Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Rubbish.

Kaa kimya.

Mumeshindwa kuendekeza Hospitali kwa muda mrefu, eti matibabu ya Lisu yaje yaendeleze Muhimbili!!
Una mtindio wa akili kama Ndugai wewe.
 
Mkuu barafu shukrani sana,umenyoosha maelezo vijana wa Lumumba wako hoi bin taabani sijui kama watapewa buku saba leo wameshindwa kujibu mapigo.
 
Chadema mnahangaika bure,mnapoliticise ugonjwa wa Lissu.
Kelele zote ni kwamba bila ya mbunge wa ccm ndege isingepatikana.
Halafu mleta mada una chembe za ubaguzi kwani ni lazima uandike mwenye ndege ni muhindi?
Kwahiyo alitumia kadi ya ccm kupewa hiyo ndege ili imsafirishe Lissu?
 
Rubbish.

Kaa kimya.

Mumeshindwa kuendekeza Hospitali kwa muda mrefu, eti matibabu ya Lisu yaje yaendeleze Muhimbili!!
Una mtindio wa akili kama Ndugai wewe.
NInawasiwasi na uelewa wako, nitaendelea kukuelimisha bure bila malipo yoyote, kwa sasa Tanzania tunaongoza katika kutoa huduma za specialized medicine katika ukanda wote huu, ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo haipeleki tena wagonjwa wa moyo nje ya nchi, badala yake inapokea wageni toka nje ya nchi za jirani ikiwemo Kenya kuja kutibiwa mwgonjwa ya Moyo pale JKCI, Hospital kubwa yenye vifaa vya kisasa vya kutibu cancer katika ukanda huu ni Ocean road, nenda ujionee wakenywa, warundi, na waganda walivyojazana pale. Mloganzila ndiyo itakuwa hosptal ya kisasa zaidi kusini mashariki na kusini mwa Afrika ukiondoa Afrika ya kusini, wewe endelea kuchapa usingizi.
 
Dunia inakuacha wewe ambaye akili yako kama Ndugai.

Unajikosha eti kufuata sheria, sheria zipi mnazozifuata?
Unaojua ule muhimili uliojichimbia? Unaomuamurisha Ndugai(kubwa jinga) awashughulikie wabunge halafu yeye atawashughulikia nje ya bunge.

Ona sasa anajitapa kumzuia Zito kutoongea bungeni kwa kipindi chote kilichobaki, ametoa wapi hiyo sheria? Kwake? Kwa mama yake? Kwako?
 
....Upupu mtupu.
 
Naona unatolea mfano kwa ugonjwa wa moyo, na mambo ya cancer Ocean road, je Lisu alikuwa anaumwa ugonjwa wa Moyo? Cancer?

Mbona huizungumzii MOI?

Tuje kwenye hali aliyokuwa nayo Lisu, japo tulihofia usalama wake ambapo dhamira ya wasiojulikana ilikuwa bado inaendelea mioyoni mwao, kwa haraka angeweza kusaidiwa japo kwa usiku mmoja?

Muhimbili nilikosa ALU nikaenda kununua mwenyewe, mambo mengine tuwe serious bana
 
Eeeh mungu mwingi wa rehema,okoa taifa letu! Tuepushie maumivu,chuki lakini pia waponye wenye majeraha mioyoni mwao kama alivyo mh. Lissu..
Amen
 
Mkuu barafu nilikuwa sijawahi kukufuatilia ila kuanzia sasa hivi nitakuwa nafuatilia maandiko yako.. Big respect mkuuu
Unaitendea haki shule uliyosoma.. Nadhani wewe utakuwa Mwandishi nguli
 
Hizo Hospitali unazozisifia kuwa zinatoa huduma bora kuliko zote East Africa kuna kiongozi yeyote anayekwenda kutibiwa hapo? nafikiri usilete ujinga wa kuchukulia lile tukie la yule mama kulazwa pale Muhimbili kwa kuugua Mafua na kupigwa picha ikawa kama kigezo cha kuwaaminisha watu eti huduma ni bora. Kama tuna huduma bora za magonjwa ya Moyo na Cancer inakuwaje hao akina Ndugai wanakwenda kutibiwa India na Ufaransa? kama tuna huduma bora ilikuwa wale watoto wa ile ajali ya shule ya Luck Vincent wakaenda kutibiwa nje? na tena Baadhi ya kauli za Serikali walijigamba kuwa wao ndio waliofanikisha hilo?
Majibu mnayoyatoa sasa ni wazi yanaendana na chuki na aibu juu ya hiki mlichokifanya ambacho kwa mapenzi ya Mungu dhamira yenu haijatimia. na nina uhakika adhabu mtakayoipata hamtakuja kuisahau kamwe kwani siku zote Mungu ulipa hapahapa duniani.
 
Kwanza usilete matusi kuita watu ni wajinga, kama ni ujinga wewe ni wakwanza kabisa. Pili sema ukweli tangu awamu ya tano imeingia madarakani ni watu wachache sana wanapelekwa nje baada ya sisi hapa nchini kushindwa, sio kwamba tunaweza kila kitu, hata huko India wanashindwa na watu wanakufa, ila kiukweli huduma zimeboreka sana, mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi mbalimbali wamekuwa wakitibiwa Muhimbili kwa sasa, unamkumbuka Martin Shigela alivyotibiwa Muhimbili kwa zaidi ya mwezi alilzwa pale, unamkumbuka yule mbunge wa viti maalumu wa kike aliyegongwa na pikipiki akitoka bungeni pale Dodoma alikua na hali mbaya sana akapelekwa Muhimbili kwa ndege?, unakumbuka mzee kawawa alivyokua akitibiwa nchini hadi kifo chake?, unamkumbuka mtoto wa Magufuli apivyotibiwa Muhimbili hadi alipofariki mwaka 2010?, Hao ni baadhi tu ya watu wanaojulikana ila mawaziri na wabunge wengi sana wanatibiwa nchini, ikishindikana ndiyo hupelekwa nje
 
Umetaja MOI, nitakuomba upite pale MOI ukaangalie jinsi ilivyo kwa upande wa vifaa, dawa na wataalamu na kazi wanazofanya, ukitoka hapo uende Kenya Jommo Kenyatta Hospital utembelee kitengo kama MOI, uende Uganda, Rwanda na nchi zingine, kisha urudi nchini, ninakuhakikishia hutokuja kuandika lolote kuhusu huduma zw tiba Tanzania zaidi ya kukaa kimya au kusifia tu.

Kuhusu Lisu nilishaelezea hapo juu kitaalamu zaidi, ninakuhakikishia hata Lugalo ingeweza kumtibu acha Muhimbili, kama risasi haikupiga kichwani, Shingoni kifuani au haikuliaribu ini, basi tatizo kubwa ni damu aliyopoteza, akiwahi na kuwekewa damu na kutoa risasi na kushona sehemu zilizotobolewa, kinachobaki ni kuuguza vidonda, lishe ya mgonjwa na kumfanyia close assessment ya vital signs kama vile Bp, renal functions, mfumo wa kupumua na mambo machache tu, kazi kubwa kwa Lisu ilifanyika Dodoma, huko Kenya wanamalizia kutoa risasi zilizokuwa hazijatolewa na kufanya hayo hapo juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…