Sadio Mane kuwakamua Al Nassr bilioni mbili kwa wiki

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Msenegal SADIO MANE aachana na B.MUNICH waliokuwa wakimlipa zaidi ya milioni mia saba kwa wiki na kutua kwa wazee wa kugawa Minoti Al NASSR ambako ataanza kukunja kitita cha shilingi bilioni mbili kwa wiki ambayo ni sawa na shilingi bilioni nane kwa mwezi na kwa mwaka itakuwa zaidi ya B.90 kwa hakika mpira unalipa sana.

Kiasi hicho ukikigawa kwa siku ni zaidi ya shilingi milioni mia mbili, fedha ambayo inasimamisha Kituo cha Afya kule kijijini kwetu.

Na kiasi hicho hicho cha siku kinaweza kuwalipa kiinua mgongo wazee zaidi ya watano baada ya KIKOKOTOO waliolitumikia Taifa kwa zaidi ya miaka Thelathini na Tano.

Hakika Soka linalipa ndugu zangu msiviue Vipaji vya watoto huko mtaani waambieni soka ni maisha.
 
Msenegal SADIO MANE aachana na B.MUNICH waliokuwa wakimlipa zaidi ya milioni mia saba kwa wiki na kutua kwa wazee wa kugawa Minoti Al NASSR ambako ataanza kukunja kitita cha shilingi bilioni mbili kwa wiki ambayo ni sawa na shilingi
Allah hamtupi mja wake

One of my all time stars

Acha avune akalee taifa lake
 
Hela atapata za kutosha, ila jina lake kwenye soka linapotea
Unataka afanye nini zaidi????

Kashinda Europa cup
Kashinda UEFa champions League
Kashinda mchezaji Bora Africa
Kashinda AFCON
Kashinda EPL
Kawa mfungaji Bora EPL
Kashinda bundasliga
N.k n.k

Huu ni muda wa kuvuta mapene angalia umri wake.. Angalia project zake Kule Senegal, jamaa ambition yake kubwa ni kuisaidia jamii kutoka kwenye umasikini uliokithiri so hakuna anahitaji zaidi ya pesa..
MANE IS NOW MONEY [emoji383]

TRUE LEGEND [emoji106]
 
"Mane is Money"

Nmeielewa sana hii,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…