Sadaka katika mtazamo wa kiroho

Sadaka katika mtazamo wa kiroho

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Sadaka ni tenda la kiimani la kiroho .. Sadaka haitolewi kwenye nyumba za ibada tuu.. Hizi zenye imani juu ya Mungu moja na dini zake
Sadaka pia hutolewa kwa miungu
Sadaka pia hutolewa na wapagani
Sadaka pia hutolewa kwenye vilinge vya mambo ya giza
Sadaka pia hutolewa kwa masanamu
Sadaka pia hutolewa kwa shetani
Blla kujali ni aina gani ya sadaka, ama ni kwa imani gani ama inatolewa kwa nani.. Sadaka ina sehemu yake rasmi na pekee ya kutoka.. Nayo inaitwa madhabahu

Sadaka haina mwakilishi
Sadaka haitumwi kwa njia ya mtandao.. Mhusika mtoaji ndiye anyepaswa kwa miguu yake asogee madhabahuni kwa miguu yake na kwa mikono yake atoe/aweke sadaka yake kwenye chombo maalum na rasmi kwa kazi hiyo tuu
Waendao kwa waganga wanalijua hili. Ukifika pale unawekewa chombo utoe ulicho nacho.. Hupangiwi
Huku kwenye imani zetu na hata kwa waganga ukishawekewa namba ya kutuma sadaka jua umeliwa

Katika sadaka kuna makundi mawili makubwa
Sadaka mfu
Sadaka hai

Sadaka mfu ni zipi?
Ni sadaka zisizo na faida, zisizo na matokeo, zisizo na baraka
.Sadaka za kutuma kupitia mitandao
.Sadaka zitokanazo na chenchi za pombe
.Sadaka zitokanazo na malipo haramu kama mauaji, rushwa nk
. sadaka za mafarisayo.. Kumbuka sadaka ni tendo la siri
Katika hilo kundi la sadaka mfu. Kuna sadaka zenye kasoro ama ambazo hazijatimia.. Ni zipo hizo?
Chocolate chenye kasoro hakifai kutolewa kama sadaka
Mganga hapokei kuku zezeta haya ya kufugwa
Mchawi hachukui noti mbovu hasa iliyopungua kipande.. Mchawi harogi mlemavu
Kwenye imani za kishetani.. Kuhani hulala na wanawake vigoli tuu..
CC: Shimba ya Buyenze
Inaendelea
 
Acha tuendelee kujiunganisha na madhabahu ya kinabii hata kama tupo Ngara
Dar na Ngara kitechnojia ni Kijiji
Acha nabii apige sadaka
 
Tuendelee
Kama tukirejea kwenye maandiko ya Biblia tunaona makasiriko ya Mungu pale Kaini alipomtolea Mungu malimbuko yasiyo bora

Sadaka hai ni zipi?
Bila kujali unamtolea nani na unatoa wapi.. Ili sadaka yako ipate chaji ya kiroho na ilete uhai na matunda tarajiwa
.Itoe mahali sahihi
.itoe kwa usahihi
.Hakikisha haina mawaa
.Hakikisha unaitoa kwa moyo mmoja, bila kushurutishwa, bila kutishwa na bila kupangiwa

Kuna makundi ya sadaka mbalimbali kwa sababu mbali mbali
Sadaka za kila wakati
Sadaka za vipindi maalum
Sadaka za mahitaji maalum
Sadaka za shukrani
Sadaka za malimbuko sahihi

Mababu wa mababu zetu walitoa sana sadaka kulingana na mahitaji mbali mbali
Sadaka za kuomba mvuta (ibada za matambiko)
Sadaka za matendo ya fanaka
Sadaka za kuomba mabaa mbali mbali yaondoke
Sadaka za kinga
Sadaka za upatanishi ni

Kwakuwa sadaka ni tenda la kiimani na la kiroho hivyo hutolewa madhabahuni kupitia ibada rasmi
Bila ibada bila uwepo wako sadaka yako haina maana yoyote

Zamani za babu wa babu zetu madhabahu zilikuwa kwenye miti mikubwa, majabali makubwa ama mahali rasmi palipoandaliwa kama ni msituni pembeni ya mto nk
Siku hizi tuna vilinge na nyumba rasmi za ibada zenye mahali rasmi pa madhabahu na vyombo rasmi vya sadaka!
Je ukubwa na udogo wa sadaka vinaweza kuathiri matokeo?
Jibu ni ndio.. Kutoa kikubwa haimaanishi utabarikiwa sana kwakuwa unatoa kikubwa kwenye nini?

Zaidi soma
Naweka pozi kidogo
 
Endelea kutuelimisha ndg Sangoma msitaafu
 
Tumeshindwa sana kujua maana ya sadaka. Sadaka ni agano. Watu wengi hupoteza sana kwa kutojua kwanini wanatoa sadaka. Sadaka sio zawadi kwa Mungu, ni agano na inapaswa kuwa umeshaweka agano hilo kabla hata ya kutoa sadaka yako. Baada ya hapo ndipo unatoa sadaka yako ambayo ndio inakuwa kama alama au mhuri wa agano lenyewe. Na unapaswa kujua nini cha kufanya baada ya kutoa sadaka yako.
 
Itishe kusema, sikuweka nadhiri ila nilibadili mtindo wa maisha nikaanza kutoa sadaka kwanza kwenye kila pato langu na iliyobaki ndo nilianza kujipangilia maisha yangu.

Imenilipa/nimepata fadhila nyingi mahala ambapo sikutegemea hadi leo, niliweka imani na bado nina imani kubwa sana juu ya sadaka.

Kadri uonavyo nafsini mwako, ndivyo unavyopokea ama kupata.
 
SADAKA ni kitu chochote chenye THAMANI kwake yeye anayetoa si anayepokea kinachotolewa kwenye madhabahu pasipo kuhakiki matumizi yake(mfano ukitoa sadaka hutakiwi uifuatilie kuhoji imetumikaje ,wewe umetoa kwa Mungu sio kwq mwanadamu) ili kuweka agano litakalo tambua hatima ya maisha yako mtoaji.

SADAKA yafaa
1)iwe na thamani kwako mtoaji(sadaka ya Habili,mwanamke mjane
2)utoe kwa kupenda kama ulivyokusudia moyoni mwako si kwa lazima si kwa huzuni
3)kwa imani na isiyo na mashaka na kwa uaminifu(anania na mkewe safira hawakutoa kwa uaminifu wakafa,ni bora wasongetoa sadaka au wasingedanganya wasingekufa
4)Kwa heshima na unyenyekevu sio kwa kujisifu (watu wawili walishuka hekaluni kusali mfarisayo na mtoza ushuru--mfarisayo akaanza kujisifu mbele za Mungu kimoyomoyo kwa sadaka zake na matendo yake,mtoza ushuru alinyenyekea akajiona hastahili ni mwenye dhambi akaomba toba na rehema.(mwisho wa ibada aliyehesabiwa haki ni mtoza ushuru kwa unyenyekevu wake na si mfarisayo kwa sababu ya pride yake ego pamoja na kuwa alikuwa mtoaji wa sadaka mzuri na kufunga/fasting juu ila PRIDE EGO ilimuangusha
5)SI kwa kujionyesha mbele za watu ili usifiwe ukiweza kutoa kwa siri ni vizuri zaidi ili Mungu aonaye sirini akupe thawabu
6)kwa moyo safi usio na kinyongo na mtu(kama ukifika madhabahuni kumtolea Mungu sadaka ukakumbuka kuna mtu umekosana naye hamko sawa naye iache sadaka madhabahuni nenda kapatane naye kwanza ndipo urudi kumtolea Mungu sadaka

NGUVU YA SADAKA
Sadaka inaongea ina nena mema,sadaka inakuwa ukumbusho mbele za Mungu
KORNELIO sadaka zake zilifika mbele za Mungu na kuwa ukumbusho
Inapatanisha,inatakasa,inakomboa,inakupa baraka katika mambo yako yote ulinzi wako na mali zako,
IBADA IKIAMBATANA NA SADAKA ni vyema zaidi inakuwa na nguvu zaidi mtu asijitokeze mbele za Bwana mikono mitupu.
Ingawa tumeokokewa kwa neema kwa Yesu kufanyika sadaka kwa ajili yetu,na si kwa vitu viharibikavyo so fedha wala dhahabu.
Mungu mwenyewe alitoa sadaka yenye thamani kwa kupenda akamtoa Yesu afe msalabani ili kutuokoa.Hii inatukumbusha pamoja na hayo tuwe wanyenyekevu(tujione kuwa hatustahili ila tumestahilishwa,sio wakamilifu,ni wenye dhambi) kwa Mungu tuombe toba na rehema yake tusijisifu kuwa sadaka zetu pekee tunazotoa ndio zinatosha kutuokoa au kwa matendo yetu mema sana ila Yesu pekee anatosha kutuokoa kwa neema yake.Ukumbuke ulimwengu ikiwemo dunia na vyote vilivyomo ndani ya ulimwengu na dunia ni MALI YA MUNGU.Tinamtolea Mungu shukrani sadaka sehemu ya vingi alivyotubariki.Mungu ni tajiri.
pamoja na na hayo bado sadaka ni muhimu kama ikitolewa kwa namana nzuri kwa usahihi madhabahu sahihi.MTU ASIKUDANGANYE SADAKA HAINA UMUHIMU KWA AGANO JIPYA eti kwa vile Yesu alishafanyika sadaka kwa ajili yetu.sadaka ni muhimu sana sana.
Hakuna aliyehai ambaye hana sababu ya kumtolea Mungu sadaka hata ya shukrani kwa uhai tu.Hakuna ambaye hana uwezo au kitu cha kutoa sadaka .HATA MASKINI NA WANAWAKE TENA WAJANE wana kitu cha kutoa sadaka(mfano wa mwanamke mjane alitoa sarafu mbili za fedha na bado Mungu alizipokea na kuona zilikuwa na thamani kwa sababu zilitokewa na maskini,mwanamke ,mjane ambaye alikuwa nazo hizo tu bila ziada na akazitoa zote sadaka.Kumbuka biblical time wanawake walichukuliwa kama kundi la wenye mahitaji wahitaji maalumu wanyonge wasiojiweza ,sasa huyu alikuwa mwanake tena MJANE na MASIKINI lakini alitoa sadaka Hata wewe una sababu na uwezo wa kutoa sadaka.
 
Itishe kusema, sikuweka nadhiri ila nilibadili mtindo wa maisha nikaanza kutoa sadaka kwanza kwenye kila pato langu na iliyobaki ndo nilianza kujipangilia maisha yangu.

Imenilipa/nimepata fadhila nyingi mahala ambapo sikutegemea hadi leo, niliweka imani na bado nina imani kubwa sana juu ya sadaka.

Kadri uonavyo nafsini mwako, ndivyo unavyopokea ama kupata.
Sadaka ina NGUVU sana
 
Sadaka ni tenda la kiimani la kiroho .. Sadaka haitolewi kwenye nyumba za ibada tuu.. Hizi zenye imani juu ya Mungu moja na dini zake
Sadaka pia hutolewa kwa miungu
Sadaka pia hutolewa na wapagani
Sadaka pia hutolewa kwenye vilinge vya mambo ya giza
Sadaka pia hutolewa kwa masanamu
Sadaka pia hutolewa kwa shetani
Blla kujali ni aina gani ya sadaka, ama ni kwa imani gani ama inatolewa kwa nani.. Sadaka ina sehemu yake rasmi na pekee ya kutoka.. Nayo inaitwa madhabahu
Kwa maelezo ya maandiko ni kwamba, Mungu alimtoa mwanae wa pekee sadaka ili kutukomboa na dhambi zetu.
Kama Mungu ndiye mkuu wa vitu vyooote ulimwenguni, sifa na ukuu na kila aina ya nguvu ni zake. Sasa alitoa sadaka yake kwa nani!?
 
Sasa kwenye SADAKA anayembariki mtoaji ni yule MPOKEAJI anapo shukuru au ni MUNGU?

Huyu mpokeaji yeye ananafasi gani kwenye hii sadaka? ni myororo tu wa kuwapa BARAKA watoaji?

Kuna MATAIFA tajiri hutusaidia, yani hutoa kwenye sehemu ya Kodi za wananchi wao na kutusaidia sisi, hii nayo sadaka, Je, anayebarikiwa ni TAIFA hilo, au wananchi wake, ama ni kiongozi wa nchi hiyo?

Ni sadaka gani hasa inapokelewa na yenye baraka zaidi?, Nguo, chakula au Pesa?
 
Back
Top Bottom