Safari iliyo salama

Safari iliyo salama

partey

Member
Joined
Nov 16, 2020
Posts
50
Reaction score
56
Tusaidizane kutunza Roho zetu, Maisha yetu, tuombeane heri na mema katika Matumizi ya Vyombo vya moto, leo tuzungumzie "Gari".

Pata Elimu ya Mambo 10 ya Kuzingatia
Kabla na Wakati wa
Kuendesha Gari.

Kuendesha gari ni suala linalohitaji umakini na utulivu mkubwa, hasa pale unapoendesha gari umbali mrefu. Mara kwa mara kumeshuhudiwa ajali mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na madereva kutokuzingatia kanuni muhimu katika utumiaji wa vyombo vya usafiri.

Ili kuhakikisha usalama wako pamoja na watumiaji wengine wa barabara, yapo mambo kadhaa unayopaswa kuyazingatia kabla na
wakati wa kuendesha gari umbali mrefu.

1. #Kagua na andaa gari Kabla ya safari yoyote gari linahitaji kukaguliwa na kuandaliwa, hasa kabla ya safari ndefu. Kuna mambo kadhaa unayohitaji kuyakagua kwenye gari lako:
Kagua hali na ubora wa magurudumu.

Hakikisha magurudumu yamejaa vizuri na
hayajazeeka.

Kagua mafuta lainishi (oil).

Hakikisha gari
yako ina mafuta lainishi ya kutosha tena ya ubora unaotakiwa.

Kagua kiasi cha maji.
Maji? Ndiyo maji ni muhimu sana kwenye gari kwa ajili ya kupooza injini ya gari pamoja na kusafishia vioo.

Kagua utendajikazi wa injini. Hakikisha injini yako inafanya kazi vizuri.

Kagua sehemu nyingine za gari kama vile breki, kiongeza mwendo (accelerator),
usukani, taa, honi, viashiria (indicators),
n.k.

Hakikisha unalikagua gari lako vyema na
kuliandaa kwa ajili ya safari.

Unaweza pia
kumtumia mtaalamu wa magari ili akusaidie
kulikagua na kuliandaa kwa safari yako.

2. #Pumzika
Ili uweze kuendesha gari vyema wakati wa safari ndefu ni muhimu kupumzika kwa kiasi cha kutosha kabla na wakati wa safari.

Hakikisha kabla ya safari unapata muda wa kutosha wa kulala ili kuepusha kusinzia barabarani kunakoweza kusababisha ajali.

Unapokuwa barabarani unaweza pia kupumzika baada ya umbali fulani ili usichoke sana.

Kumbuka! Kupumzika uwapo safarini kutakuwezesha kupata nguvu zaidi na kutoa nafasi ya gari lako kupoa ili kuepusha ajali ya gari kuwaka moto.

3. #Fahamu_sheria na kanuni. Kuna kanuni zinazotawala matumizi ya barabara pamoja na vyombo vya usafiri. Ili kuepuka kuingia kwenye matatizo, hakikisha unafahamu vyema sheria za barabarani za eneo unalokwenda

Cont...
 
Madereva wengi wanazingatia hayo yote uliyoorodhesha hapo juu Ila swali ni je wanaendeshaje Magari Yao wakiwa Safarini?
.....Acha na Mimi niongezee kidogo dondoo chache au kanuni Bora za uendeshaji hasa Kwenye Safar ndefu
1)unapoendesha gari ikiwa speed kuanzia 100 hakikisha gari yako ikaa Kati yaani ule Mstari Mkuu unaotenganisha barabara unakuwa chini ya gari yako.
2)usikaze Sana mikono wala kuinuia Shingo juu pindi upo Safar ndefu tafuta namna Bora ya ukaaji Kwenye siti yako ili usichoke mgongo na Shingo

3)Dereva Bora akiwa Kwenye high way anaangalia Mita 100 mbele ili aweze kuona chochote kilichopo mbele yake na kuchukua tahadhari mapema.
4) hakikisha kama upo speed Kali kuanzia 140 k/pH na zaidi hasa Kwa usiku kuangalia Sana mwisho wa Mstari unaomaliza barabara Kwa pande zote mbili yaani kushoto kwako na upande pili wa kulia
5) zingatia alama vizuri alama zote za barabaran
.......asanteni Sana......


 
Back
Top Bottom