Elections 2010 Sabodo aichangia CHADEMA Milioni 100 (tena)

Chief Isike

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2010
Posts
445
Reaction score
462
Leo tena majira ya asubuhi, historia imezidi kukolezwa wino baada ya mmoja wa wazalendo wa nchi na mfuasi wa kweli wa siasa za Mwalimu Nyerere, Mustafa Jaffar Sabodo amechangia Tsh. Mil 100 kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa Mwenyekiti wake Bw. Freeman Mbowe.

Huwezi amini mzee anajiamini, anasema wazi kuwa CCM imeyumba...kashangazwa na 'muungwana', the outgoing President na mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete, kwa kuwashika mikono na kuwakampenia watuhumiwa wa kesi za ufisadi...

Anasema upinzani si uadui, na bila upinzani madhubuti, serikali (ya chama chochote) iliyoko madarakani itayumba...

Ni hayo kwa sasa, ngoja niingie mtaani kwanza kuhangaikia mabadiliko ya nchi hii...ALUTA CONTINUA CAMARADOS
 
May God bless him and make him 1,000,000 times more rich
 
Hahaaaaa huyu mzee bana ananifurahishaga sana misimamo yake...
 
CCM wao wanakwapua kutoka hazina na matajiri.
Heko SABODO, najua wataanza kukufatilia ila simama kama ulivyosimama awali
 
Kweli hii ni digital population. Kabla hata ya kutoa hizo Mil 100 kwa chadema hujui tayari keshatoa ngapi kwa ccm.
 
Kweli hii ni digital population. Kabla hata ya kutoa hizo Mil 100 kwa chadema hujui tayari keshatoa ngapi kwa ccm.

siyo lazima awe ametoa kwa ccm pia, kwa misimamo yake angetangaza tu.
 
Naomba mods mdhibitishe habari hii. samahani mleta hoja, nimekugongea thanks, usimindi ila habari hii ni nzito inahitaji nguvu kwani huenda zikaongezeka soon.
 
And now abideth faith, hope, charity, these three; but the greatest of these is charity. I Corinthians 13: 13)

May Almighty enrich you Sabodo
 
Uyu mzee anajiamini wenzake wanatoa kwa kificho
 
Asante sana mzee!...

"...Sijawahi kuona mtu anayetoa misaada akifilisika"...Reginald Mengi
 
Mungu ambariki, anatoa kwa ajili ya mabadiliko ya maisha bora kwa waTZ wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…