ELISHA MKWAI
New Member
- Jul 26, 2022
- 1
- 0
Mabadiliko katika nyanja za kielimu, utawala,uchumi, afya,kilimo sayansi na teknolojia yanaweza kuchochewa na sababu zifuatazo.
Uzalendo. Uzalendo ni miongoni mwa sababu kubwa sana inayoweza kuchochea mabadiliko katika nyanja mbalimbali.
Mfano, katika nyanja ya elimu kama walimu na baadhi ya watumishi wataamua kufanya kazi kwa moyo pasipo kujali maslahi yao, kutakuwa na uwezekano mkubwa nyanja hiyo kupiga hatua na kuwa na maendeleo, na hata katika nyanja nyingine kama afya n.k, kama watumishi wataamua kufanya kazi kwa moyo basi maendeleo yatakuwepo katika nyanja hizo.
Utoaji wa elimu ya ukombozi wa fikra. Wadau mbalimbali wa elimu wanatakiwa kutoa elimu ya ukombozi wa fikra katika jamii zetu. Wakoloni walitutawala kwa miaka mingi sana, ila baada ya kupata uhuru wetu walituachia nchi yetu ila walihakikisha tunawaona wao kuwa ni bora sana kuliko sisi, na hii hupelekea kuona bidhaa zao ni bora sana kuliko bidhaa zetu. Kuna baadhi ya bidhaa zinatengenezwa nchini, ni bora sana kuliko za nchi zilizotutawala, ila bidhaa hizo zikija nchini tunazitumia hizo tukiamini kuwa ni bora sana kuliko zetu, hivyo basi elimu ya ukombozi wa fikra inabidi itolewe ili kukomboa taifa letu.

Upvote
0