Sabaya under probe for seven other claims

Yawezekana kulikuwa na sababu ya kwa nini TAKUKURU haikumchunguza wakati huo na sasa ni wakati muafaka kumchunguza na bila shaka ikibainika ni innocent atakuwa huru.
Umemjibu kwa hekima sana. Kama ni muelewa atakuelewa, ila kama ni wale waimba nyimbo, hawezi kukuelewa.
 
Siasa tu hapa gamna kitu, hata akituumiwa kwa makosa 1000 ni siasa tu. Wenye akili timamu wananielewa.

Hata kama alikosea ila sio kwa makosa yote, na sidhani kama ni yeye mwenyewe

Hiyo ndo siasa. Nalo litapita.
 
zile za kubaka wake za watu zimo au zenyewe bado.....
Kesi za ubakaji, ukishapita muda mrefu, ushahidi wake huwa mgumu. TAKUKURU na POLISI wanapokea taarifa nyingi lakini wanazifanyia uchunguzi na kubaki na zile wanazoweza ku establish case mahakamani.
 
Najiuliza hivi watu kama akina Sabaya wangefanikiwa kukaa madarakani miaka 10 ingekuaje ?

Lengo lao lilikua nini hasa kuamua tu kutumia ukatili wao kwenye nchi ya Kidemokrasia.?
Hivi hawakuona kua hata CCM ni chama chenye Demokrasia ya vyama vingi ndani yake?
Hawakujua kuwa CCM ilisukwa kikamilifu na Mwalimu Nyerere ,hivyo muda wowote chama kinabadili uelekeo wa utawala anapokuja mtawala mwingine?

Sabaya awe wa kwanza na wa Mwisho kutumia ofisi za umma kutisha watu kwa manufaa binafsi au ya genge Fulani au kundi Fulani . Kila mtanzania ana haki ya kuheshimiwa na kusikilizwa bila kujali rangi ,chama ,kabila na dini.

Kama kuna mtu au chama au kundi linalokiuka sheria kuna vyombo vya sheria ,na sio MTU kupita mitaani na genge lake na kupiga watu na kuwanyanganya Mali zao kwa kisingizio cha kupambana na wakwepa kodi.

MTU akikwepa kodi kuna taratibu zake za kisheria sio kutekwa na kuteswa.

Hata hivyo tunawaomba wafanya biashara wa Mbeya ,Moshi ,Arusha na Mwanza nao wabadilike na kulipa kodi bila shuruti na pia waache uhalifu wa kutumia maguvu kupata fedha.
Kuna maeneo yaligeuka kuwa vichaka vya majambazi waliokua wanatafuta fedha kwa nguvu huku wakiwa wanakesha kwenye mabaa kwa kujipongeza.
Tunaweza tukawaonea huruma watu wengine lakini kuna watu walipata utajiri kwa ujambazi na uhalifu. Hao nao ni wa kupigwa vita kwa nguvu zote. Vita ya kupambana na majambazi wote isiishie kwa Sabaya na Genge lake . Kuna majambazi wengi sana wapo mitaani wakijifanya ni wafanyabiashara na wengine wanajivika migongo ya siasa na kuwa karibu na watawala na na baadhi ya watu ndani ya vyombo vya dola.
Nchi yenye matajiri majambazi ni hatari sana.
Jambazi ni jambazi tu awe anatumia ofisi ya umma au vinginevyo. Wote wachukuliwe hatua Kali.
Mwanza Mbeya ,Arusha na Moshi wasikubali tena kurudi kwenye matukio mabaya ya ujambazi ,uwe wa watu kama akina Sabaya au wa wafanya biashara wabaya.

Kila mtu afanye kazi yake kwa mujibu wa sheria.

Viongozi wa umma waongoze kwa mujibu wa sheria na wananchi wote ,wafanya biashara na wafanya kazi wote wafuate sheria.

Sabaya ,Makonda, Happy, Chalamila na wengine waliokua nyuma yao wanapaswa kuchukuliwa hatua Kali sana ili wananchi nao waone kuwa sheria ni msumeno.

Hakuna aliyeko juu ya sheria .

Mama yetu Samia usikubali kabisa kabisa kabisa kuvumilia wavunja sheria za nchi. Iwe ni mwananchi wa kawaida au kiongozi. Wote wafuate sheria.
 
Mku kuna kiongozi aliyemzid bashite kwa ujinga?
 
Mayor Juma Raibu
 
namwona makonda akiwa anaweka maji nywele... aisee Dar italipuka kwa shangwe mtoto wa mtukufu akipanda ngazi kuelekea kwa pirato.
Na itakuwa sherehe kubwa ule msambwanda utakavyopolelewa hapo mjini segadance
 
Wewe kifutu unaambiwa huyo Mzee Lyimo alipita kote huko hadi kwa Waziri Mkuu lakini wote walimgwaya jambazi Sabaya kwa vile alikuwa analindwa na dhalim mwendazake
 
Huyu sabaya ilikuwa tu siku yake ifike tu
Ila kwa waliyobahatika kukutana naye
Ule ushamba na ubabe wake wa kijinga waliuwona

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…