Yaani ni raha hureeeeeeee, 2025 CCM ijipange kutoa rushwa. Pamoja na kuwa Sabaya kwa kweli alikeuka miiko ya utumishi, ila kwa kazi alizofanya za kufifisha upinzani alipaswa CCM wamlinde, ila sasa ndiyo basi. Kitakachoendelea sasa ni wateuliwa kupiga (hasa wale ambao ziyo wazalendo). Na hii trendi ya uharamia wa Sabaya hayupo peke yake, kwenye taasisi nyingi za umma kuna ka kikundi kaliko tumia jina na ukali wa Dkt Magufuli kujifanya wametumwa then wanaomba rushwa ili wasifikishe tuhuma zao kwa rais, kitu ambacho watu wengi waliogopa sana kufikishwa kwa Dkt Magufuli hivyo ilibidi watoe rushwa. Kwa hii issue Sabaya katumika kama kafala ila waliofanya huo uovu wanaweza kuwa wengi sana. Ndiyo maana Mama anapotoa maagizo yake awe specific sana lasivyo watafanya kama kwa Dkt Magufuli (mfano kuna kipindi Dkt Magufuli alipokuwa waziri wa mifugo na akapiga marufuku mifugo kuhama hama, basi kuna njemba walijitokeza tokea pande zote tiss polisi wakafanya msako kuna msukuma alipoteza ng'ombe mia 600, na walitumia kauli ya waziri). In short vetting inahitaji irekebishwe, irudi kama zamani yaani vetting siyo miezi iwe miaka na pawe na pool ya watu waliofanyiwa vetting kurahisha kazi za uteuzi.