Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Unapokuwa kiongozi,kauli zako inabidi zisiache ukakasi nyuma.
Naongea ninachokielewa,sina tabia ya kutunga...Unaposema ndege ya NHIF mwananchi wa kawaida atajua kuwa kumbe mfuko wetu wa bima una ndege yake binafsi kama ilivyo AMREF na bima nyingine,ondoa utata na mgogoro wa kijami kuwa "ndege ya kukodiwa na NHIF",maana kuna watu wataona michango yao imenunuan ndege wakati wao bima zao zina-limit baadhi ya magonjwa kutibiwa na hiyohiyo NHIF.

Baada ya CHADEMA kutaka kwenda Nairobi,bunge lilijitoa kugharamia,mzigo ukawa kwa CHADEMA na kina Mbowe,hili ndio Ndugai analipotosha.Tunaojua mahusiano ya Turky na Muna (mmiliki wa Flight Link) tunajuakwanini Mbowe aliamua kumtumia Turky na si Ndugai wala bunge kudhamini.

Hivi hufikirii hata kidogo,kwamba Turky anadhamini ndege yeye binafsi tena kwa mali kauli kuliko Spika?yaani kwanini isiwe bunge ndio liwadhamini kina Mbowe kumsafirisha Lissu na badala yake akawa Turky?Kwamba mpaka mwenye ndege imani yake ni kwa Turky na sio Spika wa Bunge(nje ya jina Ndugai?)

Bunge hata kama halilipi,ndio lilipaswa kudhamini hata kwa mali kauli kuokoa afya ya mmoja wa wabunge wake,maana linaaaminika zaidi kama taasisi kuliko mtu binafsi.Yaani mnataka mpaka dharula ya afya ya mtu ifuate urasimu?Mbona bungeni huwa mnaleta muswaada kwa hati ya Dharura kukwepa mlolongo na urasimu,halafu uhai wa mtu mnakuwa hamna dharula?Ebooo!!!
Salute barafu
 
Si sahihi kumkashifu kiongozi mkubwa kama Ndugai . Barafu uwe na hekima na busara, Tabia kama hizi ndio zimesababisha Lissu akakosa msaada wa pesa.
Hahaaaa badala ya kusikitika imenibidi tu nicheke, kisu kimegusa mfupa [emoji30] [emoji30]
Shukrani kwa kuchangia
 
Alitedhamini ndege hakupenda hata kujulikana,zimepita siku ngapi tangu adhamini?

Ubaguz wa BUNGENI unaonekana na kusikika daily.
Sasa kwanini Lema aanze kutupa lawama kwamba hajahudumiwa na Bunge wakati Mbowe mwenyewe aliomba kwamba wanaomba mgonjwa asipitie njia zinazoruhusiwa na bunge na akasema wapi tayari kubeba gharama?, hivi kama mtoto wako amefaulu kwenda sekondari ya serikali lakini ukaona kwamba kwasababu shule za private ni bora zaidi ukaamua kumpeleka huko, bado utaomba serikali ukamlipie huko private?

Inaonekana wanaolaumu bunge hawafanyi kazi za kuajiriwa kwa maana ya kulipwa mshaara, au hawana bima ya afya, kawaida waajiri walio wengi huwakatia bima za afya wafanyakazi wao, wanapoumwa sio mwajiri tena anayehusika kumlipia mfanya kazi wake, wala hiyo pesa haipo tena kwa sababu ilishapelekwa kulipia bima, sasa ukitaka bunge litoe hiyo pesa kwa bajeti ipi wakati pesa ya matibabu ya Lisu ilishapelekwa NHIF, ila kwa mapenzi ya familia yake na Uongozi wa chama chake wameamua wasiitumie?, sasa kwanini waanze kuomba katika balozi mbalimbali wakati hata hizo nchi hutumia utaratibu huu huu wa bima ya afya wakijua kwamba matibabu ni ghali sana duniani kote?, sio rahisi kwa hizo nchi kuchangia lolote kwa sababu wanajua Lisu ana bima ya afya ila ni kutaka kuendeleza kiburi kisichokua na maana yoyote
 
Mie siwez kubishaba na wewe,ubish wangu na wewe hauna tija kwa Mgonjwa.
Ila huyo Turky amemkana bosi wa Bunge unataka niandike nini tena.
May God bless Lissu as my fellow human being.
 
Ndugai ule ugonjwa utakuwa umempanda kichwani sidhani kama hata ataelewa ulicho andika hapa

Ila uzuri Mungu huwa ni fundi tutasikia matokeo ya uongo wa Ndugai soon na adhabu yake pia

Si ajabu mdomo wake ukaanza kupinda, yuko wapi Komandoo Salmin Amor?
itafika steji viamerika vitapanda kichwani Na ndipo hapo sasa. Ila ataondoka Na wengi hasa vibinti vya udom
 
Kuna watu humu nimeona nao wanachangia kwa upotoshaji,akiwemo mtu anaitwa Tume ya Katiba juu ya namna Lissu alivyotoka Tanzania kwenda Nairobi.

Kwanza naomba ku-declare kuwa nilishiriki "indirectly" kuona namna gani usafiri wa kwenda Nairobi unapatikana,japo nilikuwa mbali na nyumbani,lakini niliwasiliana na wadau ili kuona huyu mtu anapata usafiri kufika eneo la matibabu baada ya kusikia uhitaji mkubwa ni kufika Nairobi usiku uleule.

Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge ilikuwa ni kumleta Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link na si ya NHIF kama anavyosema huyo Ndugai,ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link),bahati mbaya ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.

Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.

Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.

Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Turky wa Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi

Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Arena),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu ya "height" ya ndege,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.

Sijaelewa huu upotoshaji wa huyu Ndugai ameutoa wapi,kwamba kuna ndege ilikodiwa toka Nairobi?Hiyo ndege ni ipi?kwamba aliomba itumie "airspace" ya Tanzania kinyume na sheria za nchi?Kwani sheria za nchi zinavunjwaje kwa ndege iliyoomba kibali kutua Tanzania na ikaruhusiwa?

Huu uwongo ni wa nini?hiyo ndege mliyokodi toka Kenya ni ipi?Maana kila mtu hata siyekuwa Dodoma aliona ndege iliyoondoka na Lissu ni 5H-ETG mali ya kampuni ya FlightLink.

Hii ni kampuni ya Tanzania,ndio maana usajili wa ndege umeanza na "5H",ndege zote zilizosajiliwa Tanzania huanza na "5H",zile za Kenya huanza na "5Y" na majirani Uganda ni "5X"...Wewe Ndugai hiyo ndege ya Kenya mliyoiombea kibali cha kutumia "airspace" yetu tena kinyume cha sheria ni ipi?Na sheria zipi mlizovunja?

Sasa unaona mtu anakuja humu anasema eti Lissu alitoka na ndege Dodoma hadi Dsm then ndio akaenda Nairobi.Huu uwongo mnauzalisha toka wapi??Wacheni upumbavu katika uhai na maisha ya watu sbb ya siasa!!Eboooo!!!!

Nimemsikiliza Ndugai hapa Jf kwenye video,ameongea kwa uchungu na huzuni,sababu maneno ya Lema yamemuingia sana,amefikia hatua ya kusema kama CHADEMA wanataka kumpeleka Lissu India,bunge lipo tayari endapo Waziri atakubali.Maneno ya Lema yamegusa mfupa,Job anajua aliondoka na hali gani hapa nyumbani kwenda India,amekaa miezi kibao akiugua.

Kila aliyekuwa anasimama bungeni,kabla ya kuchangia,alimuombea Spika afya njema na arudi mzima nyumbani.Watu walisali...Kuna siku Bulaya aliongoza sala ya kuomba afya ya spika katika Canteen ya Bunge.

Malumbano yanayoanzishwa na Spika ndani ya bunge juu ya afya ya Lissu si afya kwa ubinadamu na utu.Kuanzia lile la kutofautiana idadi ya risasi na Kubenea mpaka kamati ya maadili,na lile la kusema Turky ndio kachangia.Turky ni muislam safi,sadaka isiyo na mawaa na yenye thawabu haitangazwi.

Palipo na tendo jema,Mungu hufungua riziki...Kuitangaza sadaka ya Turky bungeni ni kumuondolea neema na thawabu kubwakubwa na ndogondogo mja wake aliyetoa sadaka.Mh.Spika,tumia busara kufunga malumbano ya afya ya Lissu Bungeni,wakati upo India,watu walijibiidisha kukuombea na si kujadili na kulumbana juu ya afya yako na matibabu yako.FUNGA MJADALA WA KUSIMANGANA BUNGENI KUHUSU AFYA NA HALI YA TUNDU LISSU...HUU SI UBINADAMU.

Kuna kijana sijui ni msemaji wa chama naye katoka kabisa na "Press Release" kupongeza hali ya Mbunge Turky,kutoa "mali kauli" ya safari ya ndege.Jamani mnaharibu sadaka za wenzenu.Turky mwenyewe amenukuliwa akisema;
" Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” .Watu mnaharibu sadaka za watu bila kujua,nia njema ya Turky ipo katika hayo maneno yake ya mwisho yenye "bold".

Msaidieni Lissu kama nyie mlivyosaidiwa kwa kofia za ubunge na uspika wenu,wacheni masimango,tendeni kama vile mlivyotendewa,wengine mlikwenda India miguu haingii hata katika viatu,mlivaa suti na sandozi.Mungu amewaponya...Lipeni wema juu ya wema!!Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu uliopigwa na kulowa risasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?

barafu wa JF

We Live Once,but Legacy Lives forever!!
View attachment 588456
Juu ni ndege ya kampuni ya FlightLink(Tanzania) iliyompeleka Lissu Nairobi

View attachment 588458
Hii ni ndege ya Safari Air Link iliyokusudiwa kumleta Dsm ikashindikana
BARAFU WEWE NI MUUNGO
 
Mie siwez kubishaba na wewe,ubish wangu na wewe hauna tija kwa Mgonjwa.
Ila huyo Turky amemkana bosi wa Bunge unataka niandike nini tena.
May God bless Lissu as my fellow human being.
Wewe ni mwongo tena mzandiki sana, clip ya video ya Turky inasambaa akihojiwa na waandishi wa habari anakubaliana na yote yaliyosemwa na Ndugai kwamba alitoa dhamana na CHADEMA wamelipa jana saa sita na nusu, acha mapenzi ya kitoto na lawama zisizokua na tija kwa mgonjwa, kama kweli mnampenda Lisu endeleeni kumchangia hadi apone, ama mrudisheni Muhimbili au Aga khan pale DSM ambapo NHIF itamlipia, na kama hofu ni usalama wake, kwanini vijana wa kikundi cha ulinzi wa viongozi wa Chadema tunaowaona wakati wa uchaguzi wasewekwe kumlinda masaa 24 hapo Hospitalini?, acheni kutumia hasira, kiburi na mihemuko isiyo kuwa na maana, haiwezi kumsaidia mgonjwa
 
IMG_20170915_075858.jpg
IMG_20170915_075905.jpg
IMG_20170915_074435.jpg
 
Respect kwako Mkuu barafu
Sijajua motive behind ya Ndugai kuwa frontline ku spin tukio la kushambuliwa kwa Lissu,for whose benefit ????
Comrade
Kwani huelewi kuspin huku
Baada ya plan yao kufail
Wameanza kupindisha maneno
Shame on them

Kwa hili SISI tuliooko HUKU hatuungi mkono unyama huu kwa kificho eti 'wamefanya hayo kulinda maslahi mapana'

cc barafu
 
Wewe ni mwongo tena mzandiki sana, clip ya video ya Turky inasambaa akihojiwa na waandishi wa habari anakubaliana na yote yaliyosemwa na Ndugai kwamba alitoa dhamana na CHADEMA wamelipa jana saa sita na nusu, acha mapenzi ya kitoto na lawama zisizokua na tija kwa mgonjwa, kama kweli mnampenda Lisu endeleeni kumchangia hadi apone, ama mrudisheni Muhimbili au Aga khan pale DSM ambapo NHIF itamlipia, na kama hofu ni usalama wake, kwanini vijana wa kikundi cha ulinzi wa viongozi wa Chadema tunaowaona wakati wa uchaguzi wasewekwe kumlinda masaa 24 hapo Hospitalini?, acheni kutumia hasira, kiburi na mihemuko isiyo kuwa na maana, haiwezi kumsaidia mgonjwa
Akili zako ndipo zilipoishia kufikili pole sana!!! Mtabaki kufanya maigizo tu, yasioweza kuuza hata copy 10!! Poleni sana.
 
Hii nchi tumeshapoteza hata utu na ubinadamu. t
TL yupo hospitalini mahututi halafu watu wazima tena viongozi wanalumbana hadharani na kupotosha kuhusu ndege na gharama za kumsafirisha kwenda Kenya. Shame!

Sent using Jamii Forums mobile app
Taja majina kaka, acha uoga? Kama Ndugai sema, kama Lema sema au hata nani wewe mtaje tu. Uoga ni kifo!!
 
Barafu, Mungu awabariki nyote ambao mlitoa michango ya namna mbalimbali kumfanya mpendwa wetu Lisu aweze kupata matibabu. Hatuna maneno mazuri ya kusema. Hamkutenda kwaajili ya Lisu bali kwaajili yetu sote tuliopatwa na simanzi kubwa katika tukio hili.

Mungu wetu tunaomba usikie maombi yetu, ni maombi yetu sisi wenye huzuni, siyo maombi ya Tundu Lisu. Kama ulimfufua Lazaro, kama uliwaponya viwete, vipofu na wengine wengi, kwa nini isiwezekane kwa Lisu? Tunajua katika wewe Mungu wetu hakuna usiloliweza, ukitaka, mpendwa wetu anaweza kusimama wakati wowote.

Wewe ulisema, 'Ombeni mtapewa', tunajua wewe ni mwaminifu katika ahadi zako. Tunaomba kwaajili ya uhai na afya ya Mpendwa wetu Tundu Lisu.

Tena ulisema, 'Tafuteni mtapata', tunakutafuta wewe uliye asili ya yote, umjalie uzima na afya ndugu yetu Tundu Lisu, aliyepo kitandani, si kwa mapenzi yako bali kwa mapenzi ya ibilisi.

Bwana wetu ulituambia, 'gongeni mtafunguliwa', tunagonga kwenye nyumba ya mamlaka yako ili mkono wako wenye nguvu ukamguse na kumnyanyua ndugu yetu Tundu Lisu.

Ni mapenzi yetu, ndugu yetu arejee katika hali yake lakini kwa mapenzi yako katika haya mateso anayoyapitia, unaweza kumvusha, hata akatoka akawa bora zaidi kama ilivyokuwa kwa Ayubu. Mapenzi yako yatimizwe, sasa na hata milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
Amen [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Back
Top Bottom