Sad Truth: Sijivunii na mama wa mtoto wangu

Najaribu kuwaza huyo mwanamke uliyezaa nae ana mwonekano gani mpaka baba alivyomuona na kusema umezaa nae akatoka nyumbani bila kuaga[emoji1][emoji1][emoji1]

Atakuwa mnene,mfupi na mweusi halafu kajichubua ngozi[emoji1][emoji1]

Nimecheka sana leo
 
Najaribu kuwaza huyo mwanamke uliyezaa nae ana mwonekano gani mpaka baba alivyomuona na kusema umezaa nae akatoka nyumbani bila kuaga[emoji1][emoji1][emoji1]

Atakuwa mnene,mfupi na mweusi halafu kajichubua ngozi[emoji1][emoji1]

Nimecheka sana leo
Ni limama mkuu.
Mpaka baba yake aliliogopa usifanye mchezo

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kabla hatujafika mbali nakuomba unipe somo kuhusu mwanya jinsi ya kutumia maana naona nipo nao afu hauna mchongo.Labda ni muda sasa wa kuutumia
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah!!!!
 
...... Mzee wetu alikuwa na kawaida moja, ukitokea msala alafu Mama akaupoza. Hapendagi kumbishia, Ila next time ukiingia kwenye 18 zake atakupa kipigo na cha msala uliopita. So, hiki kipigo kilichokuwa kinaendelea muda huu, ilikuwa ni majumuisho na ule msala wa kuondoka home. Mzee alikua anakaza mikono kadiri anavyokumbuka matukio niliyofanya, ikafika hatua sauti ya Mama nikawa siiskii kabisa, nikaona hapa sasa nakufa. Katika kujitetea ikabidi nimng'ate, nilikaza meno mpaka akaniachia. Kawaida ya mshua akishakuachia, wakati ww unahangaika kuvuta pumzi, yeye anawahi kusimama ili akurushie ngumi za mfululizo. Alivyoniachia tu, sikutaka hata kusubiria, nikatoka nduki, mshua akaunga tela. Tukaanza kufukuzana kuizunguka nyumba. Mama nae kule ndani anafanya kazi ya kuhama madirisha tu, mara yuko dirisha ili, mara lile kutegemeana na sisi tuko upande upi. Round moja tu, Mzee akakaa chini, na Mimi nikatulia upande niliokuwepo kwanza navuta pumzi.

Mzee akaamua kuingia ndani, me nikaenda zangu kuoga then tukarudi kuendelea na kikao Mimi na Yeye. Safari hii Mama hakutaka tuongelee nje tena, tukakaa sebleni. Mama akatuletea chai, tukawa tunakunywa huku tunapiga story sasa.

Mzee ananiuliza "Unakunywa pombe?" Nikajibu hapana."Unavuta bangi?" Nikajibu hapana. "Sasa ilikuwaje ukachukua lile tank? Akili yako ilikua wapi?". Nikakosa jibu la kumpa, nikawa mbali kimawazo. Akaendelea tena"Hivi huu ujasiri uliutoa wapi haswa, mbona hufanani na ndugu zako?" Mama akadakia "Hafananii na ndugu zake, anafanana na wewe, inamaana ushajisahau?" Mzee nae akawaka "Walau Mimi (Mshua) nilichukua mtu wa umri wangu" ( Unajua Bi mkubwa wangu nae amejaa jaa, japo ni mdogo kiumri kwa Baba). Mama nae akamjibu " Swala sio kuchukua wa umri wako, kwani wakati unanifata ulijuaga umri wangu, we siuliangalia kilichokuvutia?. Mwanao ashakuletea mkwe, inabidi umkubali tu"

Lile neno mkwe likaonekana kumkera Mzee. Unajua Mama yetu wala sio mtu wa kukaa na kitu moyoni. Muda huu anajibizana na Mzee, Yeye Mama alikua anatabasamu kabisa, Ila Mzee kakunja ndita. Battle ikatoka kwangu, ikahamishiwa kwa Mama, Mzee akaanza kumwambia Mama yeye ndio chanzo cha yote haya. Mshua akamwambia Mama "Nilikwambia tuzae mapema ukawa unasema tusubirie subirie, matokeo yake mtoto alikuwa anakulia kiunoni, huyu kazaliwa akiwa mtu mzima" Unajua katika familia yetu, watoto waliotangulia wote wamepishana miaka miwili miwili kasoro kaka yangu ninayemfuata amenizidi miaka 7. So alichokuwa anamaanisha Mzee ni kwamba hiyo miaka 7 yote ambayo walikuwa wanasubiria, Mimi nilikua naendelea kukua tu, dah [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Anyway, msala ulikuja ukapoa tukaongea kistaarabu, Ila Mzee alikuwa so disappointed. Akawa ananiambia kuwa anastaili kujifunza toka kwangu maana Mimi ni legend, Nina namna zangu za kurun things ambazo hajawahi imagine.

Alinipa ushauri wake kuhusiana na mambo mbali mbali. Ila katika maongezi nae ndio nikagundua kuwa watu wetu wa karibu huwa wanaumizwa sana na mambo ya ajabu tunayofanya. Ile kauli ya mchuma janga ula na wa kwao, ilidhihirika mbele yangu. Sema kwavile ilishatokea hapakuwa na namna. Kutokana na hiki kisanga Mzee wangu ni mara chache sana kuniita jina langu,mara nyingi ananiita legend. Sipendagi akiniita hivyo, Ila Sina namna ya kumzuia, niliyataka. Mara chache chache huwa ananitania kuhusu yule Maza, now days anachukulia as a joke tu. Ananiambiaga nikiamua kuoa, nisisite kuwajulisha. Ila wao hawatonipush maana wanahofia nisije kuwafanyia surprise nyingine

** ********* ****** ***

Tukafunga huo ukurasa kuhusu mtoto na yule Maza. Ndio tukaanza kuongea kuhusu harakati zangu zingine. Alitaka kujua ilikuwaje tukakutana pale Magingo kwenye soko la tangawizi. Nilimuelezea kwa ufupi mizunguko yangu mpaka kufikia ile siku tunaonana, Yeye akiwa kama Boss, Mimi nikiwa kama kibarua..

Nadhani hayo Sina haja ya kuyaongelea hapa, maana nilishayaelezea kwa urefu sana kwenye ule Uzi safari yangu.



** *** ***** ***

Kwa sasa dogo alishatoka kwa Dada anaishi kwa Babu na Bibi yake. Yule Maza sina mawasiliano nae, japo kwasasa anaishi nyumbani kwake Kisarawe. Mpaka now inanipaga ukakasi nikiingia kwenye mahusiano kujielezea kuwa nina mtoto, hasa kuepuka swali la mama yake yuko wapi? Kwanini mliachana? Akirudi je? n.k

So, kwa kifupi sipo nae (maana najua ili swali litaulizwa tu). Dogo hajawahi kumuulizia Mama yake, labda kwavile walitengana akiwa mdogo sana so hakupataga ile bond ya Mama. Yule Maza nilishawahi kutana nae mara moja maeneo ya mawasiliano ubungo, tuliongea mawili matatu kuhusu mwanangu, then kila mmoja akaendelea na safari yake. Namba yake ninayo, pia anayo yangu japo hatuna mawasiliano.Huyu Maza hakuwahi kupata mtoto kabla ya huyu, nashangaa kwanini aliamua kumpeleka home kwetu, nilitarajia angemng'ang'ania kama dhahabu, but haikuwa hivyo.

Anyway, hiyo ndio ilikua story yangu. Until next time,

Regards;

Analyse
 
Na kwa uandishi mzuri wa jamaa, nahisi kama ni story ya katunga tu [emoji1]
Nikiwa na content yangu ambayo nataka kuiwasilisha, napendaga kuiweka katika namna ambayo hata mtu mvivu atalazimika kusoma. Maisha yanaboa, nikikusimulia life events zangu ktk namna ya kuboa, utaboreka zaidi

Tunaishi kujifunza.
 
Najaribu kuimagine mwamba Analyse alivokua anaelekezwa kutumia "mwanya".. laiti angejua later anaenda kupigwa kabali ya kumwaga kimba, angekimbia spidi ya bolt
Why nikimbie mkuu? Somo lile huwa linaeleweka kiwepesi sana, na mwanafunzi hawagi mbishi [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Najaribu kuwaza huyo mwanamke uliyezaa nae ana mwonekano gani mpaka baba alivyomuona na kusema umezaa nae akatoka nyumbani bila kuaga[emoji1][emoji1][emoji1]

Atakuwa mnene,mfupi na mweusi halafu kajichubua ngozi[emoji1][emoji1]

Nimecheka sana leo
Alaf sio kusema ni mbovu hapana. Mimi mwili wangu ni mdogo, alaf yeye ni mnene na amepanda hewani, alafu mweupe. So mtu yeyote ukimwambia nilikuwa napush ule mwil, ni ngumu kuamini. [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…