Nimefuatilia mjadala huu tangu mwanzo, ila nimegundua kuwa wapo watu wana ushabiki na chuki zaidi kwa imani za wengine;
Kumbukeni kwamba kila imani/dhehebu imejengwa kwa misingi, kanuni na sheria. Kila dhehebu lina sheria zinazoliongoza. Seventh day kama kanisa, lina misingi yake, na nina imani kwamba hata makanisa mengine yanaongozwa kwa imani, sheria na kanuni zake.
Moja ya kanuni na sheria za kisabato ni kuitunza siku ya saba ya juma, hii imetoka katika amri za Mungu ambazo Yesu alipokuja hakutengua hata amri moja, yeye mwenyewe alisema ni Bwana wa Sabato, aliponya siku ya sabato kwa sababu lilikuwa ni jambo jema, aliokoa siku ya sabato kwa sababu lilikuwa jambo jema, hata leo hospitali za wasabato zinatoa huduma za afya siku ya sabato... KWA SABABU NI VYEMA JUTENDA YALIYO MEMA SIKU YA SABATO! wasabato wanawatembelea wagonjwa, wanawatembelewa waliofiwa, walioko magerezani, kwa vile ni mambo mema.
Serikali yetu haina dini hivyo kutoa uhuru wa kuabudu siku na saa ambazo kila mmoja wetu anawiwa. Kusomea vyuo visivyo vya kisabato haina maana kuwa msabato asiruhusiwe kusali siku ya sabato, uhuru wa kuabudu ndio tunaotaka.
tedo, jaribu kuacha chuki na ushabiki dhidi ya imani zingine! Tuishi kwa amani na upendo, mwisho wa yote we are all Tanzanians!