Safari ya kuanzisha biashara ya nafaka kwa mtaji wa Tsh. milioni 50

Safari ya kuanzisha biashara ya nafaka kwa mtaji wa Tsh. milioni 50

Bullshit

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,357
Reaction score
1,596
Habari wana JF na poleni kwa kipindi hichi cha corona.

Mimi ni mjasiriamali ninajishughulisha na biashara mbali mbali.ila katika harakati za kibiashara huwa napenda sana kufanya biashara ya kuuza nafaka ambayo imepakiwa kwa jina langu,mfano kama Azam.

Nilitaka nipite hapa ili niwaeleze jinsi ngani nimejipanga kuanza biashara nikiwa na ndoto ya kushindanishwa na bidhaa za Azam.

MALENGO
malengo yangu ni kuanzisha campuni inayojishughulisha na maswala ya chakula ambacho kimeppakiwa kwenye mifuko na kisambazwe kwa jina langu Tanzania na africa kwa ujumla.

Nitakuwa napakia vyakula kwenye mifuko.mfano:maindi unga,mchele,maharage nk ili niwe nasambanzia watu sehemu mbali mbali
IMG_3700.JPG

Mfano wa picha hapo juu..

MIPANGO:
Ili kutimiza lengo la biashara hii nataka kwanza nianze tutafuta masoko nchi za tanzania,congo na burundi,hapo kila sehemu nitaweka store mbili mbili ili bidhaa inapofika vinauzwa hapo.

Lakini kabla ya kuanza kupakia products zangu,nitaanza kuuza nafaka kutoka kwenye kampuni zingine ili kupima upepo kwenye store hizo nitakazo kuwa nimefungua.

Ila lengo langu la baadae ni kufungua matawi mengi na kiwanda kikubwa chenye wafanyakazi wengi

MTAJI.
Nina mtaji wa M50 ndo bajet nimepanga katika harakati za kumfikia bakrhesa.
Nina kundi la watu watatu wachapa kazi kweli kweli wanaelewa nini wanafanya wanapokuwa kazini

Katika Team yangu kuna Msimamizi wa shughuli za uzalishaji vyakula,mtafuta masoko mtandaoni na mtaani na mtu wa mipango.wako vizuri maana nimeshashirikiana nao naona wako vizuri kabisa licha hawana elimu ya darasani lakin ni jeshi lenye kuwa na lengo la ushindi.

Nataka ninunue machine 3.
Machine ya kusaga maindi,mashini ya kukoboa maindi,na mshini ya mchele,
NB:najua zipo nyingi za kufanya kazi hii ila nataka nianzie kwanza na hizo tatu.
Kazi zingine zitafanywa na watu.

Baada ya kuanza kutengeneza bidhaa zangu nataka ninunue fuso la kusambaza bidhaa,dar,congo na burundi.

USHAURI.
Biashara hii sina uzoefu nayo na sijawahi kuifanya ila tu ninashauku ya kuifanya na nina imani itanipa pesa.

Sasa ndugu wewe mwana JF ambae una idea na wazo langu au una uzoefu na aina ya biashara ninayoenda kuifanya unaweza kunishauri nini ili nifanyikiwe katika biashara yangu ya kushindanishwa na Azam.

Mfano wa ushauri.
Kias gani kinafaa kuanza nacho.
Nizingatie vitu gani kabla ya kuanza.
Ni wapi nchini Tanzania panafaa kutafuta nafaka na kuweka kakiwanda kangu nk...

NAKUMBUSHA.
Nataka niwe napakiwa maindi,unga ambao nimetengeneza mimi,mchele nilikoboa mimi,maharage niachambue mimi na mazaoengini kwenye mifuko ya uzito tafauti na niwe sambaza nchi tatu tofauti.
Lakini baada ya hatua hii nataka niamie kabisa niwe nauza mpaka samaki wa kopo,yaani chakula kilichopagiwa kwenye makopo au mifuko
Mafano hapo chini
IMG_3700.JPG

Ushauri wako waweza kunipa hatua ya mafanikio yangu.kwaiyo husisite kunielemisha chochote kuhusu mambo haya ya chakula.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Attachments

  • IMG_3700.JPG
    IMG_3700.JPG
    586.7 KB · Views: 53
Good idea ila ushauri wangu anza na product moja kwanza hakikisha unaiweka vizuri yaan parked yake tu ijiuze yenye unaipromote to the maximum then ikiwa inaelekea vizuri unaingiza nyingine baada ya 1 year hii itakufanya uwe vizuri sokoni utajua nafaka gani inafaida nzuri zaidi.

ukitaka ushauri zaidi naweza kukupatia.
 
Mkuu wazo lako zuri...lakini kwa 50m ni ndogo sana hutaweza....tukianza na hiyo gari la fuso used 15m....machine ya kisasa ya kusagia 20m....imebaki 15m.....bado hujafunga machine...kodi ya jengo....kodi ya store....TRA....leseni....TFDA....hujanunua material kama mahindi....hujalipa mishahara ya wafanyakazi wako...kumbuka sio kila bidhaa utakayo tengeneneza utauza....uzoefu huna na wateja wa kutosha huna....

Hivyo hasara zakufikia tu..Mkuu kuna ushindani pia...unaweza ukafanya biashara mwaka mzima hujaona faida ya moja kwa moja...lakini matumizi yako pale pale..hivyo ukiwa na mtaji mkubwa unakubeba...hiyo idea angalau ungekuwa na 200m...Nakushauri fanya biashara ya kununua na kuuza nafaka Jumla jumla...au saga sembe na dona uuze hapa hapa ....

Achana na issue za kupeleka nje ya nchi...wala kuajiri watumishi wengi mapema kiasi hivyo,,,mbinu nzuri ni kuanza na biashara ndogo...ili upate uzoefu na kusoma mazingira...pia itakusadia usipoteze mtaji....kupata mtaji ni rahisi kidogo...issue ni kuukuza huo mtaji...ukicheza kidogo to unarudi kule kule.
 
Mkuu wazo lako zuri...lakini kwa 50m ni ndogo sana hutaweza....tukianza na hiyo gari la fuso used 15m....machine ya kisasa ya kusagia 20m....imebaki 15m.....bado hujafunga machine...kodi ya jengo....kodi ya store....TRA....leseni....TFDA....hujanunua material kama mahindi....hujalipa mishahara ya wafanyakazi wako...kumbuka sio kila bidhaa utakayo tengeneneza utauza....uzoefu huna na wateja wa kutosha huna.... hivyo hasara zakufikia tu..Mkuu kuna ushindani pia...unaweza ukafanya biashara mwaka mzima hujaona faida ya moja kwa moja...lakini matumizi yako pale pale..hivyo ukiwa na mtaji mkubwa unakubeba...hiyo idea angalau ungekuwa na 200m...Nakushauri fanya biashara ya kununua na kuuza nafaka Jumla jumla...au saga sembe na dona uuze hapa hapa ....achana na issue za kupeleka nje ya nchi...wala kuajiri watumishi wengi mapema kiasi hivyo,,,mbinu nzuri ni kuanza na biashara ndogo...ili upate uzoefu na kusoma mazingira...pia itakusadia usipoteze mtaji....kupata mtaji ni rahisi kidogo...issue ni kuukuza huo mtaji...ukicheza kidogo to unarudi kule kule.

Mkuu nitaanza na maduka ya nafaka kwa hiyo pesa,mafuso na mambo mengn ni kwa baadae baada ya kuona mambo yanaenda sawa

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Good idea ila ushauri wangu anza na product moja kwanza hakikisha unaiweka vizuri yaan parked yake tu ijiuze yenye unaipromote to the maximum then ikiwa inaelekea vizuri unaingiza nyingine baada ya 1 year hii itakufanya uwe vizuri sokoni utajua nafaka gani inafaida nzuri zaidi.

ukitaka ushauri zaidi naweza kukupatia.

Nimependa ushauri wako mkuu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ungemchek Mama alaska anaweza kukushauri...ila kwa 50 naona km una mambo mob hela ndogo!
Nikupe tu kongole na usikate tamaa esp serikalini kupata vibali..maana kuna kaukiritimba!...kabiliana na changamoto kibabe na kibishi

Mkuu naanza na maduka kwanza kwa M 50 kabla ya kuanzisha kiwanda,mwelekeo wa maduka ndo utanipa nguvu ya kununua gar,mchine na kuingia rasmi kweny biashara.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu wazo lako zuri...lakini kwa 50m ni ndogo sana hutaweza....tukianza na hiyo gari la fuso used 15m....machine ya kisasa ya kusagia 20m....imebaki 15m.....bado hujafunga machine...kodi ya jengo....kodi ya store....TRA....leseni....TFDA....hujanunua material kama mahindi....hujalipa mishahara ya wafanyakazi wako...kumbuka sio kila bidhaa utakayo tengeneneza utauza....uzoefu huna na wateja wa kutosha huna.... hivyo hasara zakufikia tu..Mkuu kuna ushindani pia...unaweza ukafanya biashara mwaka mzima hujaona faida ya moja kwa moja...lakini matumizi yako pale pale..hivyo ukiwa na mtaji mkubwa unakubeba...hiyo idea angalau ungekuwa na 200m...Nakushauri fanya biashara ya kununua na kuuza nafaka Jumla jumla...au saga sembe na dona uuze hapa hapa ....achana na issue za kupeleka nje ya nchi...wala kuajiri watumishi wengi mapema kiasi hivyo,,,mbinu nzuri ni kuanza na biashara ndogo...ili upate uzoefu na kusoma mazingira...pia itakusadia usipoteze mtaji....kupata mtaji ni rahisi kidogo...issue ni kuukuza huo mtaji...ukicheza kidogo to unarudi kule kule.

Tufunge mada😅😄
 
Mkuu naanza na maduka kwanza kwa M 50 kabla ya kuanzisha kiwanda,mwelekeo wa maduka ndo utanipa nguvu ya kununua gar,mchine na kuingia rasmi kweny biashara.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Ni Tanzania tu utakapokuta mfanyabisha ana mpango wa kuteka soko la kuuza nafaka Afrika nzima lakini hajawahi kufanya biashara ya kuuza robo kilo ya nafana.
 
Mkuu naanza na maduka kwanza kwa M 50 kabla ya kuanzisha kiwanda,mwelekeo wa maduka ndo utanipa nguvu ya kununua gar,mchine na kuingia rasmi kweny biashara.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Pesa hiyo ni ndogo sana, kwa mipango yako hiyo, hiyo 50 million, ni gharama ya kununua mchele ule super kama tani 30 tu!!!! Ila kwa mtaji huo ukiuweka kwenye mchele, na ukapata soko la uhakika kama, nchi za RWANDA, au ZAMBIA, ndani ya miezi sita tu, utakuwa umepata mtaji wa kufanya hayo unayotaka kuyafanya sasa.

Zambia/Rwanda wao wanataka mchele mzuri tofauti na congo/burundi, na siku hizi congo biashara ya mchele sio,nzuri sana kwani kuna wahindi wameanza kuingiza yale ya pakistani, ya bei nafuu, na tatizo la congo hawaangalii quality ya mchele, bali ni kipimo tu!!!
 
Pesa hiyo ni ndogo sana, kwa mipango yako hiyo, hiyo 50 million, ni gharama ya kununua mchele ule super kama tani 30 tu!!!! Ila kwa mtaji huo ukiuweka kwenye mchele, na ukapata soko la uhakika kama, nchi za RWANDA, au ZAMBIA, ndani ya miezi sita tu, utakuwa umepata mtaji wa kufanya hayo unayotaka kuyafanya sasa. Zambia/Rwanda wao wanataka mchele mzuri tofauti na congo/burundi, na siku hizi congo biashara ya mchele sio, kwani kuna wahindi wameanza kuingiza yale ya pakistani, ya bei nafuu, na tatizo la congo hawaangalii quality ya mchele, bali ni kipimo tu!!! Ndio maana siku hizi mchele wa tz kupeleka congo ni hasara, labda mahindi.

Congo nina watu nawajua wanafanya biashara hii,wafanya kimazoea ila bado inawalipa mpaka wanajisahau kuwa wabunifu,ninachotaka kusuindana nao ni ubunifu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sijajua kitu nilichojifunza hapa ila kuna kitu nimejifunza japo sijakijua mpaka sasa...!

Hongera sana mkuu.
 
Moja naomba usirudi nyuma hatua ulizopiga yafaa kuanza tuu na si kingine. Biashara yoyote kuianza ni ngumu ila utazidi kuilewa unavyoendelea nayo si cha msingi wekeza kiasi kidogo katika izo millioni za biashara ili ujifunze mambo mengi, kumbuka kuna wizi, ujanja , dhuruma vyote hivyo utavipitia.

Jambo la pili ingekuwa vizuri ukaanza kununua mchele kutoka kwa store za watu au mikoani au ukapeleka mahindi yako kwa watu wenye mashine wakakukobolea nakusaga. Wewe andaa jina la kampuni ufanye packaging nzuri ukuze brand .Brand ndio itakayokuja kuwa silaha yako kufikia malengo ya kufungua store congo na nchi jirani

Kila la kheri bossy ,usitusahau kwenye ajira

It is never to late to begin. Start now
 
Wazo zuri bro, nikushauri uanze na dsm kwanza. Tengeneza Jina na bland taratibu,zaidi kwa kuanzia mahali ulipo....

Kama tutaanza na unga,....nk ni vizuri then uanze kutanua masoko sasa.
Utapata uzoefu mzuri wa business, lakn unapaswa kuanza na mbinu za ushindani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF na poleni kwa kipindi hichi cha corona.

Mimi ni mjasiriamali ninajishughulisha na biashara mbali mbali.ila katika harakati za kibiashara huwa napenda sana kufanya biashara ya kuuza nafaka ambayo imepakiwa kwa jina langu,mfano kama Azam.

Nilitaka nipite hapa ili niwaeleze jinsi ngani nimejipanga kuanza biashara nikiwa na ndoto ya kushindanishwa na bidhaa za Azam.

MALENGO
malengo yangu ni kuanzisha campuni inayojishughulisha na maswala ya chakula ambacho kimeppakiwa kwenye mifuko na kisambazwe kwa jina langu Tanzania na africa kwa ujumla.

Nitakuwa napakia vyakula kwenye mifuko.mfano:maindi unga,mchele,maharage nk ili niwe nasambanzia watu sehemu mbali mbaliView attachment 1430044
Mfano wa picha hapo juu..

MIPANGO:
Ili kutimiza lengo la biashara hii nataka kwanza nianze tutafuta masoko nchi za tanzania,congo na burundi,hapo kila sehemu nitaweka store mbili mbili ili bidhaa inapofika vinauzwa hapo.

Lakini kabla ya kuanza kupakia products zangu,nitaanza kuuza nafaka kutoka kwenye kampuni zingine ili kupima upepo kwenye store hizo nitakazo kuwa nimefungua.

Ila lengo langu la baadae ni kufungua matawi mengi na kiwanda kikubwa chenye wafanyakazi wengi

MTAJI.
Nina mtaji wa M50 ndo bajet nimepanga katika harakati za kumfikia bakrhesa.
Nina kundi la watu watatu wachapa kazi kweli kweli wanaelewa nini wanafanya wanapokuwa kazini

Katika Team yangu kuna Msimamizi wa shughuli za uzalishaji vyakula,mtafuta masoko mtandaoni na mtaani na mtu wa mipango.wako vizuri maana nimeshashirikiana nao naona wako vizuri kabisa licha hawana elimu ya darasani lakin ni jeshi lenye kuwa na lengo la ushindi.

Nataka ninunue machine 3.
Machine ya kusaga maindi,mashini ya kukoboa maindi,na mshini ya mchele,
NB:najua zipo nyingi za kufanya kazi hii ila nataka nianzie kwanza na hizo tatu.
Kazi zingine zitafanywa na watu.

Baada ya kuanza kutengeneza bidhaa zangu nataka ninunue fuso la kusambaza bidhaa,dar,congo na burundi.

USHAURI.
Biashara hii sina uzoefu nayo na sijawahi kuifanya ila tu ninashauku ya kuifanya na nina imani itanipa pesa.

Sasa ndugu wewe mwana JF ambae una idea na wazo langu au una uzoefu na aina ya biashara ninayoenda kuifanya unaweza kunishauri nini ili nifanyikiwe katika biashara yangu ya kushindanishwa na Azam.

Mfano wa ushauri.
Kias gani kinafaa kuanza nacho.
Nizingatie vitu gani kabla ya kuanza.
Ni wapi nchini Tanzania panafaa kutafuta nafaka na kuweka kakiwanda kangu nk...

NAKUMBUSHA.
Nataka niwe napakiwa maindi,unga ambao nimetengeneza mimi,mchele nilikoboa mimi,maharage niachambue mimi na mazaoengini kwenye mifuko ya uzito tafauti na niwe sambaza nchi tatu tofauti.
Lakini baada ya hatua hii nataka niamie kabisa niwe nauza mpaka samaki wa kopo,yaani chakula kilichopagiwa kwenye makopo au mifuko
Mafano hapo chiniView attachment 1430068

Ushauri wako waweza kunipa hatua ya mafanikio yangu.kwaiyo husisite kunielemisha chochote kuhusu mambo haya ya chakula.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kabda sijachangia ulichouliza, mkuu umenikumbusha mwaka 2008 baada ya kuhitim kidato cha 6 nikajifanya sitaki kukaa home kizembe nikaanza mishe za hapa na pale kusaka pesa. Katika harakati zakutafuta pesa nikakutana na m' bembe mmoja toka Congo (tulikutania ujiji kigoma) akanipa idea yakupeleka Kuku Drc (sintoisahau ile safari) kwanza usiku wa safari hiyo tukiwa robo3 ya safari mawimbi makali yakaanza kutikisa boti na hata maji kuanza kuingia wamiliki wa boti wakasema jamani boti limejaa sana mizigo na watu hivyo yatulazimu tupunguze baadhi ya mizigo ili tusizame.

Wakagusa mzigo wa jamaa mmoja (yalikuwa magunia ya mchele ) jamaa akaja juu akasema mzigo wangu hautupwi, wakagusa mabaloo ya vitenge ya mama mmoja wa kikongo yule mama akacharuka , ikabidi waje kwenye Kuku zangu duh! Namimi nikasara nikasema jaman yan magunia yote yaliyomo humu ndani kuku zangu2 ndio zizamishe boti. Kwa hasira jamaa wa boti wakasema acheni tufe wote lakin baada ya muda wimbi likapoa na hatimae tukafika karemii saa 5 asbuhi .

Tukalala pale tukisubiri mnada kesho yake na ilipofika kesho tukaanza mnada na hapo ndo balaa likaanza mana nilikuwa nimetulia akaja mtu (amevalia sare za jeshi) akaanza petii nani kakutumanga kuweka mabezinesoo hapa nikajibu mkuu ni utaftaji tu nauza mnada akanambia petit yu vile we ni kiyana mudugho Nataka nikusaidiaghe nipe yoghoro moya (jogoo) hakuna wakukushumbua teena, duh! Jamaa lile likaondoka na jogoo Bonge la jogoo.

Hata dakika kumi hazijaisha akaja mwingne "pettii unaitwanga nani " nikajibu "yuu vile nani karuhusu kufanza kufasi ya bhakongo? Sasa ili nikusamehe lete yoghoro moya " duh! Nikabisha jamaa likichomoa shaba likaniambia ntakupigha masase embu wacha bhukaramushi lete yoghoro.

Jamaa walipiga jogoo kama 3 kibabe duh! Sintowasahau. Nikija kwenye thread yako mkuu me uzoefu wangu ni biashara ya mchele na mahindi nchini D.r.c. maeneo ya Kivu kusini, Baraka, karemii na mjini sehemu moja kuna wafurelo wengi jina nimelisahau. Biashara za nafaka Congo zinalipa changamoto ni ubabe tu na ili uepukane na changamoto hiyo upate dalali ambae ni mwenyeji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabda sijachangia ulichouliza, mkuu umenikumbusha mwaka 2008 baada ya kuhitim kidato cha 6 nikajifanya sitaki kukaa home kizembe nikaanza mishe za hapa na pale kusaka pesa. Katika harakati zakutafuta pesa nikakutana na m' bembe mmoja toka Congo (tulikutania ujiji kigoma) akanipa idea yakupeleka Kuku Drc (sintoisahau ile safari) kwanza usiku wa safari hiyo tukiwa robo3 ya safari mawimbi makali yakaanza kutikisa boti na hata maji kuanza kuingia wamiliki wa boti wakasema jamani boti limejaa sana mizigo na watu hivyo yatulazimu tupunguze baadhi ya mizigo ili tusizame. Wakagusa mzigo wa jamaa mmoja (yalikuwa magunia ya mchele ) jamaa akaja juu akasema mzigo wangu hautupwi, wakagusa mabaloo ya vitenge ya mama mmoja wa kikongo yule mama akacharuka , ikabidi waje kwenye Kuku zangu duh! Namimi nikasara nikasema jaman yan magunia yote yaliyomo humu ndani kuku zangu2 ndio zizamishe boti. Kwa hasira jamaa wa boti wakasema acheni tufe wote lakin baada ya muda wimbi likapoa na hatimae tukafika karemii saa 5 asbuhi . Tukalala pale tukisubiri mnada kesho yake na ilipofika kesho tukaanza mnada na hapo ndo balaa likaanza mana nilikuwa nimetulia akaja mtu (amevalia sare za jeshi) akaanza petii nani kakutumanga kuweka mabezinesoo hapa nikajibu mkuu ni utaftaji tu nauza mnada akanambia petit yu vile we ni kiyana mudugho Nataka nikusaidiaghe nipe yoghoro moya (jogoo) hakuna wakukushumbua teena, duh! Jamaa lile likaondoka na jogoo Bonge la jogoo. Hata dakika kumi hazijaisha akaja mwingne "pettii unaitwanga nani " nikajibu "yuu vile nani karuhusu kufanza kufasi ya bhakongo? Sasa ili nikusamehe lete yoghoro moya " duh! Nikabisha jamaa likichomoa shaba likaniambia ntakupigha masase embu wacha bhukaramushi lete yoghoro. Jamaa walipiga jogoo kama 3 kibabe duh! Sintowasahau. Nikija kwenye thread yako mkuu me uzoefu wangu ni biashara ya mchele na mahindi nchini D.r.c. maeneo ya Kivu kusini, Baraka, karemii na mjini sehemu moja kuna wafurelo wengi jina nimelisahau. Biashara za nafaka Congo zinalipa changamoto ni ubabe tu na ili uepukane na changamoto hiyo upate dalali ambae ni mwenyeji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hhaahha nimesoma huku nacheka jamani!..hahaha...kulostishana balaa...! Biashara bila kuwa na roho ya kibabe jamani ngumu sana sana kutoka...!

Mie kiasili huwa mpole sana...yaan soft sana nimekuja gundua watu wananipiga as mie mpole...! Yaan wanatumia huruma nilonayo kuniumiza! Yaani unaweza kufa kwa presha jamani...nimekuwa mtataaa!
 
Back
Top Bottom