SoC02 Safari ya kijani kibichi

SoC02 Safari ya kijani kibichi

Stories of Change - 2022 Competition

Unicentaur

New Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Hakika lilikuwa taifa la kushangaza, ilikuwa ni nchi ya kuvutia macho na kupendea kwa kutazamwa kwa macho. Ilikuwa ni sehemu ambayo yeyote angependa kuitembelea, eneo lenye mapori ya kipekee, misitu minene, na savana yenye wanyama wengi mno. Mwenyezi Mungu ali iipendelea kwa kuimwagilia kwa mvua zisizo na kipimo na jua angavu.

Kwa hakika kila kitu kilistawi katika nnchi hiyo ambayo kwa sasa inasikika kama sehemu ya kufikirika. Misimu na majira ya mwaka yalikuja kwa wakati wake. Mvua zilinyesha na kipupwe mwanana kilipuliza katika misimu yake kama ilivyoratibiwa na alieviumba. Matunda, mboga na mazao yalistawi ajabu.

Kila mtu aliepata nafasi ya kutembelea nchi hiyo ambayo hufahamika kuwa kisiwa cha Amani hakukosa cha kusimulia kulihusu. Wengi wao walisifia mito na vijito vilivyotiririka bila kigugumizi, huku wengine wajipendezwa zaidi na vilima na milima iliokuwa ya kuvutia sana na ilijengeka kwa ustadi wa hali ya juu, katika hao wengi walivutiwa zaidi na mlima Kilimanjaro ambao ulivutia sana kwa kutazama na hata wakathubutu kuukwea kukifikia kile kilichoonekana kama kofia nyeupe ya bara la Afrika. Wengi walinena maneno mengi mazuri juu ya taifa hilo lenye fukwe angavu na visiwa vyenye kuvutia, lenye watu wenye tamaduni za kipekee Zaidi ulimwenguni.

Siku na miaka vikasonga, sayansi na tekinolojia navyo vikakua, nalo taifa likachangamka. Viwanda vikajengwa na biashara zikatanuka. Kila mtu akavutiwa Zaidi na kuingiza fedha kwa kutumia maliasili bila ya kujali endapo zinatumika kwa akili ya kujali mazingira au la. Miti ililia kwa kuwa hakuna aliejali endapo inapotea au la kwa kuwa ilikatwa bila hofu. Moshi wa viwanda ulichafua hali ya hewa, kelele za viwanda na mashine zilienea kila mahali. Ongezeko la magari nalo lilizidisha hatari kwa kila mtu.

Kwa hakika mambo yalibadilika, kama mzaha vile ardhi iliyomea kila kitu ikathubutu kuwaacha wananchi wake katika janga la njaa katika miaka ya tisini. Nayo mito ikaanza kukauka na hata sayansi na teknolojia ya umeme wa maji ikawa siyo uti wa mgongo wa uzalishaji wa umeme tena. Ile theluji nzuri iliyo funika mlima mtukufu wa Kilimnjaro ikapoteza uzuri wake na kuyeyuka. Visiwa vikatishiwa na ongezeko la kimo cha maji ya bahari na baadhi ya fukwe nzuri zikaanza kudidimia katika tope.

Tishio halikuishia kwa mimea pekee, bali hata wanyama waliotegemea mimea hiyo, baadhi ya mapori mazuri yakabaki kuwa kivutio wakati wa mvua tu na huku barabara zikitishia uwezekano wa kuyafikia. Wanyama hatari walianza kupotelea katika mazingira ya binadamu kutafuta hifadhi na maji. Lakini hakuna alieonesha kujali kasoro watu wachache ambao pengine jamii haikuweza kusikia sauti yao kutokana na kuwa haikuwa kubwa wala haikuwa na ushawishi.

Pengine wengi hawakuona lakini hatari ilikuwa kubwa Zaidi kwa binadamu. Mlipuko wa magonjwa hatari na ya ajabu uliongezeka hasa kutokana na uharibifu wa mazingira na muingiliano kati ya wanyama pori na wanadamu kuwa mkubwa. Utapia mlo nao ulionekana kutishia baadhi ya maeneo kutokana na kwamba sasa ardhi haikutii kwa kuzalisha mazao kama ilivokuwa mwanzo na wala mbingu hazikuimwagilia tena ardhi hiyo iliyowahi kuwa bustani Ya kuvutia.

Saratani ni kati ya magonjwa yaliyokuja na haribiko hilo la mazingira, pumu na magonjwa ya kifua hayakukaa mbali. Huko kusini nao walilia na gonjwa la ghafla la Mgunda. Hadithi juu ya homa za misimu nazo zilienea kila mahali. Kutokana na hali halisi ya uchumi wa taifa hilo basi nguvu nyingi iliwekezwa katika kutibu wananchi wake kwa kutumia rasilimali nyingi, pesa na hata mikopo kutoka katika mataifa makubwa.

Matatizo hayakuishia katika afya pekee, uchumi nao ukawa ni wa kutegemea vyanzo vichache kwani kilimo na utalii vilikumbwa na kilio kisichoelezeka. Katika mazingira nako kulikuwa na shida kuu, mvua za misimu zikawa na uzito wa kutisha huku zikiacha misiba na watu wasiokuwa na makazi. Misimu ya joto nayo ikawa ni ya kuogofya na tishio kwa wananchi wote.

Mama wa taifa hilo aliinuka akijaribu kuokoa japo sekta ya utalii katika taifa hilo; alitangaza vivutio mbali ambavyo taifa hilo lilijaaliwa, si kwamba watu walikuwa hawavifahamu lakini lengo kuu lilikuwa kuwakumbusha watu ya kuwa taifa bado li hai. Lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu aliyesahau uzuri wa vivutio hivyo, hakuna aliyesahau ya kwamba mlima mrefu sana barani ulikuwa hapo, ama kuwa urithi wa dunia ulipendeza hapo, la hasha kilicho wazuia watio ni kuwa uzuri huo kwa sasa haukuwa kama walivyo utambua kale. Joto liliyeyusha kofia za mlima huo, ukame uliharibu mapori na misitu, sasa haikuwa sehemu ya kuvutia tena bali sehemu ya kutia huruma.

Kizungumkuti na fumbo kubwa lilikuwa katika kuhakikisha kuwa matatizo hayo yanafika kikomo, na ukweli ulikuwa kuwa njia pekee ilikuwa ni kuokoa mazingira na kurejesha asilia ya mwanzo. Wananchi na viongozi wote walichanga akili na mawazo ili kuokoa hatma ya taifa lao. Kila mmoja alipaswa kushiriki kwa uwezo wake wote.

Safari ya kubadilika si fupi wala si rahisi, inahitaji bidi na nguvu pamoja na mshikamano. Inahitaji viongozi wenye tija na wananchi waliojizatiti haswa ili kuleta matarajio yao katika maisha. Inahitaji watu walio tayari kuachana na ulimbukeni wa teknolojia zisizo na tija na kugeukia matumizi ya teknolojia mbadala. Pengine jambo hili litafikia utatuzi ama pengine litabaki kuwa kitendawili kisichotegulika ama donda lisilotibika, yaani donda ndugu.

Imeandikwa na
Renata Nicas
 
Upvote 1
Back
Top Bottom