gidamulida
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 286
- 95
Tarehe 7.7. 1954 kilizaliwa chama cha Ukombozi wa Tanganyika. Kiliitwa Tanganyika African Nation Union (TANU).
Maazimisho ya sabasaba yalikuwa na historia ya kuanzishwa kwa Chama (TANU). Mnamo mwaka 1992 baada ya JAMHURI ya muungano wa Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi...vyama vya upinzani vilihoji kwa nini nchi ianzishe siku ya kuzaliwa chama? Je Serikali itaruhusu vyama vyote hata vya upinzani siku yake ya kuanzishwa iwe siku kuu ya mapumziko kitaifa? Mwaka 1993 saba saba ilifutwa rasmi
Suluhisho ilikuwa ni kuondoa nguvu ya Serikali kwenye maadhimisho ya Sabasaba (maana viongozi walikuwa wakitumia sabasaba kutoa hotuba kwa taifa).
Kwa kuwa tayari siku ya Sabasaba ilikuwa ilishajitangaza tayari, ikabidi sasa itumike kwa ajili ya maonesho mbalimbali ya biashara....siku hizi saba saba ni siku ya maonesho ya wafanyabishara.
8 8 ilikuwa ni siku kuu ya wakulima tangu enzi ila ilihamishiwa siku ya tarehe 7.7 kila mwaka. Kwa hiyo baada ya mfumo wa vyama vingi. 8 8 ilirudishwa kwenye tarehe yake. Wenye uelewa mpana zaidi karibuni