Safari kuelekea uhuru wa Tanganyika: Nani anawakumbuka hawa?

Mzee kuna namna ambayo nawewe unaanda vijana kuwajuza mambo haya ukiaachana na kutumia majukwaa haya na magazetini,
Ukizingatia umri wako pia unasogea ,na ya M/Mungu mengi

Kwa usalama wa historia hizi ?
 
Tutawafundisha watoto wetu madrasa na katika shule zetu za Kiislam historia hii isomwe na waijue wallah historia itaandikwa upya na haqq itatendeka kwa idhini ya Allaah tabaraka.
 
Karimjee Hall Dar es Salaam , Tanganyika 1960

Julius Nyerere sworn in as Chief Minister of Tanganyika as 36th session of Legislative Council. Various shots in the Karimjee Hall at Dar Es Salaam. CU Mr Julius Nyerere being sworn in as Chief Minister. MS as he walks towards camera and signs a book. CU Mr A S Bajaj of the Iringa constituency shaking hands with one of the Justices. MS the Minister for Health and Labour Mr D N M Bryceson signing the book. MS Mrs E Markwalder of the Tanga Urban constituency shaking hands with one of the Justices. CU the Governor of Tanganyika Sir Richard Turnbull rising to make his speech. Elevated shot of the Governor speaking to the house. Exterior LS Mr Nyerere being cheered by fellow Africans. MS two men wearing banners saying "long Live Nyerere". Various shots as Nyerere walks along waving to the crowds. LS crowds of Africans waving branches rushing towards camera. LS Mr Nyerere getting into a Land Rover and waving to crowds. LS as it moves off. CU Nyerere in it. High angle LS Land Rover travelling through crowds of people cheering and waving. Various shots masses of people waving branches, dancing and running behind the Land Rover. LS one man waving a branch and dancing on his own.


Surce: British Pathe
 
CHOZI LA MZEE KIMITI JINSI TANGANYIKA ILIVYOPATA UHURU



“Wakati bendera ya Tanganyika inapandishwa, baba alitoa machozi. Hakuwa na uhakika kama wazungu wakiondoka sisi tungeweza kuendesha nchi.
Baada ya kuona wote waliokuwapo walikuwa wazungu, akasema hawa wanaondoka sisi tutaweza kuendesha nchi?” Hii ni sehemu ya simulizi ya Paul Kimiti; mwanasiasa mkongwe aliyeaminiwa na marais wa awamu zote kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini.
Kimiti ambaye alizaliwa Januari 15, 1940 mkoani Rukwa, ametumika katika uongozi wakati wa serikali ya awamu ya kwanza baada ya mwaka 1982 Mwalimu Julius Nyerere kumteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu. Alianza kufanya kazi chini ya Waziri Mkuu Cleopa Msuya na kisha Edward Sokoine (marehemu). Mwaka 1984 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mwaka 1989, Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi alimteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera hadi mwaka 1991 alipoteuliwa tena kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya. Macho ya viongozi wakuu wa nchi yaliendelea kumwona Kimiti kwani mwaka 1995, Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alimteua kuwa Waziri wa Kilimo na mwaka 1998 akamteua kuwa Waziri wa Kazi na Vijana.
Kwa upande wa uwakilishi, mwaka 1980 alikuwa mbunge wa kuteuliwa na mwaka 1995 aliamua kwenda kugombea jimboni alikohudumu vipindi vitatu hadi mwaka 2010 alipotangaza kutogombea tena ubunge wa Sumbawanga Mjini. Serikali ya awamu ya tano pia imeendelea kumtumia mwanasiasa huyu mkongwe.
Oktoba 16 mwaka jana, Rais wa awamu ya tano, John Magufuli alimteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi ya Taifa (NARCO). Kutokana na nyadhifa hizo mbalimbali alizoshika, Kimiti anayo mengi ya kulinganisha na hatimaye kuja na suluhisho kuhusu hatua ambayo nchi imepiga katika hii miaka 58 tangu uhuru. Lakini pia, licha ya kumulika kipindi baada ya uhuru, Kimiti ambaye alipata elimu ya msingi mkoani Rukwa na hatimaye mwaka 1954 kujiunga na shule ya sekondari ya Mzumbe, anazo kumbukumbu juu ya namna Tanganyika ilivyopata uhuru.
Baada ya kuhitimu sekondari, mwaka 1959 akiwa na umri wa miaka 19 aliajiriwa Wizara ya Kilimo kama ofisa kilimo (Extension Officer). Wakati nchi inapata uhuru, alijiunga na chuo cha kilimo Tengeru. Ndiyo maana anakumbuka namna ambavyo kipindi cha Watanganyika kuchukua madaraka kilivyokuwa kigumu kutokana na kutokuwapo watu wengi waliokuwa na ujuzi wa kushika madaraka.
Anakumbuka Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyopambana kuandaa watu wa kushika madaraka na wakati huo huo kuwaondolea Watanganyika mawazo ya kudhani kwamba bila wakoloni, nchi isingekwenda. Chozi la babake Kimiti anazungumzia hofu aliyokuwa nayo baba yake, Mzee Petro Kimiti mpaka akajikuta akitoa machozi baada ya bendera ya Waingereza kushushwa na kisha kupandishwa ya Tanganyika. Baba yake alikuwa dereva wa Mkuu wa Wilaya (DC) wa Sumbawanga wakati wa serikali ya kikoloni. Kimiti anasema mzazi wake huyo hakuwa na uhakika kabisa kama Watanganyika wangemudu kuendesha nchi baada ya Waingereza kuondoka.
“Wakati bendera ya Tanganyika inapandishwa, baba alitoa machozi. Hakuwa na uhakika kama wazungu wakiondoka sisi tutaendesha nchi. Baada ya kuona wote waliokuwapo walikuwa wazungu, akasema hawa wanaondoka sisi tutaweza kuendesha nchi,” anasema Kimiti.
Anaendelea kusema, “Baba hakuwa na imani… Wakati walipoanza kuteuliwa wengine, aliona hawafanani na hadhi ya viongozi wa kikoloni. Aliwaona ni waswahili anaowafahamu. Lakini baadaye alizoea akaendelea kuwatumikia hao hao.”
Kwa mujibu wa Kimiti, baba yake alikuwa askari polisi na baadaye ilipendekezwa ajifunze udereva ndipo akawa dereva wa Mkuu wa Wilaya tangu mwaka 1938 hadi 1972 alipostaafu wakati nchi ikiwa huru. Anasema mzazi wake huyo alikuwa dereva wa kwanza katika Sumbawanga nzima na hapakuwa na gari lolote katika eneo hilo zaidi ya alilokuwa akiendesha.
“Hapakuwa na gari lolote Ufipa (Sumbawanga) nzima. Gari la kwanza lililoonekana pale ni la mzee Petro.”
Kutokana na utumishi uliotukuka, mzee huyo aliongezewa muda wa kufanya kazi licha ya umri wa kustaafu kupita. Alikuwa akiendesha gari la wagonjwa la serikali. Mwaka 1954 baba yake alitunukiwa cheti cha utumishi bora uliotukuka kutoka kwa Malkia Elizabeth wa Pili. Alikabidhiwa cheti hicho na Gavana wa Kiingereza nchini Tanganyika, Edward Twining.
Uhuru bila wasomi Akizungumzia ugumu wa kipindi baada ya uhuru ambacho Watanganyika walichukua madaraka, Kimiti anasema ulitokana na kutokuwapo watu wengi waliofunzwa kushika madaraka. Hata hivyo, anasema Mwalimu Nyerere aliteua Watanganyika katika nafasi mbalimbali zilizokuwapo wakati wa ukoloni. Baadhi ya nyadhifa alizibadili majina kuondoa mawazo ya kuhusisha uongozi wa Watanganyika na utawala wa kikoloni.
Anatoa mfano wa nafasi ya Mkuu wa Wilaya (DC) kwamba aliibadili jina ikajulikana kama Area Commissioner. Vile vile wakati wa Tanganyika huru ndipo baadhi ya sare za mavazi ziliondolewa. Mathalani, Mkuu wa Mkoa (Province Commissioner) alivaa kaptula lakini baba wa taifa katika kufuta ukoloni vichwani mwa wananchi, aliwataka wavae kawaida. Vivyo hivyo kwa maofisa kilimo, Kimiti anasema, “tulivaa kaptula lakini baadaye ikabadilishwa.”
Mwanasiasa huyu mkongwe akiwa na umri wa miaka 19, Aprili Mosi, 1959 aliajiriwa kama Bwana Shamba bila kwenda kozi.
“Kipindi hicho tulivaa kaptula, bonge la koti limeandikwa agriculture na kofia. Tulitembea na note book kwa sababu lengo mojawapo ni kuangalia kama wakulima wanafuata masharti waliyopewa katika kilimo.” Baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili, mwaka 1961 aliambiwa aende kwenye kozi Chuo cha Tengeru mkoani Arusha.
Anasema wakati wa Tanganyika kujitawala, watu wengi waliendelea kupata mafunzo na chuo walichokuwa wakitumia kilikuwa cha Mzumbe ambako walifundishwa masuala mbalimbali. Akielezea uongozi katika miaka ya awali ya uhuru, Kimiti anasema baadhi ya viongozi waliendesha nchi mithili ya wakoloni (kwa maana ya tabia) wakitaka kuendesha kwa mikiki kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
Anasema wengi walitumia madaraka vibaya, wakiwaweka watu ndani kwa misingi ya kutaka kuendesha nchi inyooke.
“Mwingine unakutana naye klabu anaagiza mtieni huyu ndani. Kutia watu ndani ilikuwa ni kujenga nidhamu lakini wakatumia madaraka vibaya.”
Endelea kufuatilia mfululizo wa makala za mahojiano na mwanasiasa huyu mkongwe, Paul Kimiti akieleza serikali ilivyompeleka nje ya nchi kusoma; alivyokutana kwa mara ya kwanza na Mwalimu Nyerere na kumkabidhi kitita cha fedha zilizotokana na bendi ya muziki aliyoianzisha ughaibuni.
 
Askari wa 'Keya' King's AFrican Rifle KAR ambapo wengi akiwemo Mzee Sykes walipitia mafunzo na kumtumikia Mfalme wa Uingereza ktk jeshi la KAR na ambao baadaye walikuja kuwa kichocheo cha kudai uhuru wa Tanganyika kutokanana kujifunza kuwa 'mzungu' ni mtu wa kawaida kama wao.

Hivyo funzo hilo kupitia vita, mafunzo jeshini na utumishi katika serikali ya mkoloni kama watoza ushuru masokoni, mabwana-soko, watozwa ushuru, makarani, waalimu, waganga n.k vijana hao 'wamatumbi' wa miaka hiyo waliona hakuna cha ajabu hivyo wakaanza harakati za kudai uhuru toka kwa mkoloni

Mwaka 1942 Askari wakipitia mafunzo mbalimbali ktk jeshi la mkoloni


Source ; British Pathe
 
Mzee kuna namna ambayo nawewe unaanda vijana kuwajuza mambo haya ukiaachana na kutumia majukwaa haya na magazetini,
Ukizingatia umri wako pia unasogea ,na ya M/Mungu mengi

Kwa usalama wa historia hizi ?
Chizzo...
Historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimeiandika na ipo katika Kiswahili na Kiingereza.
Hii ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kuwa historia hii haipotei.

Kuandaa wasomi watakaokuja kusomesha hii historia hiyo ni kazi ya shule na vyuo vikuu vyetu.



 
Na Nyerere ni BABA LAO.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mng'ato,
Mwalimu Nyerere historia yake inavutia sana katika kitabu cha Abdul Sykes mwanzo hadi mwisho kila nilipoweka kalamu juu ya karatasi msomaji anamsoma Julius Nyerere.

Tofauti na historia nyingine zilizopata kuandikwa ni kuwa kuwa katika kitabu cha Abdul Sykes hutamsoma Nyerere peke yake utamsoma Mwalimu na wazalendo wengine ambao hawakupata kuelezwa mahali popote.

Mathalan nani aliyekuwa anajua kuwa Nyerere alijadiliwa mwaka wa 1953 nyumbani kwa Hamza Mwapachu na watu waliomjadili ni Abdul Sykes, Ali Mwinyi Tambwe na Hamza mwenyewe.

Katika historia hii utajua kuwa Hamza Mwapachu kwa Abdul na Nyerere yeye alikuwa ni kaka mkubwa kwao kwani kazaliwa mwaka wa 1913 na ndiye aliyekuwa akiwashawishi vijana kujipanga kudai uhuru wa Tanganyika.

Historia ya akina Sykes katika maendeleo ya Waafrika wa Tanganyika inatoka kuanzia miaka ya 1920 wakiwa ndani ya African Association.

Vigumu kupuuza historia hii.

Si kama mimi nimeandika historia hii kwa nia ya kumdogosha Nyerere la hasha nia yangu ni kutaka michango ya wazalendo wengine nayo ifahamike na kuwa na historia kamili.

Inanishangaza sana nimapoona mnaposomeshwa historia ya wazalendo wengine waliopigania uhuru hamaki zinapanda na mnakuja na maneno ya kejeli.

Inakuwa kama vile hamko tayari kusoma historia ya kweli ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Labda unifahamishe kipi ambacho wewe unaona si kizuri kwako.
 
Huyu angeifanya nchi iwe Kama Botswana yaani mtu kujifanya mwenyeji wakati Ni muhamiaji aliletwa na wakoloni wa kijerumani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu angeifanya nchi iwe Kama Botswana yaani mtu kujifanya mwenyeji wakati Ni muhamiaji aliletwa na wakoloni wa kijerumani

Sent using Jamii Forums mobile app
Nditolo,
Aliyeingia Tanganyika na Herman Von Wissman kutoka Mozambique ni Sykes Mbuwane.

Sykes Mbuwane akamzaa Kleist Sykes Pangani 1894.

Sykes Mbuwane akamzaa Abdul Sykes Dar es Salaam 1924.

Sykes Mbuwane kwa mchango wake katika maendeleo ya Waafrika wa Tanganyika ametiwa katika Dictionary of African Biography (2011).

Abdul Sykes nimeandika maisha yake (1998).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sheikh kuna babu yangu Alikua mombo tanga anaitwa mzee Ally abdalah@ mkianyani nae alikua mstari wa mbele katika uhuru wa tanganyika .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila hatajwi alikua akiishi mtaa wa marembwe mombo mm ni mjukuu wake nyumba yake watoto wameiuza walah nimeumia sana nilikua naenda kulala pale kupata baraka zake, kunakipindi nilisimuliwa aligombea udiwani akapigwa fitna na wanafki babu akamwandikia nyerere barua kwa vile mwalimu alijua umuhimu wake katika mapambano akampa udiwani wa kuteuliwa, na kuna kipindi aliitwa ikulu apewe kazi babu akakataa kwa vile wanae walikua wadogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani anawadharau?Mlitaka wawatendeje?Naamini ulikuwa wajibu wenu kudai uhuru na mkatenda lile lililowapasa.Hayo ya kudaraulika ni inferiority complex tu.Namheshimu mzee muhamed kwa sababu anaweka historia sawa kwa kadiri ya uwezo wake ila habari ya kudharaulika abadan usituletee.Kama fikra ziko hivi basi yumkini ni mtazamo huu ulipelekea hata historia ikapindishwa
 
Kama kuna ukweli katika hilo basi timiza wajibu wako kama mjukuu kuweka rekodi sawa.Tafiti kisha andika watu watambue.Pembeni ya hapo hizo zitakuwa heka ya za kusimuliwa tu ambazo zitabaki kuwa hekaya.
 
Mzee Moh'd Hofu ya kutaja uislamu?Kwambu historia imejaa dini nyingine?Hapo unaghafirka mzee.Nakukubali sana na madini unayotoa ila sikubaliani na wewe kusema kwamba historia imepindishwa kwa sababu ya kutaka kuwaondoa Waislam katika historia.Nafikiria labda kulikuwa na chokochoko kama hizi za kuleta hoja za udini na zikapelekea kutofautiana jambo lililopelekea historia kuwa na mapengo.Wewe timiza wajibu wako kama Mtanzania mzalendo na uwekei historia sawa ili usitake kuleta habari za udini kwani utafanya kwa hakika upuuzwe hata kama historia yko ina msingi.

Katika mapambano ya uhuru ambayo kiini/kitovu hake kilikuwa Dar /Mzizima ambako wenyeji wengi walikuwa ni waislamu lazima wangeoneka mstari wa mbele katika mapambano hata kama mchango wao ulikuwa wa kawaida tu na usio na impact.Hivyo basi tukubali kwamba Historia ya nchi yetu tangu uhuru na mpaka wakati huu inahitaji kufanyiwa utafita wa kina(unbiased) kwa faida za watoto wetu ila kama mnataka kuandika historia ya nafasi ya waislamu katika history ya Tanganyika nafikir itakuwa ni somo tofauti la kufundishana wanadini wenyewe na sio historia ya uhuru wa Tanganyika.
 
Ninachojifunza hapo ni ukarimu wa watu wa pwani na wepesi wao wa kuamini wengine. Tukumbuke wageni wote walioingia Tanganyika kabla ya ukoloni na hata wakati wa ukoloni walipita pwani, wakakaribishwa na watu wa pwani na wakasaidiwa na watu wa pwani katika yale yaliyowaleta wageni hao:
  1. Waarabu walipokelewa na watu wa pwani tangu karne ya kumi, wakapewa fursa za kufanya biashara na kueneza utamaduni wao na dini yao
  2. Wajerumani wale wapelelezi wa mwanzo akina Henry Stanley na David Livingstone, na wamishionari akina Johann Ludwig Krapf, Johann Rebmann, walowezi akina Karl Peters waliokuja kutapeli ardhi na wavamizi wa kijeshi kama Emil von Zelewsky yule aliyeteketezwa na Mkwawa pale Kalenga, wote waliingia kupitia pwani, wakapokelewa na watu wa pwani na wakasaidiwa na watu wa pwani. Miongoni mwa misaada hiyo ni pamoja na kupatiwa pa kulala, vyakula, kuonyeshwa njia, kusaidiwa kubebewa mizigo (upagazi), na mjue mambo ya misheni town yalianza pwani tangu siku nyingi, walikuwepo pia wakalimani wa lugha ya kijerumani kwenda kiswahili na lugha za makabila mbalimbali, yote yalipatikana pwani! Hivi hamshangai Karl Peters aliwezaje kuongea na chief Mangungo wa Msovero? Kulikuwa na wakalimani wa lugha zote hapo Bagamoyo walikuwa wanasubiria wageni na kupiga dili kama wale 'fly catchers' wa Arusha wanavyovizia watalii. Ujanja ulianza zamani Pwani!
  3. Kama uislamu ulivyopokelewa na watu wa pwani, hali kadhalika watu haohao wa pwani, tena wakiwa waislamu, waliupokea ukristo na wakawalea wamishonari na kuwatunzia mali zao, mashamba yao bila ugomvi wa mipaka, na wakawafundisha kiswahili cha kutafsiria biblia, misale, katekisimu, nyimbo za dini nk
  4. Watu wa Pwani waliwapokea waingereza baada ya kuisha vita kuu ya kwanza ya dunia na kuwafanyia ukarimu uleule wa desturi yao.
  5. Na watu wa pwani wamepokea makabila mengine yote ya Tanzania na kuwapa mashamba na maeneo ya makazi kuanzia Ubungo mpaka Mbagala, Kinyerezi mpaka Kigamboni, Bunju mpaka Kisarawe, kote kumejaa watu wa makabila yote wakiishi kwa amani na watu wa pwani.
  6. Na wakoloni kuondolewa kwa jitihada ya watu wa pwani ni sawa kwani sasa watu wa pwani hawakuwa tena peke yao, na pia tukumbuke jamani; mwiba hutokea palepale ulipoingilia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…