Elections 2010 Sabodo aichangia CHADEMA Milioni 100 (tena)

Elections 2010 Sabodo aichangia CHADEMA Milioni 100 (tena)

Sabodo ndie yule gabachori?

Angechangia CCM usingemwita GABACHORI!! Magabachori unawajua KIBUNANGO ni wakina Manji, Subash Patel,,Dewjis na Rostam bana !!Huyu babu ni mzalendo wa kweli mambo yake hafichi wala sio mnafiki na ndio maana hamumpendi!!
 
Namfananisha sabodo na shivji. Mwaka 2005 hivi ni yeye aliyeunda finyazo ya ANGUKA (Ari, NGUvu na KAsi mpya) katika makala aliyoitoa gazetini wakati huo
 
wow wow wow wow,thanks sabodo!
May God bless you,the history will remember you
 
Kibunango bana huwa ananifurahisha sana mkuu wangu, never appreciates duh!!!

Sabodo hongera sana na ubarikiwe zaidi. Ukweli ni kuwa mabadiliko yanayotokana na nguvu ya uma yapaswa kuungwa mkono!!
 
Huwezi amini mzee anajiamini, anasema wazi kuwa CCM imeyumba...kashangazwa na 'muungwana', the outgoing President na mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete, kwa kuwashika mikono na kuwakampenia watuhumiwa wa kesi za ufisadi...

Anasema upinzani si uadui, na bila upinzani madhubuti, serikali (ya chama chochote) iliyoko madarakani itayumba...

Penye ukweli uongo hujitenga....................................
 
Source: Mlimani TV
Mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya kihindi Ndg.Sabodo amekichangia Chama cha Demokrasia na Maendeleo shilingi Milioni 100 (kwa mara ya pili sasa) na kuweka wazi kwamba yeye ni mwwnachama na kada wa siku nyingi wa CCM lakini amekerwa na tukio la Mwenyekiti wa chama chake na mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, JK kusimama hadharani kuwanadi wagombea mbalimbali wa nafasi za ubunge ambao serikali yake imewafikisha mahakamani kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi. Akisisitiza uamuzi wake huo amesema anafanya hivyo kwa faida ya demokrasia ya nchi hii.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesifu umakini na kutokuogopa kwa mfanyabiashara huyo kueleza wazi fikra na mitazamo yake bila kuogopa na kutamka wazi kua hiyo ni moja ya ishara ya usafi wa biashara zake na kuwataka wafanyabiashara wengine kuwa huru kifikra na kimtazamo kama Ndg.Sabodo
 
Safi sana mzee Sabodo. We hakika ni mzalendo, jasiri na muwazi.
 
sasa huyu ndo anatakiwa apewe degree ya heshima..sio JK ,kingredha chenyewe cha English Fountain pale makaburini sinza halafu eti Dr...
 
kweli watanzania na wasio watanzania wameamua kufata mabadiliko
 
Kibunango;1169508]Sabodo ndie yule gabachori?
ndio huyo huyo, within no time ataambiwa ni mfilipino aombe uraia upya
 
Naomba mods mdhibitishe habari hii. samahani mleta hoja, nimekugongea thanks, usimindi ila habari hii ni nzito inahitaji nguvu kwani huenda zikaongezeka soon.
Inabidi tupate uthibitisho wa hii habari, tusipongeze wakati habari haijakamilika.
 
Ijapokua hawezi kuzungumza kiswahili fasaa, bodylanguage yake by the tym anaelezea kuchukizwa na kitendo cha JK kuwashika mikono na kuwaita watu safi watuhumiwa wa ufisadi ilionyesha wazi jinsi alivyoudhika na jinsi gani hana woga wala wasiwasi kwa maamuzi yake.....nitafuatili kujua hasa mtu huyu anafanya biashara gani na kwa mda gani amekua kada wa ccm, ili kubaini kama kuna sababu zozote zinazomsukuma kwa haya yote au ni uzalendo uliopotea kwa wengi wa wa-TZ...
 
Ni ishara nzuri kwa binadamu kuwa muwazi na mkweli kwa mambo yanayohusu jamii yetu,vilevile kutoa mchango hadharani kwa chama cha upinzani bila kificho,ila maskini huyu mfanyabiashara usishangae ukisikia wanamzuria mambo kibao ili kumkata makali kwani fitina na majungu ni miimili mikuu ya CCM.
 
Wote tuige mfano huu si kupiga kelele tu hapa JF. Kuna watu nawakubali na najua kuna wengi wanachngia silently. Lakini namkubali mzee huyu kwa ujasiri alionao.
 
you can kill pipo,burn organization but revolutionary ideas will never die,mzee wetu kumbuka daima kumsaidia masikini ni kumkopesha mungu,chadema ni chama cha masikini wa kitanzania,jiandae kupata malipo yako kwa mungu
 
hizo pesa ziende zikasaidie wagombea ubunge basi... so tunafurahia hafu zinakoishia hatujui. wagombea hawajapewa sapoti kabisa.
 
Back
Top Bottom