Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Kwani Sabaya kakutwa na hatia?Hizi tuhuma ambazo zinatolewa na Sabaya kuwa mamlaka ya uteuzi ilihusika kumpa kazi maalumu kisha tuhuma za uhalifu zikatokea ni aibu kwa taifa letu...
Wazalendo nambari 1 ambao walikua hawatumwi na mabeberuHawa ndiyo walikuwa wanaoitwa WAZALENDO
Ndiyo wawapore watu malizao?Wazalendo nambari 1 ambao walikua hawtumwi na mabeberu
Sabaya hajaiaibisha ikulu, katoa picha khalisi ya namna katiba ya mwaka 1977 inavyoweza kumfanya mtawala akawa jambazi, mtekaji, mtunguaji na hayawani kabisa, na akifanya unyambilisi wake wote huo, hamna wa kumuuliza, wote mnaufyata mkiaHizi tuhuma ambazo zinatolewa na Sabaya kuwa mamlaka ya uteuzi ilihusika kumpa kazi maalumu kisha tuhuma za uhalifu zikatokea ni aibu kwa taifa letu.
Ikulu ambayo ndio mahala pa kuonyesha mamka ya wananchi kuwageuka wananchi na kumtuma Sabaya kufanya uhalifu ni aibu kubwa na fedheha kwa taifa letu.
Yaani wananchi wanapiga kura kisha kuteua mtu ambaye anapewa mamlaka ya kuwa rais ili aongoze taifa kwa niaba ya watanzania wote, alafu anatuma mtu au watu maalulu ili kwenda kutesa na kupora kwa kutumia siraha.
Hii ni aibu na fedheha kwa taifa letu.
Hakuchaguliwa...alijichagua kwa mabavuNdo kusema wananchi walichagua mhalifu
Tatizo la Magu ilikuwa ni kutoa order: "...fanya lolote uwezalo ili mradi....". Hii ilifanya watu wafanye kila kitu ili mradi mzee anaridhika. Kweli wengi wameumia hata kupoteza maisha kwa mtindo huu.Ni ukweli usiopingika kwamba Sabaya katupa JIWE kwenye mzinga wa NYUKI! Salama ya nchi yetu kwa hili ni SABAYA kuadhibiwa!
Iwapo ataachiwa huru kutokana na kile alichodai uhalifu alioutenda ni MAAGIZO kutoka IKULU! Itadhihirisha wazi kwamba viongozi wa nchi hii ndo wanaohusika na genge la watu WASIOJULIKANA.
Hata kama ni MAAGIZO ya kufanya Opresheni Maalum, si amini kama alielekezwa kwenda kupiga, kupora na kujeruhi!
Acha tusubiri.