Sabaya amekiri makosa yote yaliyokuwa yanamkabili na Uhujumu Uchumi. Walionyanyaswa na Sabaya waende wapi Kushitaki?

Sabaya amekiri makosa yote yaliyokuwa yanamkabili na Uhujumu Uchumi. Walionyanyaswa na Sabaya waende wapi Kushitaki?

Anaandika Malisa GJ

Sabaya amekiri makosa yote yaliyokua yanamkabili. Uhujumu uchumi ameomba "plea bargaining" na ametakiwa kulipa faini ya milioni 5. Yani fedha zote alizodhulumu kwa wafanyabiashara, watu binafsi na taasisi, faini yake ni milioni 5 tu. Makosa mengine Mahakama imempata na hatia na imempa adhabu ya kumwachia huru kwa masharti kuwa asifanye kosa lolote ndani ya mwaka mmoja (conditional discharge).

Lakini je, watu walionyanyaswa na Sabaya waende wapi kudai haki zao? Wapo waliopigwa, waliodhulumiwa mali, na wengine kugeuzwa vilema na Sabaya. Kwa mfano Diwani mstaafu wa kata ya Narumu (Chadema), Bw.Nickodemo Mbowe, yeye na mwanae walivunjwa miguu na Sabaya. Oktoba 2020 Sabaya na genge lake walivamia nyumbani kwa Nickodemo na kumpiga wakimtuhumu kuchapisha kura feki.

Akaambiwa aoneshe mtambo wa kuchapishia kura ulipo. Akasema hana mtambo wowote. Sabaya akapekua nyumba akakuta laptop akavunja, akakuta TV akavunja, kisha wakampiga mzee Nickodemo na kumvunja mguu. Mwanae alipojaribu kumuokoa baba yake nae akapigwa na kuvunjwa mguu. Dogo alipoonekana mbishi akakatwa sikio. Nyumba nzima ikatapakaa damu. Familia ikaomboleza, kijiji kizima cha Narumu kikaomboleza. Lakini wafuasi wa Sabaya wakamsujudu na kumtukuza wakimwita "Jenerali"

Leo Nickodemo na mwanae wamebaki na ulemavu wa kudumu. Kila wanapotizama vilema vyao wanamkumbuka Sabaya. Kijana amepata ulemavu wa kusikia. Upepo ukivuma kwake ni mateso. Lakini mtesi wao ameachiwa huru kwa kigezo cha kukiri.

Kukiri hakuondoi hatia, kukiri hakukufanyi uwe msafi, kukiri hakubadilishi yaliyotokea. Kukiri kunasaidia Mahakama iweze kukuhukumu kwa haki bila kuhitaji upelelezi wa ziada. Ni ajabu mtu anakiri, badala ya kufungwa anasamehewa.

Eti tumemsamehe kwa masharti ya kutokufanya kosa ndani ya mwaka mmoja.! Nonsense kabisa. Basi toeni fursa kwa majambazi wote waliopo magereza, wakikiri muwaachie huru kwa masharti hayohayo mliyompa Sabaya. Fanyeni ujanja-ujanja tu lakini msisahau yupo Hakimu asiyeweza kufanyiwa ujanja. Jina lake ni YEHOVAH. Yeye hana "plea bargaining". Anaweza kuingilia kati na kuamua ugomvi kama alivyoamua 2021. Hamjifunzi tu??
Kukiri makosa na kuhukumiwa kwa Sabaya kwaweza kufungua milango ya madai dhidi ya Sabaya na mwajiri wake (serikali) kwa walioathirika.
Lazima wananchi wanapopata tatizo watazame mbali kutafuta recovery.
Serikali lazima ihusishwe ili kupata fidia toshelezi kwa kuwa Sabaya binafsi atakosa uwezo wa kulipa na pia serikali inahusika kwenye makosa kwani ilimuajiri.
Wanasheria wakae mkao mzuri wa kuwasaidia waathirika, kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria katika uongozi na pia kutoa fundisho kwa watu wanapopata madaraka wayatumie kwa kutoa haki kwa busara.
 
Wite waliofanyiwa ushetani na Sabaya, wafungue kesi za madai dhidi yake na dhidi ya Serikali ambayo ilikuwa mwajiri wake.Waombe kulipwa fidia angalao ya bilioni 2 kila mmoja kwa kusababishiwa ulemavu.
 
Back
Top Bottom