Sabaya under probe for seven other claims

Sabaya under probe for seven other claims

Yawezekana kulikuwa na sababu ya kwa nini TAKUKURU haikumchunguza wakati huo na sasa ni wakati muafaka kumchunguza na bila shaka ikibainika ni innocent atakuwa huru.
Umemjibu kwa hekima sana. Kama ni muelewa atakuelewa, ila kama ni wale waimba nyimbo, hawezi kukuelewa.
 
Siasa tu hapa gamna kitu, hata akituumiwa kwa makosa 1000 ni siasa tu. Wenye akili timamu wananielewa.

Hata kama alikosea ila sio kwa makosa yote, na sidhani kama ni yeye mwenyewe

Hiyo ndo siasa. Nalo litapita.
 
zile za kubaka wake za watu zimo au zenyewe bado.....
Kesi za ubakaji, ukishapita muda mrefu, ushahidi wake huwa mgumu. TAKUKURU na POLISI wanapokea taarifa nyingi lakini wanazifanyia uchunguzi na kubaki na zile wanazoweza ku establish case mahakamani.
 
Najiuliza hivi watu kama akina Sabaya wangefanikiwa kukaa madarakani miaka 10 ingekuaje ?

Lengo lao lilikua nini hasa kuamua tu kutumia ukatili wao kwenye nchi ya Kidemokrasia.?
Hivi hawakuona kua hata CCM ni chama chenye Demokrasia ya vyama vingi ndani yake?
Hawakujua kuwa CCM ilisukwa kikamilifu na Mwalimu Nyerere ,hivyo muda wowote chama kinabadili uelekeo wa utawala anapokuja mtawala mwingine?

Sabaya awe wa kwanza na wa Mwisho kutumia ofisi za umma kutisha watu kwa manufaa binafsi au ya genge Fulani au kundi Fulani . Kila mtanzania ana haki ya kuheshimiwa na kusikilizwa bila kujali rangi ,chama ,kabila na dini.

Kama kuna mtu au chama au kundi linalokiuka sheria kuna vyombo vya sheria ,na sio MTU kupita mitaani na genge lake na kupiga watu na kuwanyanganya Mali zao kwa kisingizio cha kupambana na wakwepa kodi.

MTU akikwepa kodi kuna taratibu zake za kisheria sio kutekwa na kuteswa.

Hata hivyo tunawaomba wafanya biashara wa Mbeya ,Moshi ,Arusha na Mwanza nao wabadilike na kulipa kodi bila shuruti na pia waache uhalifu wa kutumia maguvu kupata fedha.
Kuna maeneo yaligeuka kuwa vichaka vya majambazi waliokua wanatafuta fedha kwa nguvu huku wakiwa wanakesha kwenye mabaa kwa kujipongeza.
Tunaweza tukawaonea huruma watu wengine lakini kuna watu walipata utajiri kwa ujambazi na uhalifu. Hao nao ni wa kupigwa vita kwa nguvu zote. Vita ya kupambana na majambazi wote isiishie kwa Sabaya na Genge lake . Kuna majambazi wengi sana wapo mitaani wakijifanya ni wafanyabiashara na wengine wanajivika migongo ya siasa na kuwa karibu na watawala na na baadhi ya watu ndani ya vyombo vya dola.
Nchi yenye matajiri majambazi ni hatari sana.
Jambazi ni jambazi tu awe anatumia ofisi ya umma au vinginevyo. Wote wachukuliwe hatua Kali.
Mwanza Mbeya ,Arusha na Moshi wasikubali tena kurudi kwenye matukio mabaya ya ujambazi ,uwe wa watu kama akina Sabaya au wa wafanya biashara wabaya.

Kila mtu afanye kazi yake kwa mujibu wa sheria.

Viongozi wa umma waongoze kwa mujibu wa sheria na wananchi wote ,wafanya biashara na wafanya kazi wote wafuate sheria.

Sabaya ,Makonda, Happy, Chalamila na wengine waliokua nyuma yao wanapaswa kuchukuliwa hatua Kali sana ili wananchi nao waone kuwa sheria ni msumeno.

Hakuna aliyeko juu ya sheria .

Mama yetu Samia usikubali kabisa kabisa kabisa kuvumilia wavunja sheria za nchi. Iwe ni mwananchi wa kawaida au kiongozi. Wote wafuate sheria.
 
Unapopewa cheo kumbuka kuwa umepewa dhamana na si kuwa karaha kwa wananchi. Sabaya aliiufanya mkoa wa Kilimanjaro kama wa kwake na akawa anafokafoka kama vile mkoa ni Mali yake hadi nikajiuliza haki iko wapi na kwa nini haya yanatokea. Makonda, Mrisho Gambo walikuwa na mapungufu wa kiuongozi ila ya Sabaya ni zaidi.
Mku kuna kiongozi aliyemzid bashite kwa ujinga?
 
Former Hai District Commissioner Lengai Ole Sabaya will on Friday appear in court for the second time to answer to six charges facing him.

However, the Tanzania Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) in Kilimanjaro Region says it is investigating seven other accusations facing him.

The new charges come after prominent businessman Elioth Lyimo lodged complaints to PCCB’s Director General Salim Hamduni.
Mr Hamduni told The Citizen over the phone that he had already sent his men to investigate the businessman’s claim of being robbed of Sh25 million by Sabaya.

Apart from that, the head of PCCB in the region, Ms Frida Wikesi, spoke of seven other accusations facing Sabaya and that they have already launched investigations.

Ms Wikesi said there were some people who were mentioned to have been accomplices of Sabaya in committing crime in the region including Moshi Municipal Mayor Juma Raibu, who is also under investigation and that if proved he was involved in the crime he would also be arraigned.

“As you heard, there are various unearthed accusations facing former Hai District Commissioner Lengai Ole Sabaya. “Investigations into his accusations are ongoing in Kilimanjaro Region and when completed and proved to be true he will be taken to court for justice to take its own course,” said Ms Wikesi.

According to her, investigations against all those, who have been mentioned to cooperate with Sabaya to commit crime in the region, are ongoing so that justice can be done for the victims.

“It is true His Lord Mayor of Moshi Municipality, Juma Raibu, has also been mentioned. Investigations into the accusations facing him are ongoing and if he is proved to be involved, then he will be taken to court to answer to the charges facing him,” said Ms Wikesi.
Speaking about the businessman, the PCCB regional boss admitted that he had gone to her office and queried over the matter and that evidence about the complaints was still being collected by the Bureau’s officers.

“We have already taken statements from this businessman and evidence is still being collected as investigations will reveal the truth of the matter,” insisted Mr Wikesi.

When sought, the businessman admitted to having been robbed of his cash by Sabaya and that he had already submmited all of his exhibits to PCCB including his bank statement showing he withdrew the money on February 2, 2020.

“It is true Sabaya took my money totalling Sh25 milioni as I have my bank documents that show transactions took place on February 2, 2020 and I have already presented my bank slips to PCCB. For now I can’t talk anything because all the information about how the incident took place I have already handed it over to PCCB,” said Mr Lyimo.

On June 4, this year, Sabaya and his five accomplices were for the first time appeared before the Arusha Resident Magistrate’s Court where six charges were read out against them before the court’s two different magistrates.

The charges, which included armed robbery, money laundering, economic sabotage and seeking and receiving bribe, are unbailable.

Credits: The Citizen
Mayor Juma Raibu
 
namwona makonda akiwa anaweka maji nywele... aisee Dar italipuka kwa shangwe mtoto wa mtukufu akipanda ngazi kuelekea kwa pirato.
Na itakuwa sherehe kubwa ule msambwanda utakavyopolelewa hapo mjini segadance
 
swali moja ninalo jiuliza,
kwa nini sasa watu ndio wajitokeze kumlalamikia? kwani wakati huo TAKUKURU haikuwepo?
aise haya maajabu ya Tanzania!!!
yaani hapo sasa vyonbo vyetu vinakaribisha majungu na fitina ndicho kitakacho endelee, na kwa mwendo huuu kila kiongozi lazima ataumia.
Ila ushauri wangu kwa Takukuru isikubali kupelekwa na maneno maneno ya majungu, ifanye kazi kwa weledi, kamwe isiendekeze maneno ya chuki na fitina, Majungu tupa kuleeeee!!! msipotezewe muda na rasilimali zenu kwa mambo ya kuokoteza na visasi.
Wewe kifutu unaambiwa huyo Mzee Lyimo alipita kote huko hadi kwa Waziri Mkuu lakini wote walimgwaya jambazi Sabaya kwa vile alikuwa analindwa na dhalim mwendazake
 
Huyu sabaya ilikuwa tu siku yake ifike tu
Ila kwa waliyobahatika kukutana naye
Ule ushamba na ubabe wake wa kijinga waliuwona

Ova
 
Back
Top Bottom