GE2025 SACP Mchomvu: Wengine wanapotosha ili watu walipie 'Subscription', watanzania wengi ni wavivu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wakati Watanzania wengi wakingoja kutumia haki yao ya kikatiba kwa ajili ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba, imeelezwa kuwa wapo wanaopotosha ili wanaowafuatilia walipie maudhui yao (subscription).

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Richard Thadei Mchomvu amesema wanaofanya hivyo mtandaoni watakamatwa na kufikishwa kwenye mamlaka husika.

โ€œUjue kuna hela fulani zinalipwa kule (mtandaoni) kwa hiyo mtu anaweka mambo ya hovyo ili apate hela. Sasa namwambia hizo hela zitamtokea puani, sisi tuna uhakika. Wewe usitake kupata hela kwa watu kuingia kwenye akaunti yako ukiweka vitu vya hovyo vya kuidhuru nchi,โ€ amesema SACP Mchomvu.
Your browser is not able to display this video.
 
Ajira ni za shida sana, mpaka connection.
 
Aisee mitandao mingi imefungwa na serikali
Lakini bado mnaendelea kutoa vitisho?hii nchi ya kingese sana.

Very interesting!
 
Mbona hofu ni nyingi kutoka kwa mafundi viyoyozi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ