PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Benjamini Kuzaga, amewaomba waandishi wa habari mkoani humo kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa amani katika kipindi hiki ambacho taifa linatarajia kufanya uchaguzi mkuu.
Kwenye mdahalo wa kuangazia usalama wa waandishi habari mkoani Mbeya uliohusisha vyombo vya ulinzi na usalama, Asasi za kiraia, viongozi wa kisiasa, viongozi wa Dini, wanasheria na wadau mbalimbali wa habari Sacp Kuzaga amesema mambo mengi yanafanyika kwa sasa kwasababu ya uwepo wa amani hivyo ni muhimu waandishi kutoa elimu ya umuhimu wa amani kwakua habari zao hufuatiliwa na watu wengi zaidi.
Aidha Kuzaga amewahakikishia usalama waandishi wa habari mkoani Mbeya pondi wawapo kwenye kutekeleza majukumu yao katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu na kuwataka kuweka utamaduni wa kuzungumza na kutambuana kabla ya kuanza kutekeleza majukumu hasa pale yanapotokesa matukio ya kuhatarisha usalama wa raia.