SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

Watanzania tunateseka tangu tumepata uhuru, kinacho zungumziwa hapa ni udhaifu wa raisi tu.
Ikiwa watanzania tunateseka tangu tupale uhuru unaonaje sasa ubaya kuwakaribisha wazungu ili kurudisha ukoloni tuondokane na mateso yaliyoanza toka baada ya uhuru. Hongera mama samia tuko nyuma yako
Twakuombea kwa Allah akuhifadhi
 
Ni yule aliyehama toka Anglican kwenda Catholic baada ya utawala wake au mwingine?
 
Ikiwa watanzania tunateseka tangu tupale uhuru unaonaje sasa ubaya kuwakaribisha wazungu ili kurudisha ukoloni tuondokane na mateso yaliyoanza toka baada ya uhuru. Hongera mama samia tuko nyuma yako
Twakuombea kwa Allah akuhifadhi
Ingependeza ungeomba ufafauni kuhusu hilo neno "MATESO" ili ujue nimemaanisha nini na kulenga nyanja ipi na ikupunguzie kazi ya kutafsiri usicho kijua maana naona una changamoto ya kukurupuka mkuu.

By the wei twende hivyo hivyo na hilo beat, kwanini umehisi mkoloni ataweza kuondoa mateso?
Je wakati wake hapakuwa na mateso yaliyozidi haya?
 
Kwanini Mazaa aende kutafuta ushauri kote huko, wakati hapo Msoga tu kuna mzee namfahamu anashauri vizuri tu!?!!
 
Ccm wala haiitaji kupigiwa kura kutangazwa mshindi wa uchaguzi.
 
Hatari sana kujiweka Rehani.

Awamu ya Sita tunawategemea wazungu kwa kiasi kikubwa.
Siyo dhambi kuwategemea wazungu kwenye mambo ya ushauri na teknolojia.

Tatizo wasifu wa huyo mtoa ushauri.
Tony Blair aliudanganya ulimwengu kuhusu silaha hatari za Iraq ya Sadam kisha wakaivamia Iraq na kumuuwa raisi wao na kuiharibu kabisa Iraq. Wasababisha vifo vingi kuliko hata silaha zenyewe walizo hisi zingekuwepo kweli.
Baadaye anakuja kukiri hawakuwa sahihi.

Pili Tony Blair yumo kwenye orodha ya kashifa ya Pandora papers. Kwamba alificha pesa na kufanya miamala ya kuweza kukwepa kodi. Ina maana ana tuhuma za ufisadi. Je huyu anaweza kumshauri vipi mtu aliyeingia madarakani kwa ilani ya chama chake yenye kupinga ufisadi?

Mama hapa kashauriwa vibaya sana. Na hii ni kashifa nzito ambayo inazipa nguvu tetesi za kwamba kundi la mafisadi limerudi tena awamu yake.
 
Mafi yao. Wasitupangie.

Blair ni MTU Na nusu. Ana exposure ya kutosha
 
Hangaya anajipendekeza kwa Majitu meupe.

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Huu ni wakati wanaCCM kumuomba Radhi Lissu kwa kumwiita kibaraka wa wazungu wakati mama keshamteua Tony blair kuwa mshauri wake!

Huu ni wakati wa ccm na vijana wa Mataga wote kumuomba radhi tundu lissu kwa kumuita kibaraka wa wazungu na wakala wa mabeberu mara sijui pro gay

Ni baada ya Rais Samia kumteua Tony blair kuwa mshauri wake wa masuala ya biashara na Corona

Tony blair ni beberu aliyetukuka na mzungu mwenye misimamo mikali ya kuwaza kupora rasilimali tu muda wote

Tony blair ametunukiwa tuzo ya kuwa mtetezi bora wa mashoga kwa miaka 30 mfululizo na sasa ndo mshauri wa Rais samia

Naomba ifike mahali sasa lissu aombwe radhi maana mlimsingizia watetezi wa mashoga wamelamba teuze kutoka kwa mwenyekiti wenu wa ccm na pia tunaona the jumong alivyoamua kuwa kibaraka wa wazungu aka mabeberu


Muombeni lissu radhi mara moja.....Ila mungu anatenda! Mlompakazia lissu mmeyaleta wenyewe nchini mabeberu mataga walowatukana sasa wapo nao ofisini..Malipo ni hapahapa....Ccm sasa mumuombe lissu radhi kwa kumchafua kipindi kile[emoji1317][emoji1317][emoji1317][emoji1317]
 
Sio sahihi, Tanzania sio nchi ambayo imeanza juzi, Samia akitaka kuongea na secretary of state ataongea nae ndani ya mwezi mmoja tu atakuwa tayari ameshampata , hata inaweza isifike mwezi ,week mbili tu.
Kuna procedure za kupata mawasiliano na kuweka appointment ya kuongea nae , hatua hizo zinaanzia ndani ya nchi yetu kw kuongea na Balozi husika wa nchi, hiyo ni kazi rahisi mulamula anaweza fanya .
Ni ujinga wa kiwango Cha juu kufikiri kuwa tukihitaji chanjo lazima tupitie Kwa secretary of state, Magufuli alinunua Boeing mbili USA je tulipitia Kwa secretary of state? Samia ni mweupe tu Wala sioni agenda yeyote.
 
Hii nchi tunaelekea kubaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…