Kabda sijachangia ulichouliza, mkuu umenikumbusha mwaka 2008 baada ya kuhitim kidato cha 6 nikajifanya sitaki kukaa home kizembe nikaanza mishe za hapa na pale kusaka pesa. Katika harakati zakutafuta pesa nikakutana na m' bembe mmoja toka Congo (tulikutania ujiji kigoma) akanipa idea yakupeleka Kuku Drc (sintoisahau ile safari) kwanza usiku wa safari hiyo tukiwa robo3 ya safari mawimbi makali yakaanza kutikisa boti na hata maji kuanza kuingia wamiliki wa boti wakasema jamani boti limejaa sana mizigo na watu hivyo yatulazimu tupunguze baadhi ya mizigo ili tusizame.
Wakagusa mzigo wa jamaa mmoja (yalikuwa magunia ya mchele ) jamaa akaja juu akasema mzigo wangu hautupwi, wakagusa mabaloo ya vitenge ya mama mmoja wa kikongo yule mama akacharuka , ikabidi waje kwenye Kuku zangu duh! Namimi nikasara nikasema jaman yan magunia yote yaliyomo humu ndani kuku zangu2 ndio zizamishe boti. Kwa hasira jamaa wa boti wakasema acheni tufe wote lakin baada ya muda wimbi likapoa na hatimae tukafika karemii saa 5 asbuhi .
Tukalala pale tukisubiri mnada kesho yake na ilipofika kesho tukaanza mnada na hapo ndo balaa likaanza mana nilikuwa nimetulia akaja mtu (amevalia sare za jeshi) akaanza petii nani kakutumanga kuweka mabezinesoo hapa nikajibu mkuu ni utaftaji tu nauza mnada akanambia petit yu vile we ni kiyana mudugho Nataka nikusaidiaghe nipe yoghoro moya (jogoo) hakuna wakukushumbua teena, duh! Jamaa lile likaondoka na jogoo Bonge la jogoo.
Hata dakika kumi hazijaisha akaja mwingne "pettii unaitwanga nani " nikajibu "yuu vile nani karuhusu kufanza kufasi ya bhakongo? Sasa ili nikusamehe lete yoghoro moya " duh! Nikabisha jamaa likichomoa shaba likaniambia ntakupigha masase embu wacha bhukaramushi lete yoghoro.
Jamaa walipiga jogoo kama 3 kibabe duh! Sintowasahau. Nikija kwenye thread yako mkuu me uzoefu wangu ni biashara ya mchele na mahindi nchini D.r.c. maeneo ya Kivu kusini, Baraka, karemii na mjini sehemu moja kuna wafurelo wengi jina nimelisahau. Biashara za nafaka Congo zinalipa changamoto ni ubabe tu na ili uepukane na changamoto hiyo upate dalali ambae ni mwenyeji.
Sent using
Jamii Forums mobile app