Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
1st Portion:
Na hii sio utani, sijivunii mama wa mtoto wangu. Sio kwamba nililazimishwa kuwa nae, hapana. Na katika kipindi chote nipo nae kwenye mahusiano nilikua muda mwingi anatawala mawazo yangu, na hata kuachana kwetu, ni yeye ndio aliniambia muda umefika nikatafute mtoto mwenzangu wa kudate nae. Katika kipindi chote nipo nae, sikuwahi kujua umri wake halisi ni miaka mingapi, Ila makadirio alinizidi miaka kati ya 25 hadi 30. Sijakosea, ilo ndo gape la umri kati ya mimi na mama wa mtoto wangu.
Kati ya vitu ninavyojutia sana, kimoja wapo ni ili tukio la huyu mama. Kitendo cha kukataa shule na kukimbilia mjini, sijawahi kukijutia kama ambavyo najutia kuzaa na huyu Maza. Katika huu Uzi, sito-base sana kipindi cha mahusiano yetu, Ila nitaongelea sana baada ya yeye kufahamika home, maana hapo ndio hasa niliona ukubwa wa ujinga niliofanya. Maana sterehe zangu zilileta mtikisiko kwenye familia, kibaya zaidi sikuwepo home.
Nilikutana nae kwa namna ya ajabu kwanza. Our first meeting alikuwa very harsh kwangu. Baada ya kutimuliwa kwenye nyumba niliyokuwa nafanyia kazi kwa kosa la kumtelezesha mke wa bosi kwenye malumalu, kama mtakumbuka, niliondoka bila kuwa na uelekeo maalum. Ila mwisho wa siku niliangukia buguruni sokoni. Nilifanya sana vibarua pale.
Mazingira yale kulikuwa na bi mkubwa mmoja ana kigrosary chake cha kizushi. Kama ulisoma story yangu, kuna grosary nilikua nakunywa soda, then nikamwambia muhusika abadilishe channel, maana kipindi kilichopo kilikuwa kinanipa machungu, then yule muhusika akanijibu shit. Sasa huyu muhusika/ Maza mwenye kigrosary, ndo huyu nilikuja kuzaa nae.
Wakati nafanya vibarua pale sokoni, sikuwa na sehem maalum ya kulala. Hivyo ningeweza kulala popote katika mazingira yale. Mara chache chache nilikuwa nalala pembeni ya kile kigrosary na jamaa wengine niliowakuta. Kuna siku nilichelewa kuamka, maana tulikuwa na kawaida ya kuamka mapema sana.
Hiyo siku yule Maza alikuta bado mazingira yale, japo sikuwa nimesinzia. Wala hakunikaripia, aliniacha nikaondoka kistaarabu tu. Mida ya jioni, nilikuwa nakatisha eneo lake, akaniita. Akaniuliza wewe ni mgeni maeneo haya, umetokea wapi na imekuwaje unalala nje? Siku ya kwanza nakuona ulikuwa smart, imekuwaje? Ikabidi nimfungukie tu, japo sikumwambia kama nilikimbia home. Nilimsimulia tu kisa cha kutimuliwa kwa yule Mzee niliyekuwa nafanya kazi kwake. Mwisho wa siku akaamua kunipa kazi pale kwenye grosary yake. Tulikubaliana niwe nasaidia manunuzi, usafi, ubebaji na uletaji bidhaa n.k, ujira wangu ikawa ni msosi.
Siku zilivyoenda akaanza kuniamini, nikawa hadi nasimamia biashara yake. Ikafika kipindi akanipeleka mpaka kwake, alikuwa anakaa maeneo ya gongo la mboto, japo alikuwa na makazi mengine kisarawe. Sababu ya misele yake na kazi, ndo maana alikuwa anakaa nyumba ya gomz, sababu ya ukaribu. Baada ya kufanya kazi kwake kwa miezi kama miwili, ndo akanipeleka pale gomz.
Mimi ndio nilikua naamka mapema nawahi kwenye grosary yake kufungua na kuweka mazingira vizuri, then yeye anakuja baadae. Na hata baadhi ya siku angewahi kuondoka kabla yangu, na mara nyingi tuliondoka wote.
Kuna siku alirudi amelewa maana siku hiyo alihudhuria kitchen party. Akilewa ni anaongea sana alaf usumbufu ni mwingi, mara fanya hiki, mara kile n.k. kiufupi anakuwa kama Muhindi kwa jinsi anavyotuma. Hii siku ndio ka mara ya kwanza nilitembea nae. Palivyokucha nilikuwa naona aibu as if wapangaji walijua nilichofanya (alikuwa amepangisha vyumba vilivyobaki).
Hata yeye nilikua naona aibu kumwangalia usoni. Nikawa nakwepa kukaa naye muda mwingi. Yeye akawa ananicheka tu, siku kama ya pili akaniambia najua kinachofanya uwe na aibu. Sikuelewa alimaanisha nini. Ila siku hiyo tulivyorudi home akanipa tena show, kesho yake tena, na tena. Mpaka ikawa rasmi sasa, na ile aibu ikatoka.
Tuliendelea na huu mchezo kwa muda mrefu mpaka ikawa sio Siri tena. Huyu Maza alishawahi kuolewa mara mbili hapo kabla, Ila aliachika kwenye ndoa zote sababu ya mambo yake ya kuendekeza starehe, lakini pia alikua akishika mimba zinaharibika/ zinatoka, so hakuwahi kuzaa. Taarifa zilipokuwa wazi kuwa anatembea na katoto, ndugu zake walikuwa wananichukia , kila siku wanampigia simu, maneno kibao, lakini sielewi alikua na akili gani yule Maza, Wala hakuonekana kujali.
After kama miezi 7 au 8 ya kuwa pamoja, alikuja kushika mimba. Alivyogundua ana mimba, kutokana na historia yake akajua hii haitodumu, so siku moja tunafunga hesabu, akanijulisha kuwa ana mimba, then akaniambia kabla haijatoka, nifanye mchakato wa kutafuta sehemu ya kwenda. Nikashangaa, namuuliza sasa Mimi nitaenda wapi? Akanijibu "We mtoto, Mimi sio mama yako, katafute mtoto mwenzio mfanye maisha"
Kiukweli sikutegemea angebadilika haraka vile. Akili yangu yote alikua kaiteka yeye. Na mpaka leo nikiona mtu anadate na mshangazi/jimama, simshangai. Mashangazi yaoneni tu vile vile. Sikuwa na jinsi, ikabidi siku hiyo nisirudi kwake, nikaamua kutafuta usawa mwingine. Nikamuacha yeye na grosary yake huku akisubiria ile mimba itoke. HAIKUTOKA
[emoji26][emoji26][emoji26]
Endelea hapa Sad Truth: Sijivunii na mama wa mtoto wangu