SADC yapoteza mawaziri 10 kutokana na Covid19, Tanzania tumejipangaje?

SADC yapoteza mawaziri 10 kutokana na Covid19, Tanzania tumejipangaje?

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mpaka sasa nchi wanachama wa jumuiya ya kikanda ya kusini mwa Afrika, SADC imepoteza mawaziri wake kumi ndani ya wiki mbili huku Zimbabwe na Eswatini zikiongoza kwa kila moja kupoteza mawaziri watatu.

SADC inajumisha nchi 16 ikiwemo Tanzania, majirani ugonjwa umetamalaki na ni ugonjwa unaosambaa kwa haraka huku kirusi tofauti kidogo kikiwa kimeanzia Afrika Kusini kinawaumiza kichwa wanasayansi, sisi tuna mpango gani? Watu wenye umri mkubwa ni muhimu sana kwa Taifa ikiwemo uzoefu na baadhi utaalam wao kuwa adimu nchini, tumejipangaje kwani wako kwenye 'risk' kubwa ya ugonjwa huu?

=> Sadc loses ten cabinet ministers to Covid-19 in two weeks
 
Ni mawili either wenzetu wanavyonyolewa zetu tutie maji. Au tusiwe wachoyo tuwape kile ambacho kinatufanya sisi tuwe tofauti na binadamu wengine.
 
Watakapopotea tutachagua wengine. Hao waliopotea wamepotea kama wapoteavyo watu wengine... Kifo ni kifo tu sio mawaziri tu wanaokufa na maisha yanaendelea!
In mzalendo #1 voice
 
Mawaziri pigeni kazi hakuna corona, msilete visingizio, huu mwaka sio wa raha!
 
Virusi vya kwanza walivitengenezea kwao wakaona havitusumbui wa Africa wakaona bora waje watengeneze kirusi huku huku Africa.

Yawezekana kweli kirusi hiki kitasumbua sana Africa maana kimetengenezwa huku huku Africa wazungu watu wabaya sana.
 
Kuna watu hapo wao wanaamini hakuna kabisa corona Tz na wengine wao wanaamini imepungua,ila wote hapo hawana tofauti hakuna ambaye anachukua tahadhari.

lii3.jpg
images%20(3).jpg
 
Virusi vya kwanza walivitengenezea kwao wakaona havitusumbui wa Africa wakaona bora waje watengeneze kirusi huku huku Africa

Yawezekana kweli kirusi hiki kitasumbua sana Africa maana kimetengenezwa huku huku Africa wazungu watu wabaya sana
Hicho tuu ndicho unaweza kuchangia? Pole.
 
Ni namna tu ya biashara mkuu ni ujanja tu namna ya kumfanya mwingine awe mtumwa wako milele. Hapo watauzaje chanjo afu nyie mtanunua wao wanajenga kwao na kuweka hazina kwa wajukuu wao. Sie huku tuko bize kula tunda kimasihara, vumbi LA Kongo na namna ya kumchakata mwanamke mpaka akupe heshima. Yaani unatafuta heshima kula chakula kuwa kikuheshimu haya tukomae kule kwa rikeboy ngoja namie najiandaa kuleta kimasihara moja ivi kwenye tranvai,kvartira na doma
hVirusi vya kwanza walivitengenezea kwao wakaona havitusumbui wa Africa wakaona bora waje watengeneze kirusi huku huku Africa

Yawezekana kweli kirusi hiki kitasumbua sana Africa maana kimetengenezwa huku huku Africa wazungu watu wabaya sana
 
Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo haitoi takwimu za corona.
Huo ndo ujinga ambao unaoogopesha wengi ikiwa ni pamoja na watalii dunia nzimà hawaji Tanzania, wale ambao lazima waje kwa manufaa yao wanaokuja wamejilinda kikamilifu ikiwa pamoja na kuvaa barakoa. Watoe tu takwimu hata sifuri ni namba, milioni ina sifuri 6!
 
Virusi vya kwanza walivitengenezea kwao wakaona havitusumbui wa Africa wakaona bora waje watengeneze kirusi huku huku Africa

Yawezekana kweli kirusi hiki kitasumbua sana Africa maana kimetengenezwa huku huku Africa wazungu watu wabaya sana
Ukiwa na akili kibaba utaongea kama ulivyofabya.

Kirusi hiki kipya ambacho ni mutation of the the first one, kimethibitika kuwepo huko Uingereza, Afrika Kusini na Brazil.
 
Mpaka sasa nchi wanachama wa jumuiya ya kikanda ya kusini mwa Afrika, SADC imepoteza mawaziri wake kumi ndani ya wiki mbili huku Zimbabwe na Eswatini zikiongoza kwa kila moja kupoteza mawaziri watatu.

SADC inajumisha nchi 16 ikiwemo Tanzania, majirani ugonjwa umetamalaki na ni ugonjwa unaosambaa kwa haraka huku kirusi tofauti kidogo kikiwa kimeanzia Afrika Kusini kinawaumiza kichwa wanasayansi, sisi tuna mpango gani? Watu wenye umri mkubwa ni muhimu sana kwa Taifa ikiwemo uzoefu na baadhi utaalam wao kuwa adimu nchini, tumejipangaje kwani wako kwenye 'risk' kubwa ya ugonjwa huu?

=> Sadc loses ten cabinet ministers to Covid-19 in two weeks
Tz tunapuyanga tu nadhani huyu jamaa anaeitwa Covid huku kwetu anakula na kunywa pamoja nasi kiufupi ni rafiki yetu walah
 
Natamani kusema kitu lakini hapana ila kaangalien ubalozi wa uturuki tanzania wametuletea beki mpya simba kaangalie ujionee
 
Back
Top Bottom