Sabaya ni ushahidi wa Taifa lilikokuwa linaelekea

Unasema au unatania? Nani ambaye angemfungulia mashtaka mteule pendwa kabla watu wasiojulika kufanya yao? Kuna watu walitolewa bastola hadharani lakini hakuna aliyeajibika, kuna watu walivamiwa kazini kwao kwa silaha lakini hakuna aliyewajibika, kuna watu walimiminiwa risasi hadharani lakini hadi leo kimya, kuna waliopotea mpaka leo wahajulikani walipo.

Ingekuwa vigumu MTU kufungua mashitaka kwa watu wa aina ya Sabaya, kwanza kesi kama ni hakimu yupi angeisikiliza?
 
Kuliponya taifa inatakiwa wasiojulikana wote wawe jela walipe uovu wao,uzuri wanajulikana na Jamii japo ujihisi wamejificha
Kwani waliomtolea bastola Mh. Nape hawafahamiki? Hawashikwi kwanini?
 
#29October2020; nilimkosoa Sabaya kuhusu kutumia magari yenye namba "feki" za UN kuteka na kuumiza wananchi wa Hai.

#30October2020; Sabaya akanipigia simu mara 3 sikupokea. Akaniandikia sms ya matusi na kutishia kuniua.

#1November2020; Nikascreenshot ujumbe huo na kumtumia rafiki yangu aliyekua kiongozi serikalini, just in case lolote likinitokea.

#26December2020; tukiwa eneo moja Moshi mimi na Don Mbowe, baada ya kuondoka Sabaya alivamia eneo hilo na kudai aoneshwe tulipo. Alipoambiwa tumeondoka alikataa kukubali. Akapiga risasi hewani na kuvuruga biashara eneo hilo.

#28December2020; Akakutana na binamu yangu Moshi (wanafahamiana). Akamwambia mpigie Malisa mwambie aje hapa, lakini usimwambie tupo wote. Jamaa akakataa. Akampiga na kumlaza rumande. Akamnyang'anya simu na hajamrudishia hadi leo.

#13May2021; Mama Samia akamsimamisha kazi kwa tuhuma mbalimbali.

#04June2021; akapandishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Nimwambie nini Mungu?

Malisa GJ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu pekee ndiye ametunyakua kutoka kwenye makucha ya yule nduli.
 
Siku yao yaja

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kuna viongozi waliyoteuliwa walitumia nafasi zao kuwapora watu mali na fedha zao,na vitisho juu cha ajabu mali fedha wanazozipora,wanazipeleka wanapojua wao

Ova
Mkuu si wanashinda hapo shivaz wanabaka asee[emoji22][emoji22]

Bad watch hebu aoge asee, asitutanie

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hivi mkuu mbona hueleweki??

Kuna mahali nimeona unaponda kuhusu sabaya kufungwa, sasa hivi tena unageuka!![emoji849][emoji849]

Yaan we upepo unakoelekea[emoji16][emoji16]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Utetez wa kijuha huu,hv unajua kwamba urais ni taasisi ambayo inawatu wanaoreport kwake kila siku?Jaribu kuficha huu ujinga,hakuna namna unaweza kumtetea Jiwe kwenye hili
 
Nani angemfikisha??? Kama alishindwa kumshughulikia Makonda akashughulika na Nape akatatimuliwa papo kwa papo.
 
Inatakiwa akamatwe na OCD na askari wake waliompa sabaya silaha kufanyia uhalifu nao waunganishwe kwenye kesi ya uporaji
 
Kuna wakati ukitafakari sana kwa kina utaona jinsi ambavyo hizi nchi zetu maskini zilivyo na tatizo kubwa sana kwenye hizi nafasi zakuteuana.Nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya imefika mahali nimefanywa kama fasheni.Tungekua ni nchi ya watu wanaojielewa kamwe usingeona watu kama hawa wanapata nafasi zakua viongozi.Ni aibu kubwa kuona mtu kama sabaya anapata nafasi yakutumika kama kiongozi wa umma.achilia mbali shutuma zake ambazo hadi zithibitishwe mahakamani ila jinsi tu alivyokua akiongea kwa kiburi na madaha unaona kabisa aliyemuweka kwenye hiyo nafasi alikua na sababu nje ya uadilifu na miiko ya kiongozi wa umma.kwa miaka ya hivi karibuni sidhani kama tumepata ata mkuu wa wilaya mwenye kiwango angalau cha kuwakaribia kina antony mtaka,mwenegoha,john mongela,au mkuu wa mkoa kama meck sadik,yusuph makamba au kandoro.Bado tunasafari ndefu sana yakuhakikisha mwenye mamlaka yakuteua anateua watu watakao kua na sifa halisi za kiongozi wa umma tofauti na hizi drama tulizozishuhudia hapo nyuma.
 
Sabaya was just a tip of an iceberg.
Mzee wa Burigi angeendelea kuwepo, ingekuwa KIVUMBI kwa watz. Kwenye mitano tena kila mkoa na wilaya vingekuwa chini ya li-Sabaya ili kutimiza azma ya kuifuta CHADEMA.
Halafu yangekuja ma-Sabaya mengi na mabaya zaidi kutokana na akina Heri James & co, kama njia ya kuwanyoosha wananchi 'wabishi' wasioimba mapambio wala kutajataja majina yake kwa bidii, lakini zaidi ni kujilimbikizia utajiri. Ndio ingekuwa kukamilisha mwisho wa mwanzo wa Korea Kaskazini hapa Tanzania
Tunashukuru kuwa tumeuona mkono wa MUNGU, tumeepushwa na ZAHMA hiyo.
AMEN
 
Pole
Enenda ukamtolee Mungu sadaka ya shukrani
 
Acha kupotosha watu , ni mala ngapi watu walipiga kelele juu yake, hadi na kuonyesha picha za cctv, lakini mamlaka yake ya uteuzi ilisema chochote?sana sana alikuwa ni kutoa vijembe tu!!hayo unayosema hata mtoto wa std two, atakushangaa, Jpm ndio alikuwa nyuma yake, na makonda ni mangapi alifanya watu wamepiga kelele, alifanya nini?kuna mamlaka yoyote ambayo ingekuwa na uwezo wa kumshitaki?muulize nape kilichomkuta alipotaka kufuatilia sakata la makonda na clouds .MUNGU NI FUNDI
 
Ewawwv
Tumekiepuka kikombe kile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…