Inasikitisha mno, kina Mama wa Bunge, Chama Cha Wanasheria wanawake, Mama Tibaijuka, hata Wanaume na Wanawake wengine walio viongozi na wasio viongozi, wanaoweza kumsaidia binti huyo, wasimtupe, wamsaidie ili na yeye aweze kuikomboa familia yake, Wanawake na Taifa kwa ujumla, viongozi wengi leo hii, enzi zile walisoma bure au kwa kuchangia kiasi kidogo sana cha pesa, baada ya kusoma na kufanikiwa kwao, wasiwasahau watoto wa masikini, asilimia kubwa ya hawa viongozi wetu walitokea kwenye familia masikini sana, hata viatu vya kuvaa kwendea hata shule, walikuwa hawana, wengi walivijua viatu miguuni mwao wakiwa Sekondari, lakini leo hii hawakumbuki wema waliofanyiwa naTanzania ya kipindi cha Nyerere na wakati wa wamissionari, wamekuwa na kiburi hata soksi na miswaki wananunua Ulaya, hivi hawa watu hawamuogopi Mungu, kweli shukrani ya punda mateke, wanaonaje kama wanashindwa kuchangishana pesa ili kuwasaidia hawa wanafunzi wanaotaabika na kuangusha machozi yao juu ya ardhi ya Tanzania, kwa sababu ya mioyo yao migumu, isiyojali na kuwahurumia wananchi wa Tanzania, basi wale mafisadi wafilisiwe ili hawa watoto wapate fedha za ada, malazi na matumizi mengine wanapokuwa Chuoni, sio kuanza kujiuza kwa Mashugadadi na Mashugamami ili waishi vizuri Vyuoni, tutapoteza nguvu kazi ya taifa kwa Ukimwi, ni nini tunataka wengi wao wakishafariki kwa Ukimwi, kuwaajiri Wageni au wale ambao wako bado Sekondari na shule za Msingi kama miaka ya 60, karne hii, si tutazidi kuwa masikini na kuchekwa na Dunia, au kama vipi, fisadi mmoja ama wawili wajitolee kuwasaidia hawa vijana ili hatimaye, Wananchi na Mungu wawasamehe kosa lao la ufisadi. Eeh!, Baba anayeshindwa kujitahidi kuwajali wanae na kuwapenda, ni Baba kweli, au ni Baba jina tu!, viongozi wa Tanzania vipi???!