Elewa kitu wamarekani wanaita Black Friday na siku zingine km hizo maana yake ukienda siku hio ni unauziwa bidhaa kwa bei ya punguzo ikiwa ni kuvutia watu (wateja) kununua bidhaa kwa wingi mfano mdogo tuseme MIMI Jana nilienda kununua Dawa fulani ya mbu X kwenye duka fulani la Mama Y Ile Dawa X bei ya rejareja inauzwa 2500 Ila jumla inauzwa 1500, Mama Y akaniambia hii Dawa rejareja ni 2500 Ila jumla ni 1500 basi nakuuzi kwa bei ya jumla 1500 hii 1000 rudi nayo au nunua bidhaa nyingine, sasa km hivyo ndivyo inatakiwa ifanyike sabasaba kuwe na bei punguzo ukichukua bidhaa 10 kwa pamoja uuziwe kwa bei punguzo, sijui unanielewa