silva, kati Viera, Jumberg mbele kuna Henry, Bergkamp, mawinga Overmas, Pires alafu manager mzee wa falsafa yakutotumia pesa nyingi katika usajiri. Kwa ARSENAL ile mahaba yangu yalijizatiti mazima mpaka leo hii
 
Miaka hiyo manyuu na gunners ndo walikuwa wanatamba, sasa gunners blacks walikuwa wengi zaidi so my best friend alikuwa anawaponda manyuu na kuwasifia gunners kuhusu ubaguzi so i chose the oppressed side. Hence the gunners ever since
 
Ronaldinho alinipeleka barca, kipindi hicho 2004 kila baada ya taarifa ya habari ITV ya usiku walikuwa wana kipindi cha kandanda... Siku hiyo walikuwa wanaonesha maajabu ya dinho na tokea hapo nikawa barca damu....

Uingereza nilikuwa naifatilia Chelsea lakini sijawahi kuwa fan wake... Nakumbuka mwaka 2008 nilisomaga gazeti moja kuihusu man city kununuliwa na waarabu na waliwapamba sana wale waarabu, na tokea hapo nikaanza kuwafatilia man city na nikanunuaga na jersey yao na ndo ikawa jersey yangu ya pili ya club kuivaa baada ya ile ya Barca

Kwahiyo uingereza nikawa naikubali man city zaidi kwa sababu ya mpunga wao tu...

2010 baada ya kuanza kukiwasha EPL na kuwa nafasi za juu hapo ndo nikawa die hard fan wao mpaka leo

Ila kwa barca hunitoi hata km ikishuka league
 
Nakumbuka 2004 kwenye darasa letu la sita kipindi hicho kila mtu alikua man utd... hadi vitoto vya kike man utd..nikapelekwa banda umiza siku moja kuwacheki wakiwapiga liverpool kwa kubebwa saana na mwisho wa msimu arsenal ndio akawa bingwa 03/04... nikasema niwacheki arsenal maana ligi miaka hiyo tvt na channel ten walikua wanaionesha timu ilikua ma black tupu ukimtoa kipa na pires tuu.. nikasema haya maniga ndio yamemaliza ligi bila kufungwa..niksema hawa ndio wanaume sasa...ndio ikawaa hivyo mpaka leo ni asenaali..
 
Legend Gianfranco Zola alinifanya niipende Chelsea kipindi hicho kocha gianluca Vialli. Zola alikuwa very talented player at that time.
 
The invincible Arsenal in 2003/2004- hii timu ilikuwa ya 🔥🔥 Sana kipindi hiko
 
Nilikuwa shabiki A.c. Milan early 90's ikiwa na Van Basten, Rijkaard na Rud Gullit
Baadae mimi na Rud Gullit tukahamia Chelsea
 
Nilimpenda Ronaldo Cr7 na sikubahatika kumuona akiichezea Man U nilimkuta Madrid na kuanza kuifatilia Madrid na kuipenda na Fans Wa Madrid na Ronaldo lakin siwez ishabikikia Man U.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…