Hemed Mzee Hemed
Senior Member
- Jun 26, 2013
- 186
- 41
Chama Cha Mapinduzi kimedhihirisha mikakati yake haramu ya kuhakikisha katiba mpya itabeba MATAKWA yote ya NEC.. Jioni ya leo kuanzia saa 9-11 jioni kulikuwa na kikao kikuu cha wilaya/halmashauri ya kinondoni kujadili mapendekezo ya rasimu ya katiba mpya.. Kikao hicho kimefanyika Mwananyamala ukumbi wa CCM. Mgeni rasmi alikuwa NAPE Nnauye - Katibu wa itikadi na uenezi.
Wahusika katika kikao hicho cha halmashauri ya wilaya ya kinondoni walikuwa ni viongozi wote wa CCM ktk wilaya ya kinondoni. Hawa ni viongozi wa kata zote (yaani Mwenyekiti, katibu na katibu mwenezi) viongozi wa majimbo yote matatu (kinondoni, Kawe na Ubungo), Viongozi wa wilaya (Mwenyekiti, katibu, na katibu mwenezi), na madiwani wa kata zote za wilaya ya kinondoni. Wengine walikuwa ni wageni waalikwa kama vile viongozi wa mkoa, Wajumbe wa mabaraza ya katiba (wengi mno), mgeni - Nape Nnauye, na mimi (sitamtaja aliyenialika kuepuka kumtia hatiani).
Nape Nnauye ndiye aliyekuwa msemaji mkuu na ujumbe aliouleta ni waraka wa NEC kuhusu mabadiliko ya katiba ya nchi!... rasimu - -
1. Wanapinga vikali serikali tatu!... Msimamo wao ni kufuata mfumo uliomo kwenye KATIBA YA CCM (yaani mfumo wa serikali mbili).
2. Wanapinga Vikali mawaziri kutokuwa wabunge!... Msimamo wao Waziri ni lazima awe MBUNGE.
3. Wanapinga vikali mgombea binafsi kwenye nafasi ya uraisi.
4. Wanatarajia kuibadili karibu rasimu nzima na kupitisha matakwa ya NEC ya CCM!...
Wanajiamini kuwa watafanikiwa kwakuwa wananguvu 73% Bungeni na 99% katika MABARAZA ya katiba... Nimeshuhudia kejeli dhidi ya vyama vya upinzani hasa CUF na CHADEMA. Hata wajumbe kutoka majimbo ya Kawe na UBUNGO wanaitwa watu wa Mdee na watu wa Mnyika. Nilipouliza nikaambiwa walizembea na kuwaacha wapinzani kujitwalia majimbo kirahisi.
Mytake: Kama hali iko hivi nchi nzima, AMINI MSIAMINI HAKUNA KATIBA MPYA, ni heri vyama vya siasa vianze kupigania TUME HURU ya UCHAGUZI si KATIBA. Narudia tena Kwa MIKAKATI hii ya CCM katiba itakayopatikana haitakuwa na jipya...