Saed Kubenea na gazeti la MwanaHalisi

Kuna ambaye ana CV ya huyu mwandishi wa habari? Nataka kujua, licha ya hulka yake, ni wapi ambapo amepata mafunzo ya kumpa ustadi huo.
Dingswayo, nadhani kwa hapa tulipo, huna haja wala sababu ya kiutafuta CV yake, yeye tayari ameishajusfy uwezo wake kwenye hii tasnia ya habari kwa lever ya watu kumpongeza na kulipongeza Mwanahalisi, nadhani kwa hapa panatosha, CV ya nini tena ili hali kazi yake inafahamika?.

Maadam kijana anafanya kazi nzuri, hakuna haja ya kumfuatilia mpaka ndani chumbani, ila kwa uzoefu wangu kwenye tasnia ya habari, haswa uendeshaji wa gazeti kama afanyavyo Kubenea, lazima nikiri, kama hakuna mtu ambaye Kubenea yuko nyuma yake, na hana upande fulani anaoufanyia kazi, then, nami najiunga kumpongeza kwa juhudi zote hizi na kulifikisha Mwanahalisi hapo lilipofika.
 
Wengi tunamkubali saana.

Ni vizuri kama akiangazia taasisi zingine kama vyama vya upinzani na NGO's ili kama kuna madudu yaanikwe na wajifunze
 
Kimsingi nakubaliana na mtoa hoja.Katika nchi kama Tanzania ambayo watu wake ni masikini sana wakati viongozi wakuu wanaogelea katika umasikini mkubwa.Tunahitaji wanaharakati wa kariba ya Said Kubenea na pengine zaidi ya hapo.Elimu tunayopata,hata kama ni ngazi ya cheti inatakiwa kutupa maarifa na ujuzi,lakini zaidi ya hapo inatakiwa kutupa ujasiri wa kukabiliana na changamoto katika maisha.

Changamoto kubwa sana kwa wasomi wetu wa ngazi mbalimbali ni kuona kuwa nchi yetu ni masikini kwa matakwa ya watu wachache ambao bila kupambana nao,umasikini utaendelea.Usomi wa kukaa ofisi na kuvaa tai hata kama ni joto umepitwa na wakati,ufahari wa elimu bila kusaidia harakati za jamii kujikomboa ni ujinga.

Siku ambayo Rostam Aziz anamjibu Reginald Mengi kuhusu issue ya Ufisadi,Said Kubenea alipata nafasi ya kuuliza swali akiwa na ushahidi wa kile alichokuwa anauliza,lakini kilichonisikitisha zaidi,mwandishi wa Habari Corporation,bwana Balile akaanza kumkashifu Said Kubenea,akisema kuwa yeye ni msomi zaidi.Lakini kwa maoni yangu katika ya waandishi ambao wananchi wanaona michango yao,ni Said Kubenea hata kama elimu yeke itakuwa ndogo kuliko akina Salva,Muhingo na wengineo ambao kwa makusudi wameamua kulamba miguu ya watawala.Kwa hiyo tunahitaji watu waliocommitted kwa kazizao na za kujitolea kwa manufaa ya jamii nzima.Natoa wito kwa wasomi na wasio wasomi kupigania ukombozi wa pili katika nchi yetu ambao ni mgumu kuliko ule wa kwanza,tusiwaachie kazi wakina Said Kubenea pekee.Kwa pamoja tunaweza kuikomboa nxhi yetu mikononi mwa makabulu weusi.
 
Ni mahiri pia katika ujengaji wa hoja na hasa maswali "magumu"...
Ningependa "midahalo" ijayo ialike watu wa calibre zake tu wengine tufuatilie kwenye Tv...
 
Nashauri pia aanze kulea vijana ambao kama wataonekana wanaweza mrithi awaachie agombee ubunge kupitia chadema

Jimbo la ILALA linamfaa sana, na akigombea tutahesabu kura kwenye foleni.
 
Stan Katabalo wa karne hii. Kidogo EL ampofue macho.
Hivi wale jamaa waliokamatwa na tindikali hawajataja aliewatuma hadi leo hii??
 
Hivi yule mwenzake Mzee Ndimara Tigambwake hupo wapi... yule mzee nae ni kichwa.. labda Kubenea atuambie kama yumo humu
 
Kubenea, umestahili sifa kwa sasa. Ni zako, ni halali yako na uzichukuwe maana kwa wakati wako umeyafanya yanastahili sifa. Zitunze, ziheshimu, zifanyie kazi ili tunaokusifu leo, tusijekusanyika tena kukulaumu kwa usaliti. KAZA BUTI BABA KAZI BADO MBICHI.
 
tukipata akina kubenea 20 tu nchi itaenda tunavyotaka..........tatizo ni kwamba wengi wa waandishi wa habari wanaganga njaa...wanafuata upepo...........km waandishi wa mtanzania,habari leo,clouds radio, daily news.......ni wapotoshaji wa umma.........
HONGERA KUBENEA...GOMBEA UBUNGE ILALA KM MMOJA ALIVYOSHAURI HAPO NJUU TUTAKUUNGA MKONO
 
said kubenea na gazeti lake wanafanya kazi maalum kwa kikundi kidogo call them watu maalum wenye malengo maalum hasa ya kiuchumi na kisiasa. Siwezi kusoma gazeti ambalo kila siku habari ni za EL wakati nchi imejawa na uovu na waovu karibu kila sekta. Hatuhitaji mwandishi mwenye PERSONAL difference na mtu mmoja au taasisi moja. Niko bored na habari za EL karibu ktk kila toleo la mwanahalisi. Hatumuhitaji mwandishi mwenye kutumia taaluma yake na kalamu kubomoa tuu na si kujenga.Anyway time will tell haya yote kama kweli ni hero au anaganga njaa zake tu. We shall know that when time comes..
 

Jamaaa alinimaliza pamoja na JK kwenda kumwona Hospitali alipomwagiwa tindikali na kumpeleka nje kwa matibabu, ungetegemea angemyenyekea sana kama shukrani, lakini baadala yake jamaa ameendelea kumlipua kama kawa.

Hakika amekuwa mtu muhimu katika mabadiliko ya kimsingi ya nchi.

Nashauri taaasisi na azaki za muhimu za kijamii zimpatie tuzo maalumu.

I personal will try to convince some.

Asante sana mtoa maada.

Said, big up man! If you need anything PM me.
 
Kila siku huwa napenda kujua kama ameamka hai na yu salama.
Manake anaelea kwenye ulimwengu wa vifaru,jaguar,cheetah,sharks na bado anapuyanga

Njowepo maneno yako ni mazito sana! Tunaonaje tuanzishe fund ya ku support Mwanahalisi na Raia Mwema, maana haya magazeti hayapati matangazo ya biashara ya serikali?
 
The Following 14 Users Say Thank You to DENYO For This Useful Post:

Dingswayo (Today), hmethod (Today), Jile79 (Today), King of Kings (Today), lebabu11 (Today), M-mbabe (Today), Makindi N (Today), MFUKUNYUKU (Today), Mfwatiliaji (Today), Misterdennis (Today), Mwita Maranya (Today), N-handsome (Today), Ntemi Kazwile (Today), Superman (Today)

This says a lot about SAED KUBENEA.

Nakutakia maisha marefu, naomba kukumbusha kuwa malipo ya kazi yako hii ya uadilifu na uaminifu kwa taifa lako yapo, yakicheleweshwa yatalipwa na riba inayoongezeka. Hakuna kazi isiyokuwa na malipo, Mandela alinyanyaswa akadhalilishwa lakini leo ni nuru inayoheshimiwa na kuabudiwa. Kuna siku Jina lako na kazi zako zitatambuliwa na kuheshimiwa kama ambavyo leo tunazitambua kazi za wapiganaji kama Mandela.

ALUTA CONTINUA

 
Yaahh he is a hero, na CV kutaka kujua Elimu yake si kigezo kikubwa cha kuwa shujaa, Kubenea kajitoa Muhanga, ndio maana Gazeti la Mwanahalisi
linagombaniwa kama almasi kila mahala, ukichelewa tu hupati, kama ilivyo magazeti ya Raia mwema, Tanzania daima na hata Mwananchi, ni magazeti hayakai sokoni inabidi uweke order most of times, na sbb ni uwazi, ukweli na wanaandika machafu yote ya mafisadi kwa ushahidi, hata
mafisadi wanaogopa kwenda mahakamani, pia wanawachambua wanasiasa wanafiki, wanaochumia tumbo zao, fuata upepo kwa kutoa records zao
mbovu na wanavyo kula hata bila kunawa, keep it up
 

Wewe umetoka dunia ya mazuzu au? Can you thinki objectively? I wonder.
Au wewe ni msomaji wa Habari Leo, Jambo, Uhuru? Waweza kuwa. Duh! You don't fall in the category of great thinkers. Toka JF tafadhali
 
Tuanomba u-substantiate uliyoyaandika. Otherwise we utakuwa CCM uliyeumizwa na moja ya ufisadi unaokuhusu au unaowahusu significant others wako.
 
Huyu ni mpiganaji.Na gazeti lake linapendwa mno.Kwa taarifa yenu tu ni kwamba gazeti hilo huku mikoani linauzwa bei ya juu kuliko ile iliyoonyeshwa juu ya gazeti.Lakini bado watu wanalinunua.siku ya kwanza huuzwa kwa bei halali lakini siku zinazofuata huuzwa kwa bei ya buku(1000).
 
Nawashangaa sana wandishi wa habar wa Tz, hata pale haitakiwi taaluma sana wanapotoka. Tumieni taaluma ipasavyo! Gazeti la mapinduzi ya kwel mi Raia Mwema na Mwanahalisi pekee..

Tumieni taaluma zenu vizur jamani mnaboa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…