Sabasaba siku hizi imepoteza mvuto

Wewe unataka ukawape Neno la Mungu kwani wao umesikia hawajui kwenye hayo maonyesho ya Neno la Mungu wakati huko pia wanapigaga kambi kula vichwa
Bila D 2 huwezi kuelewa comment yangu. Elewa ulichoelewa na kama unajua walipo toa location, mengine niachie mimi.
 
Naelewa Mimi nimetoa Wazo waonyeshe Ila wauze kwa bei punguzo maana pale wanauza pia sio kwamba wanaonyesha tu
Dhana nzima ya maonyesho ni kutambulisha kazi na bidhaa za wazalishaji mbalimbali kwa dunia. Suala la kuuza na kununua bidhaa kwenye maonyesho kama hayo lilikuwa maarufu kwa sababu ya upungufu wa bidhaa enzi hizo lakini siyo lengo hasa la maonyesho. Hasara ya kufanya maonyesho kama hayo yawe sehemu ya kuuzia bidhaa kwa unafuu ni kuleta vurugu na kuwafanya wanunuzi wakubwa wa jumla kushindwa kutembelea na kupata wasaa mzuri wa kujadiliana na wazalishaji. Wazo lako ni zuri lakini ingekuwa vizuri kama ingetengwa sehemu au muda mwingine wa kufanya promotion za aina hiyo.
 
Mnakosea kuwauita madada poa hao ni maofisa utelezi au utam maana wanatoa huduma ya utelezi na utam🤣🤣🤣🤣
Hakika Mkuu halafu ni kweli km walivyo Maofisa Usafirishaji sasa Hawa wapewe Jina lenye hadhi kidogo waitwe tu Maofisa warekebishaji hivyo tu inatosha swali la wanarekebisha nini wewe ukiwafikia ndio utajua wanarekebisha nini
 
Bila D 2 huwezi kuelewa comment yangu. Elewa ulichoelewa na kama unajua walipo toa location, mengine niachie mimi.
Fika Banda la Pili mkono wa Kushoto km unaelekea Magharibi mwa Banda la Kusini uelekea wa Mashariki kunja km unaelekea Kasikazini kulia kwako Kwa mbele utaona Banda lipo hapo
 
Nilijuta kuooteza muda wangu kwenda sabasaba ya mwaka jana, ile ilikuwa ni tamasha la burudani na sio maonyesho tena.
 
Bora tusubiri 8.8 ya wakulima tununue mahindi na mchele kwa gharama nafuu. 😃😃😃
 
Hapana. Black Friday na Saba Saba ni vitu viwili tofauti kabisa. Saba Saba kama ulivyoambiwa ni maonyesho ya wazalishaji kuonyesha bidhaa zao kwa wateja na siyo sehemu ya punguzo la kuuza bidhaa kwa rejareja.
Huyo haelewi hata kinachoongelewa, kataka tu na yeye achangie. Discount sales kama za black friday zina relate vipi na maonyesho ya biashara (exhibitions)..?
 
Naelewa Mimi nimetoa Wazo waonyeshe Ila wauze kwa bei punguzo maana pale wanauza pia sio kwamba wanaonyesha tu
Exhibitions haijawahi kuwa na malengo ya kuuza bidhaa kwa discount sales. Pale ni introduction of new products, new brands za biashara na connecting places za washirika, wafanyabiashara na wateja wao mbalimbali. Hio ndo primary objective ya exhibitions.
 
Kwani Serengeti breweries wao sio kampuni??! biashara yao inaendana na burudani kwahiyo kiburudisho cha muziki sio kosa kwao, au wao hawapaswi kujitangaza?? biashara zipo nyingi pale unaweza kwenda kuangalia hata wanaouza ma trekta wakakuelezea juu ya bidhaa zao.
 
Kwa hio watu hawaruhusiwi kununua zile products zinazoonyeshwa pale au inakuaje?
 
Kwa hio watu hawaruhusiwi kununua zile products zinazoonyeshwa pale au inakuaje?
Biashara ni buying and seliing of product to earn profit na wale ni wafanyabiashara, sasa kwanini watu wasinunue..? Pale ni exhibitions of products na elaborations of given services, lengo ni kwamba kutokea pale, watu waelewe zaidi kuhusu introduced products na brands mbali mbali za biashara ili waendelee kuwa wanunuzi na washirika/wadau wazuri wa hizo taasisi na biashara zilizopo kwenye maonyesho afterwards.
 
Hapa sasa nimekuelewa vizuri Mkuu
 
Upo sahihi kabisa, me nadhani bado waTanzania wengi tuna uelewa mdogo sana kuhusu exhibitions.
 
Upo sahihi kabisa, me nadhani bado waTanzania wengi tuna uelewa mdogo sana kuhusu exhibitions.
Hata suala la kusema hayo maonyesho hayana mvuto nadhani ni la huku mitandaoni tu ila kwa ground mambo ni tofauti kabisa
 
Maonesho haya zamani ilikuwa ni promotion za kufa mtu...yaani unaenda una saula unavyotaka...

Ila siku hizi Bei ya sabasaba...bora uende dukani tu.

Kiingilio kilikuwa affordable kwa kila mtu.

Sabasaba ilikuwa mtoko.
Tatizo ni ujio wa Instagram, imeondoa umuhimu wa physical marketing tools. Tukubali kubadilika.

Wewe unatumia milioni 10 kuweka banda sabasaba na kutembelewa na watu 2,000 ambao hata sio potential, maana haipo targeted. Ila Mwenzako anaweka banda lake Instagram kwa kulipia laki moja, anatembelewa na watu 20,000 ambayo ni highly potential kwa sababu wamekuwa targeted kwa bidhaa yako.
 
Maonesho haya zamani ilikuwa ni promotion za kufa mtu...yaani unaenda una saula unavyotaka...

Ila siku hizi Bei ya sabasaba...bora uende dukani tu.

Kiingilio kilikuwa affordable kwa kila mtu.

Sabasaba ilikuwa mtoko.
sasa kama watu nao wamechoka wanahangaika na hali ngumu ya maisha unategemea nini? nchi imebaki kusifiana tu kusikokuwa na kichwa wala miguu.
 
Yote Tisa,kumi tumpe mama maua yake Kwa yanayoendelea 77
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…