Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji15][emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]Umetuma kikamilifu kwenda kwa mpokeaji wa Airtel FARIDA BARASS - 0782499138. Kiasi TSh 2,000. Jumla ya Makato TSh 56, VAT TSh 7. Salio jipya ni TSh 6,016. Muamala: 45722404955. Risiti: MI220507.2118.P23881. 07/05/22 21:18.
pole ila ulifaidi kidogoNa hii sio utani, sijivunii mama wa mtoto wangu. Sio kwamba nililazimishwa kuwa nae, hapana. Na katika kipindi chote nipo nae kwenye mahusiano nilikua muda mwingi anatawala mawazo yangu, na hata kuachana kwetu, ni yeye ndio aliniambia muda umefika nikatafute mtoto mwenzangu wa kudate nae. Katika kipindi chote nipo nae, sikuwahi kujua umri wake halisi ni miaka mingapi, Ila makadirio alinizidi miaka kati ya 25 hadi 30. Sijakosea, ilo ndo gape la umri kati ya mimi na mama wa mtoto wangu.
Kati ya vitu ninavyojutia sana, kimoja wapo ni ili tukio la huyu mama. Kitendo cha kukataa shule na kukimbilia mjini, sijawahi kukijutia kama ambavyo najutia kuzaa na huyu Maza. Katika huu Uzi, sito-base sana kipindi cha mahusiano yetu, Ila nitaongelea sana baada ya yeye kufahamika home, maana hapo ndio hasa niliona ukubwa wa ujinga niliofanya. Maana sterehe zangu zilileta mtikisiko kwenye familia, kibaya zaidi sikuwepo home.
Nilikutana nae kwa namna ya ajabu kwanza. Our first meeting alikuwa very harsh kwangu. Baada ya kutimuliwa kwenye nyumba niliyokuwa nafanyia kazi kwa kosa la kumtelezesha mke wa bosi kwenye malumalu, kama mtakumbuka, niliondoka bila kuwa na uelekeo maalum. Ila mwisho wa siku niliangukia buguruni sokoni. Nilifanya sana vibarua pale.
Mazingira yale kulikuwa na bi mkubwa mmoja ana kigrosary chake cha kizushi. Kama ulisoma story yangu, kuna grosary nilikua nakunywa soda, then nikamwambia muhusika abadilishe channel, maana kipindi kilichopo kilikuwa kinanipa machungu, then yule muhusika akanijibu shit. Sasa huyu muhusika/ Maza mwenye kigrosary, ndo huyu nilikuja kuzaa nae.
Wakati nafanya vibarua pale sokoni, sikuwa na sehem maalum ya kulala. Hivyo ningeweza kulala popote katika mazingira yale. Mara chache chache nilikuwa nalala pembeni ya kile kigrosary na jamaa wengine niliowakuta. Kuna siku nilichelewa kuamka, maana tulikuwa na kawaida ya kuamka mapema sana.
Hiyo siku yule Maza alikuta bado mazingira yale, japo sikuwa nimesinzia. Wala hakunikaripia, aliniacha nikaondoka kistaarabu tu. Mida ya jioni, nilikuwa nakatisha eneo lake, akaniita. Akaniuliza wewe ni mgeni maeneo haya, umetokea wapi na imekuwaje unalala nje? Siku ya kwanza nakuona ulikuwa smart, imekuwaje? Ikabidi nimfungukie tu, japo sikumwambia kama nilikimbia home. Nilimsimulia tu kisa cha kutimuliwa kwa yule Mzee niliyekuwa nafanya kazi kwake. Mwisho wa siku akaamua kunipa kazi pale kwenye grosary yake. Tulikubaliana niwe nasaidia manunuzi, usafi, ubebaji na uletaji bidhaa n.k, ujira wangu ikawa ni msosi.
Siku zilivyoenda akaanza kuniamini, nikawa hadi nasimamia biashara yake. Ikafika kipindi akanipeleka mpaka kwake, alikuwa anakaa maeneo ya gongo la mboto, japo alikuwa na makazi mengine kisarawe. Sababu ya misele yake na kazi, ndo maana alikuwa anakaa nyumba ya gomz, sababu ya ukaribu. Baada ya kufanya kazi kwake kwa miezi kama miwili, ndo akanipeleka pale gomz.
Mimi ndio nilikua naamka mapema nawahi kwenye grosary yake kufungua na kuweka mazingira vizuri, then yeye anakuja baadae. Na hata baadhi ya siku angewahi kuondoka kabla yangu, na mara nyingi tuliondoka wote.
Kuna siku alirudi amelewa maana siku hiyo alihudhuria kitchen party. Akilewa ni anaongea sana alaf usumbufu ni mwingi, mara fanya hiki, mara kile n.k. kiufupi anakuwa kama Muhindi kwa jinsi anavyotuma. Hii siku ndio ka mara ya kwanza nilitembea nae. Palivyokucha nilikuwa naona aibu as if wapangaji walijua nilichofanya (alikuwa amepangisha vyumba vilivyobaki).
Hata yeye nilikua naona aibu kumwangalia usoni. Nikawa nakwepa kukaa naye muda mwingi. Yeye akawa ananicheka tu, siku kama ya pili akaniambia najua kinachofanya uwe na aibu. Sikuelewa alimaanisha nini. Ila siku hiyo tulivyorudi home akanipa tena show, kesho yake tena, na tena. Mpaka ikawa rasmi sasa, na ile aibu ikatoka.
Tuliendelea na huu mchezo kwa muda mrefu mpaka ikawa sio Siri tena. Huyu Maza alishawahi kuolewa mara mbili hapo kabla, Ila aliachika kwenye ndoa zote sababu ya mambo yake ya kuendekeza starehe, lakini pia alikua akishika mimba zinaharibika/ zinatoka, so hakuwahi kuzaa. Taarifa zilipokuwa wazi kuwa anatembea na katoto, ndugu zake walikuwa wananichukia , kila siku wanampigia simu, maneno kibao, lakini sielewi alikua na akili gani yule Maza, Wala hakuonekana kujali.
After kama miezi 7 au 8 ya kuwa pamoja, alikuja kushika mimba. Alivyogundua ana mimba, kutokana na historia yake akajua hii haitodumu, so siku moja tunafunga hesabu, akanijulisha kuwa ana mimba, then akaniambia kabla haijatoka, nifanye mchakato wa kutafuta sehemu ya kwenda. Nikashangaa, namuuliza sasa Mimi nitaenda wapi? Akanijibu "We mtoto, Mimi sio mama yako, katafute mtoto mwenzio mfanye maisha"
Kiukweli sikutegemea angebadilika haraka vile. Akili yangu yote alikua kaiteka yeye. Na mpaka leo nikiona mtu anadate na mshangazi/jimama, simshangai. Mashangazi yaoneni tu vile vile. Sikuwa na jinsi, ikabidi siku hiyo nisirudi kwake, nikaamua kutafuta usawa mwingine. Nikamuacha yeye na grosary yake huku akisubiria ile mimba itoke. HAIKUTOKA
[emoji26][emoji26][emoji26]
Ebu tuanzie hapa kwanza. Maana nimewaza mbali sana hapo kwenye mwanya.Na mwanaume ukiwa na mwanya na kiganja kilichokamilika, basi unaweza kumlidhisha mwanamke yeyote yule chini ya jua.
Aisee nmecheka sana hapa.... [emoji2] [emoji3] [emoji1].... Unajua katika kipindi chote cha msoto, sio kwamba sikuwa na mahusiano, la, yalitokea mahusiano mengi tu japo hayakudumu muda mrefu kama ya yule Maza. Hii ilitokana na kutotulia sehemu moja muda mrefu, lakini pia sababu nyingine kubwa ni shimo aliloacha yule Maza. Kila niliyekuwa nakutana nae alikua hatoshi, anapwaya. Huku kujuta ninakojuta sasa, kulianza baada ya yeye kufahamika home na Mimi kurudi nyumbani. Lakini kabla ya hapo nilikua namkumbuka sana, tena Ile ya kumkumbuka then una wish angekua karibu yako. Nahisi wanaosemaga mapenzi yamezaliwa Tanga, hawapajui uzaramuni. Kiufupi yule Maza alikuwa kwenye akili yangu, na hata nilipofahamu kuwa mimba haikutoka na alijifungua salama, nilijihisi furaha.
Unajua mwanamke akiwa hataki kusex, hata umlazimishe vipi ni ngumu kunyanyua hisia zake, sana sana utaishia kumuumiza maana mwili haupo tayari. Ila mwanaume hata uwe umechoka kama punda, mwanamke anaweza kukufanya mwenyewe kwa hiari yako usahau uchovu wako, then ushughurike. Na yeye ndio anachagua umalize baada ya muda gani. Kwa ufupi naweza sema kipindi natoka na yule Maza ni kama vile nilikuwa tuition, maana alikuwa ananielekeza kila kitu, mara fanya hivi, weka kwa hivi, hapa fanya kwa hivi, hutakiwi kufanya hiki n.k. Kwa kupitia yeye ndio nilijua kuwa, kwa mwanamke mwanya ni urembo, Ila kwetu wanaume mwanya una kazi tofauti kabisa. Na mwanaume ukiwa na mwanya na kiganja kilichokamilika, basi unaweza kumlidhisha mwanamke yeyote yule chini ya jua.
** ***
Siku niliyofika home, baada ya mapokezi na ukaribisho mama aliendelea kuniuliza habari za huko nitokako, story za hapa na pale. Hapa ndo nikaanza kuhisi Kuna kitu hakipo sawa. Maana maongezi ya mama yalikuwa hayajanyooka, ilikua ni kama mtu anayelazimisha story ili kuzuia jambo fulani lisitokee. Tulivyokuwa wadogo, Mama alikua akitaka tusisinzie kabla ya kula ucku, basi alikuwa anakupa vikazi vya ajabu ajabu, mara kamwage maji, kalete dekio, sogeza hiki, fanya kile ilimradi usisinzie. Basi hii siku niliyorudi story zake ndio zilikuwa za mtindo huo, kuzuia kitu fulani kisitokee, japo sikuwa nakijua.
Kumbe alikua anajaribu kumblock Baba asipate nafasi ya kuongea na Mimi. Kwa ninavyomjua mshua wangu, akiwa na jambo lake sharti lifanyiwe kazi kwanza, so pale hapakutakiwa kukucha hadi nimpe majibu ya maswali yote aliyokuwa nayo, japo mpaka time hiyo sikuwa najua chochote.
Wakati naendelea kupiga story na Mama, mshua uvumilivu ukamshinda, akatukatisha, "Kama mnataka kuzungumza mje tukae sebleni tuzungumze wote, hata mimi huku nina mengi ya kuzungumza". Mama ikabidi amwambie chakula ndio kinamalizikia kuiva, nile, nipumzike, tutaongea kwa urefu asubuhi. Mshua alivyosikia habari za kuongea asubuhi ikabidi aje jikoni na yeye. Mzee wangu huwa haingiagi jikoni, Ila siku hiyo aliingia. Mama akamwambia kama amechoka sana alale, then asubuhi ataongea na Mimi vizuri. Baba akawa mkali "Yani mtu alitaka kuniulia mke wangu alafu nisubirie mpaka asubuhi ndo nimuulize wakati namuona hapa?". Ile kauli ikanishangaza kidogo, alaf nikahisi labda kwavile niliondokaga home bila wao kujua nimeenda wapi pengine ilimpa Mama presha, ndo maana Baba anasema nilitaka kumuua mkewe. Kumbe bhana kile kizaa zaa kilichotokana na yule Maza kuja home, summary ya mshua ni kwamba nilikua na lengo la kutaka kumuua mkewe. Dada ndo alikujaga kunipa story kuwa baada ya yule Maza kuwasusia mtoto na kusepa, ilibidi wao kama familia wajadiliane inakuwaje kuhusu hatma ya mtoto. Mama na Dada wakawa wanasema hawana jinsi, yule mtoto itabidi familia imlee, Mshua akawa anapinga kuwa arudishwe kwa yule Maza.
Ilibidi na kaka zangu wengine waitwe pale home kujadiliana namna gani lile linatatuliwa. Maana Baba alishaamua mtoto arudishwe Dar. Mpaka siku hiyo ya kikao, zilishapita kama wiki mbili tokea yule Maza aondoke, lakini mshua alikua bado hataki kuamini kama nimezaa na yule Maza. Yeye fikra zake ni kwamba nilitia mimba alafu kwa uoga, nikakimbia. Sasa yule aliyekuja na mtoto ni mama wa Binti niliyempa mimba. Baba akawa anawashauri inabidi Mimi nitafutwe, then taratibu zifatwe ili Binti niliyezaa nae akabidhiwe kwetu kihalali. Dada akajiribu kuwaambia kuwa kwa jinsi yule Maza alivyokuwa anaongea nae, ni dhahiri yeye ndio mama wa mtoto. Kaka yangu mkubwa akasema kwa jinsi Dunia ya sasa ilivyo, kuchaguliana mke au mchumba ishapitwa na wakati, kwavile dogo (Mimi) amechagua, huyo ndo shemeji yetu, sioni tatizo juu ya ilo. Kauli za "shemeji", "wifi" na "mkwe" Baba ndio alikua hataki kuziskia kabisa. Mwisho wa kikao, wakaamua Dada akakae nae, mpaka akue kue kidogo then ndo ataenda kuishi pale kwa Babu na Bibi.
* * ****** ***
Mimi nilivyorudi nyumbani, yule mwanangu hakuwepo, alikuwa bado anaishi kwa Dada. Baada ya Mama kushauri niulizwe asubuhi, Baba alikubali. Usiku ule tukaongea habari tofauti kabisa. Kulivyokucha, katika story ndo akaniuliza kama katika movements zangu sijaacha mtoto sehemu, yani alianzia mbali sana, nahisi alitaka kuona nitasemaje. Mimi nikamuelezea tu kuwa nina mtoto wa kiume Dar. Baba akaniambia "Mtoto sio shida, vipi kuhusu mama ake? " The way alivyo uliza tu nikikumbuka na hali ya jana yake usiku, nikahisi kuna kitu akipo sawa. Ikabidi nimuwahi kwa kumwambia ukweli, maana Mzee wetu jinsi alivyo, kwa sisi watoto wakiume, tukikoseaga huwa anatengeneza mazingira ya kupigana. Na ikitokea hiyo chance, bila mama kuingilia, anaweza akakuua.
Wakati naendelea kujielezea, akanikatisha "Hebu ngoja kwanza legend, hivi unajiskia unachokiongea?" Nikashangaa ilo jina la legend. Mshua sasa kujizuia kukaisha, akaanza kutema nyongo. "Hivi unajua yule Maza kama angekua kazaliwa familia ya Mama ako, basi angekua mtoto wa pili kama sio wa kwanza" " Wadogo zake mama ako hakuna hata mmoja anayempata kwa umri", " Hivi ule unene wake ndo ulokuchanganya au?" Mzee aliongea sana, akawa anasema watoto wake wote wamerithi tabia kwake, sijui ilikuaje Mimi nikarithi ujombani. Ile kauli Mama akaamua kuitolea ukimya "Yani ukoo wenu (wa baba) ulivyo na damu kali, Sina hata mtoto mmoja aliyefata kwetu, tena mmeniharibia hadi Binti yangu na pua zenu zisizojua kujificha, tafuta namna nzuri ya kuelewana na mwanao, ujombani hapahusiki". Kauli ya Mama bado kidogo inifanye nicheke, nikajizuia, ila mshua akakiona hicho kitendo. Sijakaa hata sawa, alinivaa mzima mzima, akanipiga kichwa cha kifua. Wote kama tulivyo tukaenda mpaka chini. Sijakaa sawa, akaniweka kichwa kingine cha uso tukiwa pale pale chini, nataka kujiweka sawa, akaniwahi na kabali. Mzee wangu hana pumzi, ila ana nguvu sana za mikono, maana tushapigana nae mara kadhaa. Kitendo cha yeye kuniwahi na kabali, nikajisemea kimoyo moyo, "Leo hapa Mama asipoingilia nakufa". Nilijitahidi kadiri nilivyoweza, Ila wapi. Mama nae baada ya kuona tunapigana, akataka kuja. Kumbe Mzee alishajua anachotaka kufanya, so aliacha kamfungia Mama kwa nje. Mama ametoka jikoni mbio ili aje nje kuamulia, anakuta mlango wa nje umefungwa, zunguka upande wa pili, nako hivyo hivyo. Akasogea dirishani anabwata tu. Mzee alinipiga kabali mpaka nikanya. Alivyoona hali yangu tete ndo akaniachia, then akanyanyuka fasta, akakunja ngumi kwa ajili ya pambano rasmi. Mama analalama "Utaniulia mwanangu" Baba anamjibu "Huyu sio mtoto, alichelewa tu kuzaliwa, acha niende nae sawa". Muda huo Mimi ndo natafuta pumzi maana nilikuwa hoi, faza wala hajali ndo kwanza anarusha ngumi. Alinipiga moja kwenye jicho, sitokaa niyasahau yale maumivu. Ikabidi nianze kujitetea, Ila nilichezea sana vitasa vya tumbo na mbavu. Mzee alipoona pumzi inamuishia, akaanza kutafuta namna ya kunipiga kabali tena ili avute pumzi, nikawa nishamsoma maana ndio ilikua kawaida yake, mkipigana anakuwahi kwanza kwenye pua ili kukukata moto, so nikawa naichunga pua yangu, na yeye anachunga yake. Huku na kule, akanipiga tena kwenye jicho lile lile, sijakaa vizuri,akanipiga mtama then akaniwahi na kabali. Nikaona hapa nisipokuwa makini nakunya tena
Muda huo Mama anahaha tu dirishani, kelele zake zinamezwa na kelele za mifugo. Na eneo letu ni kubwa, majirani wako mbali. Dingi nae ndio kwanza anazidi kukaza mikono......
Narudi kumalizia....