SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

Status
Not open for further replies.
Jaribu kunielewa, Tumerithi Baraka za Abrahamu kwa kuwa yeye alihesabiwa haki kwa Imani.

Unapozungumzia zama zile za Abram na za Yesu Na hizi tulipo sasa. Watu walihesabiwa au watu wanahesabiwa haki kutokana na taratibu Mungu alizoweka! Lakini yote hayo hayazifuti sheria za Mungu na ndo maana ata katika sanduku la agano lililopi katika hekalu kule juu mbinguni kuna zile Amri kumi za Mungu!
 
Kama Torati/Sheria ina umuhimu kwa nini Yesu alikuja?

Baada ya mwanadamu kuingia zambini kukawa na mpamgo wa upatanisho kati ya mwanadamu na Mungu! Kuna njia zilielekezwa hapo zamani Na walizifanya kupata hiyo toba lakini yote hayo yalikua yakimlenga Yesu kufa msalabani Kama kafala halisi! Kuja kwa Yesu kuna maana nyingi, na Hilo likiwepo! Mkuu muda unakimbia sana! Saa Saba nataka kupumzika! Harakaharaka Unaweza ukanijb!
 
Jaribu kunielewa, Tumerithi Baraka za Abrahamu kwa kuwa yeye alihesabiwa haki kwa Imani.

Nashukuru sana kwa kuwa na muda kujadili hili! Nimefurahi na kupenda. Sana hoja zako! Kuna vitu nimejifunza! Mungu akubariki! Kesho saa4 Ivi ntakua kwenye line! Thx
 
Mkuu, mimi naamini wewe ni mtu mzima kabisa tena mpaka upo hapa Jf. Unaniona mimi nipo tofauti na wewe ktk Imani, kadhalika na mimi pia. Mimi bhana nilikuwa ni Mkatoriki halisi kabisa, nilipoanza kusoma sana Biblia nikaona mahali nilipo si sahihi na nikasema moyoni nipo tayari kubadilika kutoka kwenye Ukatoriki.Mwaka 2011 nikawa nasikiliza mihadhara ya dini kati ya Wakristo na Waislamu, matokeo yake nikaona Uislamu hauwezi ukanisaidia maana walizidiwa sana kwa hoja, nikasema bora nibaki zangu RC. Muda ulipita kidogo kisha nikarudi tena kusoma Biblia, safari hii nikawa nasoma sana UFUNUO WA YOHANA ghafla nikajikuta kuna dhamiri inanisukuma niokoke. Sikutaka kubishana sana na ile dhamiri kwani ilikuwa inalia sana, ilianza kulia mwezi wa 6 mwaka 2011, nikaja Nikaenda Kanisani Nikaokoka mwaka 2012 mwezi wa 7. Nilibatizwa nikiwa mdogo ila wakaniambia haya ni mambo ya Dini na Madhehebu, na mimi nilikubali moja kwa moja kwasababu niliamini baada ya kusoma Biblia. Baada ya hapo nimejikuta nikibadilika sana, mi najiona niko sawa ila watu walionizoea wananiambia Ongea yangu na matendo yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Mkuu, amini ninachokwambia, R/Mtakatifu ANAONGEA TENA ANA SAUTI KABISA, SAUTI YAKE NI YA UPOLE NA UNYENYEKEVU WA HALI YA JUU. Wosia wangu wa mwisho kwako ni huu 'Soma waraka kwa WAGALATIA WOTE, una sura 6 tu, wala sio nyingi, nina imani 98% utakusaidia sana Mkuu. Mimi siwezi kuuacha wokovu milele, nampenda sana Yesu maana pasipo ile Damu yake nisingekuwa hapa.

haupo serious mkuu. mtafute mtu anaitwa dr.zakir naik
 
yani nyie wote mnaotoa matusi mnatakiwa mtubu kwa mungu kwa dhambi mnazochuma, mnakaa na kuanza kujadili imani za watu? ingekua ni waislam msingethubutu ht kdgo kutoa matusi mtoayo,ila MUNGU atafanya kaz yake, sis wasabato c watu wa visasi na matusi
 
Mbona ni kama umekurupuka usingizini...?
 
ila we unachekesha, unajua hii nchi ina uhuru wa dini, kuwepo kwa wasabato wachache si kigezo cha kuwakandamiza imani zao. kusoma, kufanya mitihani siku ya sabato ni dhambi kwa msabato yoyote, basi na jumapili watoe hyo mitihani ili kuwe na usawa.

hata mitihani ingefanyika j2 hakuna shida kwa wakristo wa j2 maana hakuna sheria inayowazuia kufanya kazi hiyo j2. Ila mm nikiwa na mamlaka ya uongozi kwenye jamii yeyote sitowabughudhi wasabato ktk siku yao hii ya kuabudu wala kuwakwaza kwa namna yeyote maana ndicho wanachoabudu n wanajua misingi na sababu za kuiheshimu sabato.
Ni sawa na dini zingine zilivyo na misimamo yao na hawataki kusumbuliwa kwenye imani yao, mfano waislam hawataki muidhalilishe kuruani tukufu na hakuna haja ya kufanya hivyo.
Tutambue pia kuna familia ambazo ndani yake kuna madhehebu na dini tofauti, either mama or baba ni msabato, au mkristo wa J2 au ni muislam, hawa wasipoheshimiana familia itavunjika,vivyo nasi tusipoheshimiana ktk hili amani itapotea.
 
Nimefuatilia mjadala huu tangu mwanzo, ila nimegundua kuwa wapo watu wana ushabiki na chuki zaidi kwa imani za wengine;

Kumbukeni kwamba kila imani/dhehebu imejengwa kwa misingi, kanuni na sheria. Kila dhehebu lina sheria zinazoliongoza. Seventh day kama kanisa, lina misingi yake, na nina imani kwamba hata makanisa mengine yanaongozwa kwa imani, sheria na kanuni zake.

Moja ya kanuni na sheria za kisabato ni kuitunza siku ya saba ya juma, hii imetoka katika amri za Mungu ambazo Yesu alipokuja hakutengua hata amri moja, yeye mwenyewe alisema ni Bwana wa Sabato, aliponya siku ya sabato kwa sababu lilikuwa ni jambo jema, aliokoa siku ya sabato kwa sababu lilikuwa jambo jema, hata leo hospitali za wasabato zinatoa huduma za afya siku ya sabato... KWA SABABU NI VYEMA JUTENDA YALIYO MEMA SIKU YA SABATO! wasabato wanawatembelea wagonjwa, wanawatembelewa waliofiwa, walioko magerezani, kwa vile ni mambo mema.

Serikali yetu haina dini hivyo kutoa uhuru wa kuabudu siku na saa ambazo kila mmoja wetu anawiwa. Kusomea vyuo visivyo vya kisabato haina maana kuwa msabato asiruhusiwe kusali siku ya sabato, uhuru wa kuabudu ndio tunaotaka. tedo, jaribu kuacha chuki na ushabiki dhidi ya imani zingine! Tuishi kwa amani na upendo, mwisho wa yote we are all Tanzanians!
 
Last edited by a moderator:
hii imekaaje wakuu, katiba iliyopo inazungumziaje issue hii!

binafsi naweza kusema huu ni upumbavu,ina maana hawaelewi "vya kaisari mpe kaisari na vya Mungu mpe Mungu?na je ina maana bado tu hawajaelewa mafundisho ya Yesu kwa mfano alioutoa kwamba je PUNDA WAKO AKIANGUKA SHIMONI SIKU YA SABATO UTAFANYAJE?WALICHOKIFANYA HAWA JAMAA NI USHABIKI WA DINI NA WALA SIO KUFUATA IMANI.THEY ARE JUST FANATICS
 
we ndo umekurupuka nadhan, angalia tangu mjadala ulipoanza ndo utagundua kat yngu na wew nan ndo kakurupuka. poleeee
 
Nimefuatilia mjadala huu tangu mwanzo, ila nimegundua kuwa wapo watu wana ushabiki na chuki zaidi kwa imani za wengine;

Kumbukeni kwamba kila imani/dhehebu imejengwa kwa misingi, kanuni na sheria. Kila dhehebu lina sheria zinazoliongoza. Seventh day kama kanisa, lina misingi yake, na nina imani kwamba hata makanisa mengine yanaongozwa kwa imani, sheria na kanuni zake.

Moja ya kanuni na sheria za kisabato ni kuitunza siku ya saba ya juma, hii imetoka katika amri za Mungu ambazo Yesu alipokuja hakutengua hata amri moja, yeye mwenyewe alisema ni Bwana wa Sabato, aliponya siku ya sabato kwa sababu lilikuwa ni jambo jema, aliokoa siku ya sabato kwa sababu lilikuwa jambo jema, hata leo hospitali za wasabato zinatoa huduma za afya siku ya sabato... KWA SABABU NI VYEMA JUTENDA YALIYO MEMA SIKU YA SABATO! wasabato wanawatembelea wagonjwa, wanawatembelewa waliofiwa, walioko magerezani, kwa vile ni mambo mema.

Serikali yetu haina dini hivyo kutoa uhuru wa kuabudu siku na saa ambazo kila mmoja wetu anawiwa. Kusomea vyuo visivyo vya kisabato haina maana kuwa msabato asiruhusiwe kusali siku ya sabato, uhuru wa kuabudu ndio tunaotaka. tedo, jaribu kuacha chuki na ushabiki dhidi ya imani zingine! Tuishi kwa amani na upendo, mwisho wa yote we are all Tanzanians!

Asante sana Mkuu! Leo Hawa wanaoupinga ukweli ningependa waingalie Imani ya Yesu kutokana kutokana na maandiko! Na Kama wataweza kumtoa Yesu katika hivi vitu vitatu! Law, testimony, prophecy!
 
Last edited by a moderator:
Hapo haki haujatumika mbona udsm mitihani ya wikiendi mnaulizwa wanachuo wenyewe kama nafasi ipo mkipinga ratiba inabadilishwa kweli kwa stahili hiyo kuna umuhimu wa kusoma vyuo vya serikali jamani poleni wanafunzi wenzangu kwa kuonewa
 
Asante sana Mkuu! Leo Hawa wanaoupinga ukweli ningependa waingalie Imani ya Yesu kutokana kutokana na maandiko! Na Kama wataweza kumtoa Yesu katika hivi vitu vitatu! Law, testimony, prophecy!

Ili uwe huru kwako, nakushauri uazime Bible hata kwa Jirani, soma Waraka wa Galatia wote. Una Sura 6 tu, wala sio nyingi, utakusaidia sana kama ukiifungua moyo wako.
 
Ili uwe huru kwako, nakushauri uazime Bible hata kwa Jirani, soma Waraka wa Galatia wote. Una Sura 6 tu, wala sio nyingi, utakusaidia sana kama ukiifungua moyo wako.

Mkuu nataka niisome hiyo Wagalatia Na pia kabla sijaisoma! Ningependa kukuuliza hao Wagalatia Walikua ni watu gani na kwanini Paul aliandika huo walaka kwa hao kwa madhumuni gani au Kulikua na nini mpk Paul aandike huo walaka?
 
Ili uwe huru kwako, nakushauri uazime Bible hata kwa Jirani, soma Waraka wa Galatia wote. Una Sura 6 tu, wala sio nyingi, utakusaidia sana kama ukiifungua moyo wako.

Nimeisoma! Vipi kuhusu Wagalatia 3:19-25 inazungumzia mazumuni ya sheria, wewe unaonaje hapo hasa ule mstari wa24 na 25? Hii Galatians inazungumzia mambo mengi ila vitu vya msingi hapa ni sheria, upendo, Imani na neema n.k
 
yani nyie wote mnaotoa matusi mnatakiwa mtubu kwa mungu kwa dhambi mnazochuma, mnakaa na kuanza kujadili imani za watu? ingekua ni waislam msingethubutu ht kdgo kutoa matusi mtoayo,ila MUNGU atafanya kaz yake, sis wasabato c watu wa visasi na matusi

amina wew ni nuru
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom