Safari hii Jini Kizaizai atakuwa anazunguka tu ndani ya CCM yenyewe

Safari hii Jini Kizaizai atakuwa anazunguka tu ndani ya CCM yenyewe

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Uchaguzi huu ukipitishwa tu na CCM kugombea Udiwani au Ubunge, UMESHINDA. Wala hauna tena mashaka sijui upinzani.

Yaani huku Lumumba ni watu kutafuta tu connection za watu majimboni. Sasa hivi ubaya ubaya unafanyika ndani kwa ndani; yaani usishangae tu ukasikia mtu kapitishwa na Chama kesho kutwa akafanya sherehe ya kuuaga umaskini.

Ukipitishwa na CCM unakuwa umepitishwa kuwa Mbunge wa jimbo husika au Udiwani. Shaka hamna. Hili jambo linawafanya watu wamshukuru sana Mh Rais kawarahisishia sana kwa sasa.

Kinyang'anyiro, patashika na nguo kuchanika vitakuwa tu ndani ya chama mtu akipita huko.akitoka nje anakenua tu meno. UHAKIKA.
 
Uzuri ni kuwa hakuna ajuaye ya kesho wala maisha ya dakika moja ijayo....

Hapo ndipo ulipo "ujinga" wa mwanadamu. Haya ni mawazo ya ujinga wa mwanadamu tu...

Nyakati na majira ya kubadilika kwa "hali" ama "jambo" fulani yakiwadia huwa hakuna kizuizi cha kuzuia na mara zote huwaacha waliokuwa na matumaini makubwa, wakiwa midomo wazi, wamepigwa butwaa hawaamini yanayotokea....!!

Namkumbuka sana Mfalme Farao wa Misri ya kale, ubabe wake wa kupingana na majira na nyakati vs mapigo kumi na nguvu ya Mungu aliye hai....

Naikumbuka vita ya Goliath Mfilisti mbabe wa vita dhidi ya kijana mdogo mdogo kabisa asiye na silaha za kimwili Daudi....

Je, CCM dola vs Upinzani ni Goliath vs Daudi?

Nyakati na majira yaweza kuwa mwamuzi mzuri sana. Na ajidhaniaye AMESIMAMA na aangalie sasa ASIJE AKAANGUKA...!!
 
Uchaguzi huu ukipitishwa tu na CCM kugombea Udiwani au Ubunge, UMESHINDA. Wala hauna tena mashaka sijui upinzani.

Yaani huku Lumumba ni watu kutafuta tu connection za watu majimboni. Sasa hivi ubaya ubaya unafanyika ndani kwa ndani; yaani usishangae tu ukasikia mtu kapitishwa na Chama kesho kutwa akafanya sherehe ya kuuaga umaskini.

Ukipitishwa na CCM unakuwa umepitishwa kuwa Mbunge wa jimbo husika au Udiwani. Shaka hamna. Hili jambo linawafanya watu wamshukuru sana Mh Rais kawarahisishia sana kwa sasa.

Kinyang'anyiro, patashika na nguo kuchanika vitakuwa tu ndani ya chama mtu akipita huko.akitoka nje anakenua tu meno. UHAKIKA.
Udikteta ndivyo ulivyo.
 
Back
Top Bottom