huyu marandu sasa ndio anaimaliza chadema kwa kutengeneza ushahidi bandia ili MASHABIKI wao wakasirike na kuleta fujo, na hapo ndio mwisho wa chadema maana mashabiki wao masikini watapata mkongoto na huenda chadema kufutwa kabisa kwa kuchochea machafuko na kumwaga damu!!!!
mimi nawashauri viongozi wa chadema wakubali matokeo na wamepata wabunge wengi wakafanye kazi bungeni waache kukimbilia ikulu waache kumsikiza huyu marandu anataka kuua chama chenu kwani ameingia chadema kwa kazi maalumu ambayo aliisha ifanya kazi kama hiyo pale alipoua nccr-mageuzi miaka ya 90!!!
mbona cuf wamekubali matokeo ya zanzibar na kama ushindi hupatikana kwa wingi wa mahudhurio ya watu ktk mikutano ya kampeni, basi maalim sefu alikuwa anapata umati wa watu, lakini wananchi wameamua hivyo slaa huna budi kukubali maamuzi ya wananchi na hapo utaonesha uzalendo na ukomavu wa kisiasa!!! Vinginevyo utajiabisha kwa kuchochea machafuko na kumwaga na damu za mashabiki wako!!!!
slaa wewe ni padri na unatakiwa kuonyesha upendo na huruma uliyofundishwa rome ili mashabiki wako wasipate misukosuko!!!