Sad: Zari, Diamond waipasua familia ya Ivan, Baba Ivan aongea kwa uchungu

Sad: Zari, Diamond waipasua familia ya Ivan, Baba Ivan aongea kwa uchungu

Kwa ufupi mzee anasema kuwa Ivan kafa kwa sababu ya depression ambayo alikuwa nayo kwa muda wa miaka 4, ambapo alikuwa hasikii chochote anachoambiwa na wazazi. Anasema Zari alikimbia na tayari ana watoto wawili kwa mume mwingine kwa maana hiyo hana mgawo wowote. Anasema kuwa wajukuu vitu vyao viko kwenye mikono salama.
 
Yaani unaweza kuokota panga ikamfyeka mtu miguu, mtu kakuacha mpaka umekufa ndio anarejea kusaka pesa daadek, Hya maisha haya wanaume tujifunze jitu kama Zari linaonekana roho mbaya sana jamaa yupo ktk frizzer wao wanakomaa na mali? Mungu tusaidie na utukumbushe kutumia vyema mali zetu maana kitakachokufaa siku ukifa ni kile kilichotolewa ktk njia yako
Kweli mkuu uko sahihi
 
Sasa mbona huyu aliwakimbia zamani sana watoto wake mpaka akaenda kuzaa wengine nje, ila kama kuna kitu zari anajilaum kwa sasa ni kitendo cha kuzaa tiffa na nillan maana angekuwa hakuwazaa labda kidogo angekuwa na nguvu ya kupata urithi
Hao watoto alikuwa anaishi nao labda hapo kwenye kuzaa wengine, Hiyo ni changamoto mkuu pale mahusiano yanapovunjika na hasa kama una watoto.....na ni nguvu kuwa na mahusiano mapya ya wazi bila kuwa na katoto ka kuwaunganisha...ila ukirudi kwenye hali halisi bado watoto wana haki ya kupata stahi yao kutokana na jasho la baba yao, hapo changamoto inakuwa nani atasimamia show mama yao au ndugu wa baba yao wakati huo huo muda mwingi watoto wapo na mama yao though wakati mwingine wanakwenda kwa mdingi wao (hapo sasa ndio huwa wanandugu hasa sie wabantu tunapokuwa wagumu kuwakabidhi mali watoto ila wawe chini ya uangalizi wa mama yao)
 
Familia zetu nyingi bado zimeegemea kwa ukoo wa baba. Kwa hivyo hata hao watoto pengine ndugu mojawapo wa Ivan atawachukua au ndugu wanaweza kuamua kugawana. Angekuwepa baba wa Ivan pengine wangekaa kwa babu yao. Na pengine suala hili linakuwa gumu zaidi kwa sababu Zari tayari kaolewa na mwanaume mwingine.

So issue kama unavyosema, ndugu wa Ivan pengine watajiuliza wamwache Zari achukue mali za ndugu yao ampelekee Diamond?
Inahitaji busara sana ila tuliolelewa na mama kutokana na changamoto kama hizi za mzazi mmoja amefariki mapema kiukweli tuna practical experience kama mama akiachiwa watoto aelee ila kikubwa awe anajielewa na ana uwezo wa kulea familia..mara nyingi sie ndugu wa kiume huwa tunawachukua watoto wa ndugu zetu ila tunasahau kwa upande mwingine tunaishi na wake zetu ambao kwa namna moja ama nyingine wanaweza wakawa kikwazo kwa kushangaa kwanini mwanamke mwenzake asipewe watoto (kwani hata yeye moyoni anawaza endapo mumewe ataondoka atapenda yeye a-take care watoto wake.

All in all ...ukiwa age flani na watoto wakiwa age flani plus changamoto za maisha ni vyema wosia ukaandikwa pamoja na kuwajengea maisha watoto ikiwa pamoja na ku-deposit kiasi flani cha hela kila mwezi hata kama ndugu wakileta figisufigisu mambo yanakwenda sawa though kwa hiyo familia inaweza ikawa sio issue kuhusu mali ila watoto ambao hawajui chanzo cha mgogoro kati ya mama yao na marehemu baba yao wanatakiwa waachwe katika style ambayo pande zote mbile zinakuwa kimbilio yaani hata kama mama ameonekana hana haki lakini mwisho wa siku wamwone mama yao ana furaha lakini pia upande wa ndugu wa baba upo happy ili mwisho wa siku iwe rahisi kwao kujimuvuzisha kila upande freely
 
Zari alishakiuka sheria ya ndoa na mirathi,hakuna sheria inayorohusu mtu aliyekwisha zaa na mme mwingine kurithi mali ya aliyewahi kuwa mme wake,Ivan kwa Zari ni Co_Parent basi,warithi halali ni watoto wa Ivan ambao basdae wanaweza mtunza mama yao.

Hakuna sheria inayoamini kama Zari hatatumia mali za Ivan na mme wa sasa aliye naye,ukitumia mali ya marehemu na mme mwingine na watoto wa mme mwingine kisheria hao ni wezi.

Cha msingi kama marehemu hakuacha wosia,ukoo utakaa utachagua msimamizi wa mirathi ambaye atafungua shauri la mirathi mahakamani.Akikubaliwa ataruhusiwa kukusanya mali za marehemu na kuzigawanya kwa watoto wa marehemu.Kama watoto ni wadogo msimamizi wa mirathi anaruhusiwa kutunza hizo mali mpaka watoto wakue,msimamizi wa mirathi sio mrithi.

Nawashauri vijana acheni kuoa mke aliyeachana na mme wake na haeleweki kama kweli wameachana au la!

Nimeaona mtandaoni Zari na Ivan walitengana mwaka 2014,mwaka 2015 akazaa mtoto wa kwanza na Diamond,upo uwezekano wa kuaminika kuwa Diamond ndiye alivunja ndoa ya Ivan.

Inawezekana Zari na Ivan wangerudiana baada ya ndoa kutenguka kama sio Diamond.Kwa wanaume ambao si wapotezeaji Ivan alikuwa na haki kisheria kumshitaki Diamond kwa kumuibia mke na Diamond angewajibika.
Mshika mbili,, ,, .......Kwa sasa Zari atulie na mtu wake wa sasa,amuombe alee na watoto wa Ivan.Afrika haku polyhandry marriage ya mwanamke kuolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja.
 
Baby wa Ivan amesema Zari ndio atasimamia mirathi,according to post moja huko juu,Wao wamesema pesa iko damuni.
 
Mie hili nililiona kitambo kwa huyu kijana wa Tandale, nilijua tu kaingia choo cha kike huu ni mkenge keshauvaa...kiuhalisia mali za Ivan zinatakiwa kurithiwa na watoto baasi hapo Zari hana lake apige lapa tu kukomaa na za madale.
 
c67b1b684d85722b36942e7135666878.jpg
 
Mnatoana Roho Yarabi iiiii, kwa Mali Alizoacha Babaaaaa! Mali za Baba Zinawatoa Roho, Bora Mimi Nikae Peembeniiii!!

Kweli huu, wimbo umeingia kwenye misemo ya Wahenga, kwa kitendo hicho kinachofanywa na familia ya Ivan na Zari.

Hivi kweli Jamani, jina lenyewe halikufanyi mtu umuogope mtu huyo!?

"ZARI " hivi maana ya Zari hapo bongoland si itakuwa ni msala, timbwili, fujo majanga ya mtafaruku hivi!?

Ama, kishwahili ndiyo kinaanza kuniponyoka!!?

Mpenzi, FaizaFoxy , njooooo, neno ZARI linanitoa nishai hapa 🙂🙂🙂🙂

WAAFRICA KWELI WAJINGA "MTOTO WA BILLGATE ANASOMA AENDELEZE MALI YA BABA YAKE WATOTO WAKIMASIKINI WANATAKA KULISI NYUMBA NA MAGARI MABOVU .... TUMIENI AKILI
 
Mnatoana Roho Yarabi iiiii, kwa Mali Alizoacha Babaaaaa! Mali za Baba Zinawatoa Roho, Bora Mimi Nikae Peembeniiii!!

Kweli huu, wimbo umeingia kwenye misemo ya Wahenga, kwa kitendo hicho kinachofanywa na familia ya Ivan na Zari.

Hivi kweli Jamani, jina lenyewe halikufanyi mtu umuogope mtu huyo!?

"ZARI " hivi maana ya Zari hapo bongoland si itakuwa ni msala, timbwili, fujo majanga ya mtafaruku hivi!?

Ama, kishwahili ndiyo kinaanza kuniponyoka!!?

Mpenzi, FaizaFoxy , njooooo, neno ZARI linanitoa nishai hapa 🙂🙂🙂🙂
Mila za waafrica hamzujui uondoke ukaolewe huko, alafu urudi useme nina changu hapa,hupati kitu wanahofia utaenda kutapanya mali za ndugu yao na mwanaume mwingine.Hata hapa Tanzania ufiwe tu na mume alafu wakuone unaingiza mwanaume kwenye nyumba ya ndugu yao unatimuliwa.
 
Back
Top Bottom