SABATO SABATO SABATO wanafunzi 8 wa teku wafukuzwa baada ya kukaidi kufanya mtihani jumamosi!

Status
Not open for further replies.
Warumi 14: 13-20

13Kwa hiyo na tusiendelee kuhukumiana: Badala yake mtu asiweke kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya mwingine. 14Ninajua tena nimehakikishiwa sana katika Bwana Yesu kwamba hakuna kitu cho chote ambacho ni najisi kwa asili yake. Lakini kama mtu anakiona kitu kuwa ni najisi, basi kwake huyo kitu hicho ni najisi. 15Kama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. 17Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18Kwa sababu mtu ye yote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.
19Kwa hiyo na tufanye bidii kutafuta yale yaletayo amani na kujengana sisi kwa sisi. 20Usiiharibu kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula. Hakika vyakula vyote ni safi, lakini ni kosa kula kitu cho chote kinachomsababisha ndugu yako ajikwae.
 

Kwanza kabisa punguza jazba na kashfa kwa kuwaita wenzako wapumbavu.Ni kweli kwamba ya kaisari mpe kaisari na ya Mungu mpe Mungu;Siku sita za kazi za kaisari mpe kaisari bt Sabato ya Mungu mpe Mungu na ndo maana hata kwenye zaka Mungu tunampa 10% na iliyobaki ni yetu.Kuhusu kumuokoa punda aliyedumbukia shimoni,hilo ni sawa na huo unaitwa msaada siyo kazi ya kuunufaisha mwili,Kwani mtihani usipofanywa siku ya sabato kuna ubaya gani au uharaka gani huo.Huwezi kuacha kumpa Mungu utukufu au kusali kisa mtihani,kwani kipi bora kati ya Mungu na mtihani wa kidunia.Yesu alitupa mfano mzuri kabisa wa matendo yapaswayo kufanywa siku ya sabato na wala hakufuta sabato,kwa mfano;kumponya mtu siku ya sabato ni jambo jema,kumtoa kondoo shimoni siku ya sabato ni jambo jema la uokozi na msaada.Hakuna mahali panapoonesha Yesu alifanya kazi ya kikaisari siku ya sabato,kama papo nipe vifungu.
 
Waebrania 8:

[SUP]7 [/SUP]Kama lile agano la kwanza lisingekuwa na upungufu, kusinge kuwapo na haja ya kuwa na agano jingine. [SUP]8 [/SUP]Lakini Mungu hakurid hika na watu wake, akasema, "Siku zinakuja, asema Bwana, nitaka pofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. [SUP]9 [/SUP]Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao siku ile nilipowashika mkono niwaongoze kutoka nchi ya Misri; kwa kuwa hawakuwa waaminifu kwa agano langu, nami nikawaacha, asema Bwana. [SUP]10 [/SUP]Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli siku zile zitakapowadia, asema Bwana: nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. [SUP]11 [/SUP]Haitakuwapo haja tena kwao kumfundisha kila mtu mwenzake, au kila mtu ndugu yake, na kusema, ‘Mfahamu Bwana,' kwa maana wote watanifahamu, tangu aliye mdogo kabisa hadi mkubwa kuliko wote. [SUP]12 [/SUP]Nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikum buka tena".


[SUP]13 [/SUP]Anapozungumza juu ya agano jipya Mungu anahesabu lile agano la kwanza kuwa limechakaa, na kitu kilichochakaa na kuzeeka kitatoweka baada ya muda mfupi.
 

Mkuu MOSSAD II nadhani unachojaribu kuwanyooshea kidole wasabato hakina mantiki yoyote. Makosa au madhambi ya mtu mmoja ama watu wachache hayawezi kuhalalisha kuichafua jumuiya nzima ama taasisi nzima.

Kwa mfano zimekuwepo kesi nyingi za mapadri kuwalawiti waumini wao, tena wengine wanawaingilia watoto wa kiume, Je hapo tuseme kwamba hayoi ndiyo mafundisho ya kanisa katoliki? Kumekuwa na matukio ya mapadri wa kikatoliki kuzaa na wanawake wengine hata wengine wanazini na wake za watu, je hayo ndiyo mafundisho ya kanisa katoliki?La hasha.

Pia kumekuwa na matukio ya wachungaji na maaskofu wa makanisa ya kiprotestant na kilokole (wenyewe wanajiita makanisa ya kiroho) ambapo wanazini na waumini wao, wengine wanawalawiti na kuwafanyia vitendo vingi ambavyo ni kinyume na mafundisho yao na mafundisho ya biblia, je hapo tuyalaumu makanisa au madhehebu yao kwamba hayo ndio mafundisho wanayowapatia waumini wao au wachungaji na maaskofu wao? hasha.

Sitaki kuzungumzia matendo maovu yanayofanywa na viongozi wa dini nyengine zisizo za kikristo kwakuwa hawana mafungamano katika hoja hii kwakuwa naona wakristo wa madhehebu mengine ndio mmesimama kidete kuwashambulia wasabato kwa sababu ambazo mnazifahamu ninyi wenyewe, ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka inaonyesha ni chuki ya aina gani mliyonayo dhidi ya wasabato.

Kwa mifano hiyo michache nataka kujenga hoja yangu kwamba waumini wa kanisa la SDA ni wanadamu kama walivyo waumini wa madhehebu mengine ya kikristo kama Wakatoliki, KKKT, Moravian, Menonite, TAG, EAGT, FGBF, Jeshi la Wokovu, AIC pamoja na madhehebu mengine yote ya kikristo.

Waumini wa madhehebu haya yote wamekuwa wakifanya mambo ambayo ni kinyume na mafundisho yao ya madhehebu yao lakini pia wamekuwa wakifanya matendo ambayo ni kinyume na mafundisho ya biblia. Sasa utakuwa ni upofu wa akili kama unajielekeza kuwakashifu wasabato wote kwakutumia watu wachache ambao umewaona wakifanya makosa basi unawajumuisha wasabato wote.

Kila mmoja ana historia ya kuishi na watu wa dini nyengine tofuti na yake ama kuishi na watu wa madhehebu mengine ya kikristo tofauti na dhehebu lake na huko kote tunashuhudia madudu mengi yanayofanyika kinyume na maandiko matakatifu. Wengine kama ulivyo wewe tunao mchanganyiko wa ndugu zetu wanaoabudu katika madhehebu tofauti pamoja na kuwa familia moja.

Mimi katika familia yangu yupo wasabato, wapo wakatoliki, wapo walokole(TAG & EAGT), wapo AIC, wapo KKKT, wapo jeshi la wokovu, wapo Ufufuo na Uzima na pia wapo waislamu. Kwa mchanganyiko huu tuna uzoefu na ushuhuda wa kutosha juu ya mienendo na matendo ya kila mmoja kwahiyo hatuoni sababu ya kunyosheana vidole kwa sababu tu ya imani ya mmoja ambayo wewe huiamini ama hudhani kuwa ni sahihi.

Kwahiyo tuache kukashifiana na kutukanana kwakuwa hayo si mafundisho ya biblia takatifu, na kama kweli ungekuwa unaisoma kwa unyenyekevu na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Biblia bila shaka ungekuwa na staha ya Kristo unapojibishana na wenzako.
 
Last edited by a moderator:
To summarize , God's true church in these last days will be a people who;
Keep the commandments all ten of them and have the faith of Jesus.
Have the testimony of Jesus, the spirit of prophecy? Giving guidance for this time.
Teaching nothing contrary to the written word of God.
Relay God's last call to men.
Preaching the everlasting gospel.
Give the message worldwide.
Call on men to worship God as creator.
Call attention to the sabbath as the memorial of creation.
Alert men that judgement is in session began their work around the year1844.
Jipime mwenyewe kwa Haya maneno na hiyo Imani yako'
 

Hapa ndo timbwilihuwa haliishi kamwe...Bora tuyaache tuheshimiane tuuu....Unachokiamini nitofauti na niancho kiamini...
 

Umeandika mambo mengi bila sababu! Wasabato wenyewe wana kashfu sana madhehebu ya wengine kwa kujiona wao ndio wacha Mungu tu! Labda hujanielewa, nasema sioni mantiki ya kugomea mtihani kisa unafanyika jmosi! Ni unafiki wa hali ya juu kukataa kufanya mtihani huku unaenda kufanya mambo mengine machafu!! Ni kichekesho kuniambia kuwa kufanya mtihani jumamosi kutamfanya mtu aende motoni! Si hawa hawa waliopiga kambi pale airport wakitaka kwenda ng'ambo bila passport na leo wanagomea mitihani kisa inafanywa jmosi?? Hivi tukianza kupuzimzika kuanzia ijumaa hadi jpili eti ni siku za Mungu/mapumziko tutaendelea kweli? Sidhani kama mungu anapendelea wavivu!!
 
hao jamaa hawakupitia madesa ndo mana vyuo vingine we ndo kwaheri ila teku ninamashaka akasema 'Nahitaji Rehema'.[/QUO
 
Kwa wengine dini zimekuwa kama madawa ya kulevya.
 

Kwanza nikukumbushe kwamba jina la Mungu wa Mbinguni unapoliandika lazima uanze na herufi kubwa, kinyume na hapo unakuwa unamzungumzia mungu wa dunia ambaye hana mamlaka juu yetu. Pili nikufahamishe kwamba wasabato hawakashifu madhehebu mengine bali wanafundishana kulingana na imani yao na misingi ya kanisa lao. Hata mara moja hutawakuta wasabato wanasigana na dini nyingine au dhehebu jingine kwasababu ya kukashifiana. Sasa wakati mwingine mafundisho yao yyanawakera baadhi ya watu na hapo ndipo mwanzo wa chuki kama hizi tunazoziona hapa.

Sasa hili la kuabudu Jumamosi nadhani unajaribu kukijengea hoja mfu. Inafahamika tangu mwanzo na mwanzo kwamba siku za ibada zilizopo rasmi ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kulingana na mapokeo na mkafundisho tulioyapokea. Katika mafundisho tuliyoyapokea ambayo ndiyo yameleteleezea siku hizi tatu kuwa za ibada, mafundisho hayo yametoa miongozo kadhaa ambayo tunaizingatia kadri ya uelewa na msimamo wa dhehebu moja hadi jingine. Sijawahi kusikia dhehebu lolote linademand kutambuliwa kwa siku nyinge tofauti na hzio tatu kuwa siku maalum za ibada. Hata madhehebu mapya tunayoyashuhudia kila siku yakichipuka kama uyoga wanaangukia humo humo, ijumaa,Jumamosi na Jumapili.

Jambo la pili nikusaidie kwamba huwezi kuhalalisha dhambi moja kwakutenda dhambi nyingine. Kama kuna msabato unayemfahamu anatenda dhambi fulani hiyo haimfanyi ahalalishe dhambi nyingine. Kwakuwa sote ni binadamu kutenda dhambi si jambo la ajabu lakini mwisho wa siku tunarudi kwa Mungu wetu na kutubu makosa yetu kisha tunasonga mbele. Hata mitume na wanafunzi wa Yesu walianguka dhambini mara kadhaa lakini bado waliweza kusimama wakatubu na kuendelea na utumishi wao.

Kwahiyo ndugu yangu usijaribu kuichukulkia imani ya wengine kwamba ni nyeoesi kiasi hicho, kama wewe imani yako ni nyepesi kiasi cha kuwa tayari kufanya kila kitu anachotaka mwanadamu basi nakuombea kwa Mungu akupe nguvu ya kujitafakari imani yako na mwenendo wako.

Ndio maana nikakupa mifano iliyo wazi kabisa hapo juu nikiamini kuwa utaona ukweli wa hayo unayoyazungumza. Hata walokole wanajiita watakatifu lakini mbona sioni mtu akiwashambulia? kwani kujiita au kujiona mtakatifu inakukera nini wewe? au inakupunguzia nini wewe? Mungu ndiye ajuaye nani mtakatifu na nani siye kwahiyo sisi binadamu hatuna haki hata kidogo kuwadhihaki wenzetu kwakuwa huo ndio mtazamo wao na hawajakuzuia wewe kujiita ama kujiona mtakatifu.
 

Mkuu Sio Kama hayo ulio andika hawayaoni na wala hawayaju! Wanayafahamu sana ila mioyo Yao imekua migumu na kwa makusudi hawaitaki kweili! Jana wengi walikua wanakurupuka na kusema Yesu na wanafunzi wake walifanya kazi siku ya sabato! Ukiwauliza ni kazi gani hiyo walio ifanya hawajibu na wanarukia vitu vingine! Wengine wakasema bible yenye yamshuhudis Yesu kufanya kazi na sabato! Ukimuomba mafungu hatoi! Ukiwapa fungu hili sijui wao wanajiendea vp? If you love me, keep my commandments.John 14:15 Hawataki kabisa kuelewa sasa sijui huu upendo wao kwa Yesu uko wapi? Au Yesu wanamtaka lakini sheria zake hawazitaki.
It is lawful to do good in a sabbath day Matt12:12. Hapo Yesu aliwajibu mafarisayo wale na Hawa wa Leo hayo majibu ya Yesu hawayataki wanazidi kumsurubisha msalabani Kama wale wayahudi kwa Madai kua alivunja sabato!
You are my friends if you do whatever I command you. John 15:14. Sasa huu urafiki wao na Yesu wa agano jipya tu ambao Yesu mwenyewe anasisitiza sheria kuzishika una Mashaka! Wengine wanasema agano la kale limepitwa na wakati sasa kwanini Yesu Kama rafiki yetu anatuamuru kuzishika sheria Kama tunampenda?
Why do you call me Lord, Lord and do not do the things which I say? Luke6:46. Wengi wetu humu hivi ndo tumuitavo Yesu lakin kwanini hatufanyi yale Yesu anayotuagiza? Likiwepo na swala la kushika sheria Ambamo humo ndani ya sheria sabato ipo!
From the evening to evening, you shall cerebrat your sabbath. Lev23:32.
Ndio sabato itaendelea kutunzwa daima.
For I am the Lord I do not change. Mal 3:6. Huyu bwana amekuaje Mpaka wanadamu Leo waseme sheria hazipo tena wakat yeye mwenyewe anasema habadiliki?
Moreover I also gave them my sabbaths to be a sign between them and Me, that they might know tha I am the Lord who sanctifies them! Eze20:12. Hapa sasa sijui Hawa jamaa wakisoma hawaelewi! Tumepewa sabato milele Kama utakaso! Sijui utakaso utapatikana wapi mbali ya sabato?
And in vain they worship Me, teaching as doctrines the commandments of men. Mtt15:9 Jamani wanataka Yesu aseme nini tena juu ya Hawa watu?
For what will it profit a man if he gains the whole world and loses his own soul? Mark8:36. Hapa ndipo hao wanafunzi waliofukuzwa Chuo waliposimamia.
Here is the penitence of the saints; here are those who keep the commandments of God and faith of Jesus. Rev14:12 huu ni ufunuo wa yahona aliandika kwa maelekezo ya Yesu! Sasa Hawa saints wako hapa!
And I fell down at his feet to worship him, But he said to.me, see that you do not do that! I am your fellow servant, and of your brethren who have the testimony of Jesus. Worship God! For the testimony of Jesus is the spirit of prophecy. Rev19:20
To the law and to the testimony. if they don't speak according to this word, it is because there is no light in them! Isa8:20
Law
Testimony
Prophecy
Hivi vitu ndo Imani ya Yesu na Roho.
 
Hapa ndo timbwilihuwa haliishi kamwe...Bora tuyaache tuheshimiane tuuu....Unachokiamini nitofauti na niancho kiamini...

Tendo usiishiwe nguvu Mimi nataka wewe uendelee kuikosoa sabato kwa mafungu yako unayo yafahamu! Mbona hii kitu Sabato inakua tatizo?
Aleyn. Nasubiri majibu ya kitabu cha Wagalatia nimekuuliza maswali hapo nasubiri majibu!
Au Kama kuna mtu yeyote amesoma maswali Yangu niliomuuliza Aleyn juu ya Wagalatia na anafahamu vizuri juu ya nini Paul alikua anaandika juu ya Wagalatia? Na hao Wagalatia ni Walikua watu gani? atusaidie kuweka sawa hii kitu! Kwasababu huwezi kujenga Imani yako kwa kitabu kimoja tu cha Wagalatia.
Anyway! Ukisoma Wagalatia 3:19-25 hapo utaona mtume Paul anaweka wazi juu ya mazumuni ya sheria hasa ule mstari wa 24 na 25. Paul binafsi hapingi uwepo wa sheria ata kidogo!
 
Yesu ndiye Bwana wa sabatho.

Ubarikiwe sana! Hii mada inanikumbusha Kesi ya Yesu ilivo endeshwa! Alipokamatwa aliuzuria mabaraza matatu ya kutaka ahukumiwe kwa usiku ule na yote hayakumkuta na hatia! Na walipokua wakimkejeli kwa maneno mengine Yesu alikua akikaa kimya bila kujibu kitu! Lakin walipotaja Jina tu la Mungu haraka haraka Yesu alijibu tena kwa point kubwa mpaka hao Walikua wanamshitaki Walikua wanaaogopa! Hakusita kusimama imara juu ya Mungu! Hata Leo vita kubwa imeelekezwa kwenye kundi dogo hili! Wasabato simameni imara katika Imani yenu kwani hizi ni siku za mwisho!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…