Sabaya afanyiwa upasuaji wa kichwa

Sabaya afanyiwa upasuaji wa kichwa

Father of Chemistry

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2021
Posts
401
Reaction score
1,282
Mawakili wa upande wa utetezi kwenye kesi namba mbili ya mwaka 2022, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kuwa hali ya Sabaya ni mbaya baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa Julai 27,2022.

Sabaya alifikishwa Mahakamani hapo leo huku kichwa chake kikiwa na bandeji huku mkononi akiwa na kifaa cha kuchomekea dripu.
Wakili upande wa mashtaka Sabitina Mcharo aliieleza Mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba wanasubiri kibali kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali cha kuipa uwezo Mahakama hiyo kuendelea kuisikiliza kesi hiyo.

Wakili upande wa mashtaka Sabitina Mcharo aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba wanasubiri kibali kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali cha kuipa uwezo mahakama hiyo kuendelea kuisikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Elibariki Philly ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 12,2022.

source
#MillardAyoMAHAKAMANI
 
Mpeni pole, mwambieni aombe msamaha raia wana hasira kali
 
mbona nilisikia anaumwa mguu
 
mungu atamponyesha navkesi atashinda na uteuzi atapata mkuu wa mkoa
 
Kuna mtu alisema ile turu ya kichwani inatokana na laana au kulogwa... Kwamba ukiliondoa yanaota mengine ya kutosha..

Ila nadhani kilichotokea Tanzania miaka miwili iliyopita ni fundisho kubwa sana..

Kiongozi bora usilete maendeleo ila sio kutumia uongozi wako kuumiza watu.. utapigwa na laana ya kila namna
 
Back
Top Bottom