SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

Status
Not open for further replies.

Kua msabato hakumaanishi kua tayari ni mtakatifu!
 

Mimi nina rafiki yangu hapa mtaani, kutwa siku za sikukuu anaenda kwenye mkesha pale Navy beach Kigamboni kama unapafahamu. Kibaya zaidi anasimulia jinsi anavyowakamatia wanawake viuno, KITIMOTO HATAKI HATA KUSIKIA. Ni kweli kabisa, wengi wa hawa majamaa NI WANAFKI.
 

Labada Mimi ndo nachanganya mambo! Ningependa kufahamu Haya kwanza! Mungu, Yesu na Roho mtakatifu na neno la Mungu ambalo kwalo kuna agano la kale na jipya na yote Haya hayaipingi sheria! Maana naona hapa torati ndo tatizo! Ukinipa maelezo juu ya huo utatu na kazi zao na neno la Mungu lote kwa ujumla nielewe utakua umenisaidia!
 

Kua msabato au Muisrael wa kiroho hakumaanishi kua ni mtakatifu!
 
1. Kutahiriwa; Katika Agano la
Kale muumini asiyetahiriwa
hangeweza kuhesabiwa haki hata
kidogo. Katika Agano Jipya
kutahiriwa siyo lazima ili
uhesabiwe haki na Mungu (Mwa
17:9-10, Gal.6:15).
2. Katika Agano Jipya tunaweza
kula vyakula vyote isipokuwa
vilivyotolewa sadaka kwa
sanamu au vilivyonyongwa bila
kuchinjwa, lakini wakati wa
Agano la Kale kulikuwa na
kuzuiliwa kula baadhi ya vyakula
hasa baadhi ya wanyama kama
vile sungura, nguruwe, samaki
wasio na magamba, nk. (Mdo
26:12-18).
3. Katika Agano la Kale kulikuwa
na utaratibu wa kutoa sadaka za
wanyama ili mtu aweze
kuhesabiwa haki. Hii ilikuwa
sheria. Katika Agano Jipya Yesu
amelitangua kabisa hilo halipo
tena. Damu yake iliyomwagika
inatosha kuondoa dhambi ya kila
amwaminiye Yesu.
4. Katika Agano Jipya Kuhani
alipaswa kuwa mtu mmoja tu
amabaye alipaswa kuendesha
ibada yote na kutoa sadaka za
kuteketezwa. Hilo nalo Yesu
alilitangua baada ya Kifo chake
Msalabani kila amwaminiye
anakuwa kuhani wa Mungu na
anaweza kufanya ibada ya
kuongea na Mungu moja kwa
moja bila kupitia kwa mtu
mwingine.
5. Wakati wa Torati ya Musa siyo
watu wote waliokuwa wanaweza
kumwagiwa Roho Mtakatifu
ilikuwa ni kwa makuhani au
manabii tu. Lakini hilo naalo Yesu
alilitangua na watu wote wenye
mwili wanamwagiwa Roho
Mtakatifu.
Mwisho kabisa kuna vitu vingi
sana Yesu alivyotangua na leo hii
siyo tena maagizo ya sheria
kwamba usipoyafuata umevunja
Maandiko
Ntunzu.
 

Kweli Nakubali kua tunaongozwa na Roho mtakatifu! Lakini kuongozwa kwetu huku hakumaanishi kua torati na neno la Mungu kwa ujumla limepita! Kama tunavo muona Mungu baba na torati na Yesu Na injili huku tukiona torati haitenguliwi. Sasa shida ipo hapa kwa Roho mtakatifu, kwanini yeye auache msingi wa wenzake yani torati?
 
ha ha ha! acha utani kwani hayo maisha yaliletwa na nani? unaijua njaa wewe? unaweza kwenda kuimba mapambio huku wanao wanalia njaa!!?

Teh Teh! I like that men! Acha bana kunichekesha!
 
Kua msabato hakumaanishi kua tayari ni mtakatifu!

sasa kwa nini ukatae kufanya mitihani siku ya jmosi lakini ukafanye uzinzi? kwa nini ukatae kufanya mitihani jmosi huku ni dhurumati? na hayo si yamekatazwa pia ktk amri 10?
 

Roho Mtakatifu hajauacha Msingi, kumbuka alikuweko hata kabla ya Adam na Hawa. Ila tulikaa chini ya Sheria ili kusubiria ile ahadi/neema ambayo Mungu alimwambia Ibrahimu kuwa 'kupitia wewe jamaa zote wa dunia watabarikiwa' Mwanzo 12:1-5. Pia Sheria ilitufanya kutambua dhambi kaka. Sasa ili Agano la Mungu na Ibrahimu litimie ni lazima Mwanakondoo auawe, kumbuka Ibrahimu alikubali kutoka kwao kwa ajili Mungu, pia alikubali kumtoa mwanae wa pekee Isaka kama Sadaka ila matokeo yake akachinjwa Kondoo. Yule kondoo aliechinjwa ndio ulikuwa unabii, na Yesu ambae ni mwanakondoo akaja akafa msalabani, damu yake ndio sadaka. Ibrahimu alihesabiwa haki kwa KUMWAMINI MUNGU, SI KWA MATENDO YA SHERIA ILA KWA IMANI. IBRAHIMU HAKUTUNZA SIKU YA SABATO KAMA SIKU.
 

Aleyn Umerukia vitu vingine kabisa! Na katika Haya unayoeleza hayaenendi sawa na mafungu unayoyasema! Nimeekuuliza swali juu ya Utatu na maandiko haujibu! Unakuja na vitu vingine kabisa! Kwa kifupi ni Ivi Yesu anasema! If you love me keep my commandments! Sasa Kama wewe sheria hauzitaki Nina Mashaka na huo upendo wako kwa Roho mtakatifu na Yesu!
 

Alyen unachanganya sana mambo! Katika hili la Abram mbona halihusiani na sheria ata kidogo? Tuwe tunajadili kitu kimoja baada ya kingine! Hapo tutakwenda sawa! Lakini kurukaruka na mafungu mengi!
 

Mkuu Biblia inasema Sheria imefungamana ktk Neno moja tu. Galatia 5:14 'Maana torati yote imetimilika ktk neno moja, nalo ni hili: umpende jirani yako kama nafsi yako. Pia ktk Luka, Yesu aliwauliza wanafunzi wake 'Sheria inasemaje' Petro akajibu 'Mpende Bwana Mungu kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote, kwa nguvu zako zote na kwa Roho yako yote na umpende Jirani yako kama unavojipenda wewe mwenyewe'. Yesu akajibu 'Sawa, fanya hivyo nawe utaishi'.
 
Alyen unachanganya sana mambo! Katika hili la Abram mbona halihusiani na sheria ata kidogo?

Jaribu kunielewa, Tumerithi Baraka za Abrahamu kwa kuwa yeye alihesabiwa haki kwa Imani.
 

Sasa ni kipi wewe unapinga sasa! Kwasababu sheria yote imesimama katika Upendo! Sasa Kama wewe una upendo kwanini usifate yale Yesu anayofundisha likiwemo na sabato?
 
Sasa ni kipi wewe unapinga sasa! Kwasababu sheria yote imesimama katika Upendo! Sasa Kama wewe una upendo kwanini usifate yale Yesu anayofundisha likiwemo na sabato?

Kama Torati/Sheria ina umuhimu kwa nini Yesu alikuja?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…