Sabrina Sungura: CHADEMA kuna udini, Waislamu wanabaguliwa linapokuja suala la uteuzi

Sabrina Sungura: CHADEMA kuna udini, Waislamu wanabaguliwa linapokuja suala la uteuzi

Status
Not open for further replies.

"Kwa kuwa CHADEMA imemtuma Mbunge Rhoda Kumchela kunitukana kwa kuwa tu nimehama chama na kujiunga na CUF Leo ndio maana nikaona na mie nitapike nyongo zote ili Watanzania waijue CHADEMA ni chama cha aina gani, nimetukanwa"-Sabrina Sungura.
Ilo ni kosa la jinai umesharipoti polisi?
 
Nimehama CHADEMA kwenda CUF ambako hakuna udini, Wabunge wa viti maalum CHADEMA tulikuwa 36 kwa ujumla wetu lakini Waislamu ni watano tu, huko Wilayani Waislamu wengi wanafanya kazi kubwa ya kukinadi Chama lakini ukifika kwenye uteuzi wanabaguliwa"

"Kwa kuwa CHADEMA imemtuma Mbunge Rhoda Kumchela kunitukana kwa kuwa tu nimehama chama na kujiunga na CUF Leo ndio maana nikaona na mie nitapike nyongo zote ili Watanzania waijue CHADEMA ni chama cha aina gani, nimetukanwa"-Sabrina Sungura.
Kuna hoja ya msingi hapa.
Kwenye hii list ya wabunge 19
majina ya Kiashiria cha Kiislamu ni
1. Halima Mdee
2. Nasrat Hanje
3. Hawa Mwaifunga
4. Asia Mohammed
5. Sophia Mwakagenda
Majina ya Kiashiria cha Dini Zote
6. Salome Makamba
Majina ya Kimila, anaweza kuwa dini yoyote
7. Tunza Malapo
8. Kunti Majala
9. Nangenjwa Kaboyoka
Waliobaki 10 wana majina ya Kikristo
10. Ester Matiko
11. Cecilia Pareso
12. Ester Bulaya
13. Jesca Kishoa
14. Felister Njau
15. Grace Tendega
16. Stela Fiayo
17. Anatropia Theonest
18. Conchesta Rwamlaza
19. Agnesta Kaiza

NB. Idadi ya Wakristo ni 10, ila pia hao wenye majina ya Kiislamu na Kimila yanaweza kuwa ni majina tuu lakini wengine wakawa ni Wakristu, mfano Halima James Mdee, sijawahi kumuona akivaa Hijab au kuingia Msikitini, wala kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadan.

Hivyo hoja ya Mbunge huyu ni justified allegations, sio ya kuizingatia sana, kwasababu wakati wa uteuzi, dini ya mtu sio kigezo, ila pia tuhuma hii sio ya kuipuuzia!.
P
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom