Sad Truth: Sijivunii na mama wa mtoto wangu

Sad Truth: Sijivunii na mama wa mtoto wangu

.......Baada ya kutoka kwa yule Maza, sikuendelea muda mrefu kupiga ushanta pale sokoni, ndio likaja lile wazo la kwenda mgodini Msumbiji ( yaliyoendelea after hapo yapo kwenye ile story). Huku nyuma yule Maza, mimba ilikua hadi akajifungua, Mimi sina habari, maana nilihisi ingetoka, sikuwa na simu na hatuna mawasiliano. Inaonekana baada ya kuanza malezi, alikuja akawa anaona kero na usumbufu.

Ile mtoto kuumwa umwa, clinic etc. Hapo nadhani ndio lilimjia wazo la kumpeleka mtoto home kwetu. Wazazi wangu walikuwa wanaishi mkoani, tena kijijini sio town. Kipindi nafanya kazi kwa yule Maza, alikuwa ananijua taarifa zangu nyingi, mfano kwetu tupo wangapi, majina ya wazee wangu, Kijiji walichopo n.k. Unajua ubaya au uzuri wa vijijini, ukifahamu taarifa za mtu, unaweza ukafika hadi anapoishi kwa kuulizia tu. Basi ndicho alichofanya yule Maza, alifanya jitihada hadi akafika home kabisa. Matukio mengi yaliyotokea wakati sipo, nilipata taarifa zake toka kwa sister, mama, baba na wadogo zangu wengine, kwa nyakati tofauti tofauti.

Yule Maza alipofika home, alikaribishwa vizuri tu. Unajua kijijini kwetu mgeni ukifika ambaye hawakujui kabisa, wala hawakuulizi umefata nini, wao wanakukirimu, then wanakupa nafasi. Sasa yule Maza baada ya ukaribisho, ndio akajitambulisha, akaniulizia Mimi, akaambiwa sijaonekana pale nina kama miaka miwili. Akawaambia kuwa ananifahamu vizuri, na huko nilipokuwa nimeacha mtoto ambae ndio yule. Unajua pamoja na utukutu wangu, Mimi ni kipenzi cha wote kwenye familia yetu. Ile habari ya kuwa yule mtoto ni wangu, wakaipokea vizuri, tena ukiangalia Wana muda mrefu hawajaniona. Dada angu alifurahi sana, hapo ndo akaomba mtoto ambebe, maana muda wote alikuwa bado kashikwa na yule Maza. Sasa wakati yule Maza anaendelea kuongea nao pale, Mama yangu akauliza mama wa mtoto yuko wapi, mbona hajaja? Yule Maza ndo kuwafungukia kuwa yeye ndio mama wa mtoto. Mshua kusikia vile alinyanyuka kwenye kiti kama vile amepigwa shoti, akawa anamwangalia yule Maza akihisi ameskia vibaya, dada na mama wao wakabaki wametoa macho. Yule Maza akarudia tena kauli yake, kuwa yule mtoto ni wangu, na yeye ndio nimezaa nae. Unaambiwa mama yangu alipiga ukunga mmoja mkubwa sana.

Baba alitoka sebleni speed mpaka chumbani kwake, then akatoka kabeba kibegi kama anasafiri. Mama akamuuliza, "Baba nanii unaenda wapi?" Mshua akawajibu huku anaondoka, kuwa anaenda serikali za mtaa kwa ajili ya ule mgogoro wa ardhi. (Huu mgogoro ulikuwa ni wa muda mrefu sana, na mshua alikuwa kila akiitwa anakataa kwenda, siku hiyo ndo akaona aitikie wito). Akawa anasisitiza, akirudi asimkute yule Maza.

Mama na dada wakabaki na yule Maza pale, hawaelewi wafanye nini. Yule Maza yeye katulia tu anawachora. Mama mara kaingia jikoni, mara chumbani, mara nje ili mradi hakuwa na utulivu. Yule Maza nae kila akitaka kumuita dada angu, alikuwa anamuita "Wifi", hapo ndio mama angu anazidi kuvurugwa. Dada nae akitaka kumuita yule Maza "Wifi" akili inakataa, ulimi unakuwa mzito. Siku hiyo mshua hakurudi home, na bi mkubwa Wala hakukumbuka kumuulizia. Dada ilibidi ampe kampani mama, akalala chumbani kwake ili kumpunguzia mawazo. Yule Maza akalala chumba cha dada. Niliivuruga sana familia yangu.

Usiku wakati wapo chumbani mama na dada huku, dada akawa anamwambia mama, labda yule Maza anawatania tu au amepotea nyumba, wasubirie pakuche waongee nae vizuri. Mama akawa anabisha, kuwa yule Maza hajakosea nyumba. Akawa anamwambia dada "Hivi katika kuzunguka kwako kote pua za namna ile ulishawahi kuziona wapi kama sio kwenye ukoo wa baba ako?, Yule mtoto ni wa hapa, cheki pua yake, tena nahisi ni wa baba ako, wanamsingizia tu mwanangu kwavile hayupo, we huoni baba ako alivyokimbia hapa?"

Katika kukua kwangu, hakuna siku ambayo niliona baba na mama wakigombana sababu ya swala la uaminifu. Hii ni kwa mara ya kwanza niliwaingiza katika mgogoro wa aina hiyo. Nakumbuka kipindi niko mdogo sana, tulikua tunatoka sokoni na mshua, wakati tupo njiani alitokea mwanamke from nowhere akamchapa Kofi la maana mshua, then akasepa bila kuongea chochote. Mshua alibaki ametoa macho tu, hata mimi nilibaki surprised maana sikuelewa imekuwaje kuwaje, nilishindwa kumuuliza mshua, nikatarajia ataongea kitu, nae hakuwahi niambia chochote mpaka leo. Lile tukio lilionwa na wengi, maana ilikuwa asubuhi, story zikamfikia mama. Aliniuliza sana, nikawa nakataa kuwa hapajatokea kitu kama hicho, so kitendo cha huyu Maza kuja na mtoto alaf anasema wangu, basi mama akaona ni yale yale tu, tunafichiana na mshua, yule mtoto ni wa baba, na yule Maza ni mchepuko [emoji26][emoji26][emoji26].

Kesho yake mshua alipiga simu kuuliza kama yule Maza ameondoka, alivyoambiwa bado yupo, faza akasema anaenda kumtembelea mdogo wake anaumwa, akirudi asimkute yule Maza. Jioni kabisa alirudi, tena baada ya kufatwa na mdogo wangu kuwa Kuna ugomvi home, mama anasema yule ni mke mdogo wake( baba), so mshua alikuwa anaitwa akamchukue mchepuko wake na mtoto wa uzeeni. Baba kufika home, anaingia sebleni kwa hasira, anapokewa na kelele. Yule Maza nae anamwambia "Afadhali mkwe umekuja". Ile kauli ya kuitwa mkwe ndo inazidi kumchanganya Baba, Mama nae anaona kama wanamuigizia. Kiufupi pakawa vululu vululu. Kipindi wao wanajiandaa kukaa kikao wajadili vizuri ili swala, yule Maza akawaaga kuwa anaondoka, kikao cha familia hakimuhusu. Akamuacha mtoto, akaondoka wala hana wasi wasi. Mshua wetu jinsi alivyo, akiwa katika hali ya kawaida, akitaka kumuongelea Mama yetu, huwa anatumia maneno kama "Mama fulani", "Kamuite Mama", "Mama yupo?" n.k Ila akishavurugwa, yule anakuwa sio mama yetu tena, bali ni mke wake. Utasikia anasema, nitawafukuza wote nibaki na mke wangu, au oeni mpeleke stress kwa wake zenu, niachieni mke wangu. Kiufupi mshua anamuelewa sana mke wake, na mkewe (Mama yetu) analijua ilo, lakini kizaa zaa nilicholeta kilisahaulisha vyote, mama akawa haelewi kitu.

Ile kauli ya mchuma janga ula na wakwao, hapa ndio niliona. Msala wangu, tabu imeenda kwa familia. So yeyote anayesoma hapa, namshauri awe makini sana na mambo anayofanya, asirudishe mzigo kwa familia.

Wazazi at last walikuja wakaelewana, Ila wakashindwa kuamua kuhusu mtoto. Baba alikua hataki kabisa kukubali kuwa yule mtoto nimezaa na yule Maza. Mama nae akawa anasema kuhusu mtoto, anauhakika kabisa ni wetu, Ila kuhusu mama wa mtoto ndo hawezi sema chochote mpaka Mimi niulizwe. Katika ile story niliyokuwa naelezea hustle zangu, Kuna kipindi nilikutana na mshua ghafla bila kutarajia, alaf mshua akanikazia. Kipindi Mimi namwangalia mshua kwa hudhuni nikitegemea atanionea huruma, kumbe yeye alikua anajaribu kutafakari hii ng'ombe (Mimi) ndo kweli imezaa na yule Maza? Akaniacha nikaendelee kusota kwanza. Alaf alivyorudigi home Wala hakuwaambia kama tulikutana

Hatimae nikarudi nyumbani. Siku niliyorudi home kwa mara ya kwanza toka niondokage, ndo nilijua kuwa kumbe mshua ni kichaa zaidi yangu........
Ila wewe mwamba nimekuvulia kofia, umechekesha sana! Sasa itabidi nyuzi zako nizifuatilie maana si kwa comedy hii [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Pole mzee, majuto ni sehemu ya Maisha. Ukiona hujutii baadhi ya mambo uliyotenda basi kama mwanadamu ambaye ukamilifu wake unategemea udhaifu alionao unakua haupo sawa.
Kama kuzaa ushazaa nae siku moja ongea nae mjadili msatakabari wa mtoto wenu umsikie inakuaje. Usiache damu yako ilelewe na mzazi mmoja wakati wewe U hai.

Akileta ukaidi mshirikishe mzee wako atajua jinsi ya kufanya, kuna familia haziibiwi watoti. Mzee ataongea maneno ya kikurungwa huyo mama atakutafuta mweyewe[emoji4]

Halafu seems like chuki uliyoitengeneza zaidi kwa huyo mama haina mashiko ni kwa sababu uli-Experience Post traumatic stress Disorder (PSTD) iliyosababishwa na wewe kuachwa Mazingira magumu na huyo mama. Jaribu kuangalia the beauty side of her ile uCope with that PSTD.

Sema 25yrs parefu sana mzee[emoji124][emoji124]
View attachment 2215986
Ni kweli usemacho mkuu. Majuto ni kitu cha kawaida kwenye maisha
 
Back
Top Bottom