Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,380
KWANINI CCM WAMESHINDA, NA WAPI WAPINZANI WAMEJIKWAA.
TATHIMINI INALETWA NA DON NALIMISON.
1. KWANINI CCM WAMESHINDA?
Tuangalie pande mbili Chanya na Hasi.
Tuanze na MATOKEO Chanya:
CCM ndio Chama kinachoshika Dola na hata Uchaguzi umefanyika TUME ya Uchaguzi ikiwa chini ya Dola ya CCM hivyo wamefanya Yao Kama Dola. Kumbuka Utii kwa vyombo vya Dola ni lazima hivyo vyombo vya Dola ni Mali ya CCM.
Wananchi waliwapenda CCM kwa kuwa walikuwa wanawapa burudani za Wasanii, ikumbukwe ukitaka kuwafariji watu wenye matatizo ni kuwapa Pesa au kuwapigia Disco waondoke na msongo wa mawazo, hivyo Wanamuziki ilikuwa ni kishawishi kikubwa kwa Wapiga Kura.
CCM walijikita zaidi kwenye Sera na sio kwenye madongo na walionesha huruma ya kuhurumiwa.
Wananchi walichoka na majimbo Yao kuwa na wabunge wasio timiza mahitaji Yao zaidi ya kuongea ongea tu na kujenga hoja bila vitendo hivyo wakaona wachague CCM.
Wagombea wa CCM wengi wamekuwa ni watu wazima na sio watoto kwa visingizio ni Vijana.
Tuangalie upande wa Hasi ya CCM:
Ni kweli CCM inaweza kuwa imepindua MATOKEO lakini je mawakala wa upinzani si walipewa Nakala za MATOKEO zinazo zungumza ukweli. Je, majeshi huenda yaliwakingia kifua CCM, na kama waliwakingia kifua mbona hakukuwa na vurugu?
NI WAPI WAPINZANI WAMEJIKWAA UCHAGUZI HUU?
Hapa ndipo tujiulize wote Wapinzani na wanaCCM. Nafikiri kilichowaangusha Wapinzani ni Kuanzia mchakato wa kupeleka fomu za wagombea ambapo wagombea wa Upinzani waliuza majimbo na kusingizia wamewekewa mapingamizi na wengine kusingizia wametekwa ili hali walikuwa Hotelini wamejificha wakila posho za kuuza majimbo.
Jambo jingine ni Mawakala wa upinzani wengi wamenunulika kiulani nakushindwa kujitokeza vituo vya kupiga Kura na wengine kujifanya wamebadilishiwa fomu.Kiujumla mawakala hawakuwa waaminifu.
Lazima tuangalie kule majimboni huenda hamjafanya lamaana na ndio maana wananchi wakapigia Kura CCM.
Vijana wengi sio Wapiga Kura ni Mashabiki tu, na ndio maana CCM walijikita na Watu wazima ambao ndio Wapiga Kura.
Wagombea wengi kutoka Upinzani walikuwa watoto japo mliwaita Vijana na hivyo wananchi wakaona Bora wawape kura CCM.
Kama kweli MATOKEO yamepinduliwa Kuna njia mbili za kudai Haki ikiwa Ni kwenda mahakamani japo Haki inachelewa na njia ingine nikuitisha Maandamano ya Amani kudai kurudiwa Uchaguzi kwa kutokuwa na Imani na Tume ya Uchaguzi.
Kwanini mpaka wabunge tegemezi wameanguka wakiwemo Mbowe, Sugu, Msigwa, MBATIA,Msigwa, Lema n.k Lazima kukaa na kutafakari Sana. Pia Upinzani mmetupa Vijana wazuri wenye Busara ya kuwaokoa na kutengeneza Vijana wapya wasio jua michezo michafu ya Kisiasa na michezo ya kijeshi. Hamkuona uthamani wa vijana wenu mkawatupa na kuinua waliotoka vyuo juzi wasio jua lolote wanaotaka Ubunge bila kusota kiharakati.
Haiwezekani Wabunge 28 wa CCM wapite bila kupingwa, kwanini Wabunge baadhi wa Upinzani nao wasipite bila kupingwa? Hii ni kuwa CCM wanatumia akili ya kiufundi lakini Upinzani wanatumia akili ya kuambiwa na ndio maana hawajui wafanyalo.
Lakini pia tuangalie kuwa Viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji ni Wana CCM wote na hao ndio walio kusanya Wapiga Kura na kuniokoa CCM, kumbuka Uchaguzi wa Serikali za mitaa wapinzani hamkushiriki na ndio njia iliyo wapa CCM Uchaguzi huu Mkuu KUSHINDA kupitia Viongozi wa mitaa na vijiji. Kwaheri ndimi Don Nalimison. Lakini pia je, Kuna uwezekano matokeo yakawa yamegeuzwa yaani matokeo ya CCM wamegeuziwa Wapinzani na matokeo ya Wapinzani yamegeuzwa kuwa matokeo ya CCM. Je, haya Mambo yanaweza pia kutokea? Na Kama yapo mmechukua hatua gani za Kisheria au za kudai Haki? Don Nalimison nawasilisha.
Tuangalie yafuatayo Sasa:-.
CHADEMA na ACT Wazalendo-Kipindi hiki baada ya Uchaguzi ndio muda wa kufumua Mfumo wote wa ngazi za Taifa hasa nafasi ya Katibu Mkuu ambayo ndio nafasi tendaji ya kubuni Ushindi. Uongozi ni kijiti na hivyo kufanyia MABADILIKO baadhi ya nafasi za uongozi ni Jambo la msingi Sana ili kurudisha heshima ya Chama. Kuunda mkakati mpya wa kujenga Imani mpya kwa Chama na Viongozi baada ya uchaguzi. Kusafisha Chama bila KUOGOPA kupoteza maana wengi watahamia CCM baada ya kupoteza matumaini. Hili Jambo la msingi kuinua Mfumo wa mpya wa Chama.
CUF-wao wamebahatika kupata Mbunge mmoja wa kuchaguliwa na hivyo watawajibika kunipanga upya katika kujenga Chama kwa kuweka Viongozi shupavu wa kurudisha matumaini ya CUF Ile ya zamani.
VYAMA VINGINE-vimepata mtaji wa wanachama kupitia Wapiga kura hivyo ni muda Sasa wakuwavuta wanachama wapya waliowapigia Kura na kujenga Imani mpya ya Chama.
Najua na kutambua kuwa RUZUKU za Vyama zitapungua Sana kutokana na kupoteza Wabunge na pia kura kuwa chache Sana lakini hilo sio Jambo la kuzimika kiharakati bali pambanieni kurudisha heshima za Vyama vyenu na Uongozi wenu yaani Wananchi wabaki na Imani na ninyi hata Kama mmepoteza majimbo na kata. DON NALIMISON nawatakia harakati njema wakubwa zangu.
Lakini pia je, Kuna uwezekano matokeo yakawa yamegeuzwa yaani matokeo ya CCM wamegeuziwa Wapinzani na matokeo ya Wapinzani yamegeuzwa kuwa matokeo ya CCM. Je, haya Mambo yanaweza pia kutokea? Na Kama yapo mmechukua hatua gani za Kisheria au za kudai Haki? Don Nalimison nawasilisha.
TUTAFAKARI NA DON NALIMISON KISHA TUANGALIE TUMEPOROMOKEA WAPI?