Nimepitia michango yote lakini nilichoona ni wengi kuingia kwenye ushabiki tu wa kuponda US na wengine kupingana na wanaoponda.
Ninachoweza kusema ni labda wengi wanachangia lakini hawajaitizama hiyo clip hapo juu,na kama wameitizama,inawezekana hawajaelewa.
Matatizo yaliyompata ni ya kujitakia.Nimesikitishwa sana na stori yake lakini amejitakia na pia hasemi ukweli wote.
Yani mtu aliyekuwa akienda shule,akaambiwa na mwanamme aache shule eti na yeye akakubali,sasa wanawake kudanganywa inatokea marekani peke yake?
Nimesema hajasema ukweli wote kwasababu kuna wakati alisema kuwa manamme wake alimwambia aache kazi na yeye atamlipia ada and everything,halafu akadai kwamba hakujuwa kama alikuwa ni drug lord!Sasa yeye ni kitu gani kilimwaminisha kuwa huyo mwanamme ana uwezo wa kumlipia ada na yeye kubakia nyumbani ama ku concentrate na shule?
Ok,baada ya kuona kwamba halipiwi ada alichukuwa hatua gani?Yeye alichosema ni kwamba sasa mwanamme wake huyo alitaka tu abakie nyumbani,yani awe mama wa nyumbani,again ninaamini kuwa ni mambo ya pesa yaliyomuaminisha kuwa jamaa yuko fit,lakini kuja kusema alikuwa hajui kuwa ni drug dealer,hilo tayari kaongopa.
Kifupi matatizo aliyopitia ni matatizo ambayo mwanamke anaweza kuyapitia akiwa popote pale,na kwa kiasi kikubwa ni wrong decisions.Jambo ambalo halijalishi upo nchi gani.Mistakes are mistakes.
Hilo la wachangiaji karibia wote kusingizia kuwa matatizo aliyoyapata ni kwasababu ya kuwepo kwake US ni kushindwa kuelewa tatizo lilipo hata mara baada ya kuitizama clip hiyo(assume mmefanya hivyo),mbona kuna wasanii wenzake wamefanya makosa makubwa zaidi wakiwa bongo(mfano Ray C,Lulu na wengineo)
Ambao mnaponda US mna chuki zenu binafsi.Toeni ushauri ama mu express sympathies zenu lakini msiwe kama watu wasioweza ku analyze hata mambo madogo.
Kosa alilofanya ni kuacha shule baada ya kudanganywa na mwanamme.Na pia labda angeanza kuhangaika na makaratasi ili unafuu wa kusoma uwepo.