yoeli kagoma
Member
- May 20, 2017
- 37
- 19
Akili zako ni km jina lako shetani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rubbish.Umeshindwa kujenga hoja unaanza matusi, ulitaka mtoa mada asijibiwe au wote tukubaliane na mawazo yake wakati tunaona anapotosha?, wajinga ni wale wanaoacha kutumia bima ya afya walioichangia kwa pesa yao wenyewe wanabaki kuomba omba misaada kwa watu wengine tena nje ya nchi, sasa hiyo milioni 10 kwa siku wanawalepa wakenya badala ya kuja kulipia pale Agakhan au Muhimbili ikazidi kuimarisha Hospital zetu ili ziendee kutuhudumia watanzania wengine vizuri zaidi, utaita huo ninini?
Kwahiyo alitumia kadi ya ccm kupewa hiyo ndege ili imsafirishe Lissu?Chadema mnahangaika bure,mnapoliticise ugonjwa wa Lissu.
Kelele zote ni kwamba bila ya mbunge wa ccm ndege isingepatikana.
Halafu mleta mada una chembe za ubaguzi kwani ni lazima uandike mwenye ndege ni muhindi?
NInawasiwasi na uelewa wako, nitaendelea kukuelimisha bure bila malipo yoyote, kwa sasa Tanzania tunaongoza katika kutoa huduma za specialized medicine katika ukanda wote huu, ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo haipeleki tena wagonjwa wa moyo nje ya nchi, badala yake inapokea wageni toka nje ya nchi za jirani ikiwemo Kenya kuja kutibiwa mwgonjwa ya Moyo pale JKCI, Hospital kubwa yenye vifaa vya kisasa vya kutibu cancer katika ukanda huu ni Ocean road, nenda ujionee wakenywa, warundi, na waganda walivyojazana pale. Mloganzila ndiyo itakuwa hosptal ya kisasa zaidi kusini mashariki na kusini mwa Afrika ukiondoa Afrika ya kusini, wewe endelea kuchapa usingizi.Rubbish.
Kaa kimya.
Mumeshindwa kuendekeza Hospitali kwa muda mrefu, eti matibabu ya Lisu yaje yaendeleze Muhimbili!!
Una mtindio wa akili kama Ndugai wewe.
Dunia inakuacha wewe ambaye akili yako kama Ndugai.Tatizo lako wewe huna uelewa wa basic knowledge kabisa unaendekeza ubishi badala ya kutaka ueleweshwe, invoice is request for payment, while receipt is the proof for payment, mwambie huyo Msigwa aonyeshe risiti waliyolipia hiyo $9,200 tuone tarehee yake. Tatizo la watanzania wengi ni kutosumbua vichwa vyao katikw kufikiria kwa undani wanaendeshwa na ushabiki na kusikiliza maneno ya mitaani, tubadilikeni dunia inatuacha
....Upupu mtupu.Malumbano wanaoanzisha ni chadema wenyewe..wakijibiwa wanaona wanaonewa..ndugai alielezea taifa wingi wa risasi alizopigwa lisu kwenye gari..kubenea akasema ndugai muongo..wakati kitendo tu cha kutaja wingi kule wa risasi ilibidi mumpongeze..maana angeweza pia kukaa kimya..kamsema zito bungeni..zito akagusia lisu..wakati lisu hausiki..Lema nae anamshutumu kuhusu lissu..
Sasa vitu mnaanzisha wenyewe..mkijibiwa mnasema malumbano..basi kaeni kimya uguzeni mgonjwa wenu..ila msidhani shughuli zitasimama kwa sababu ya ugonjwa au kifo cha lisu..hata vikao vya Acacia na timu ya magufuli havijasimama
Naona unatolea mfano kwa ugonjwa wa moyo, na mambo ya cancer Ocean road, je Lisu alikuwa anaumwa ugonjwa wa Moyo? Cancer?NInawasiwasi na uelewa wako, nitaendelea kukuelimisha bure bila malipo yoyote, kwa sasa Tanzania tunaongoza katika kutoa huduma za specialized medicine katika ukanda wote huu, ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo haipeleki tena wagonjwa wa moyo nje ya nchi, badala yake inapokea wageni toka nje ya nchi za jirani ikiwemo Kenya kuja kutibiwa mwgonjwa ya Moyo pale JKCI, Hospital kubwa yenye vifaa vya kisasa vya kutibu cancer katika ukanda huu ni Ocean road, nenda ujionee wakenywa, warundi, na waganda walivyojazana pale. Mloganzila ndiyo itakuwa hosptal ya kisasa zaidi kusini mashariki na kusini mwa Afrika ukiondoa Afrika ya kusini, wewe endelea kuchapa usingizi.
Mkuu barafu nilikuwa sijawahi kukufuatilia ila kuanzia sasa hivi nitakuwa nafuatilia maandiko yako.. Big respect mkuuuKuna watu humu nimeona nao wanachangia kwa upotoshaji,akiwemo mtu anaitwa Tume ya Katiba juu ya namna Lissu alivyotoka Tanzania kwenda Nairobi.
Kwanza naomba ku-declare kuwa nilishiriki "indirectly" kuona namna gani usafiri wa kwenda Nairobi unapatikana,japo nilikuwa mbali na nyumbani,lakini niliwasiliana na wadau ili kuona huyu mtu anapata usafiri kufika eneo la matibabu baada ya kusikia uhitaji mkubwa ni kufika Nairobi usiku uleule.
Suala la kwanza lilioafikiwa na Bunge ilikuwa ni kumleta Dsm-Muhimbili,ndege iliyokodiwa ilikuwa ni ya kampuni ya Safari Air Link na si ya NHIF kama anavyosema huyo Ndugai,ambayo ni MEDEVAC,ilikuwa ni Caravan usajili wa 5H-EWA,mali ya Peter Fox(mmiliki wa kampuni ya Safari Air Link),bahati mbaya ikatokea mabadiliko ya kwenda Nairobi,na ile ndege ikawa na rubani mmoja na haiwezi kwenda Nairobi usiku ikiwa na rubani mmoja ambaye hakuwa na masaa ya kuruka usiku.TCAA walikuwa tayari kutoa kibali cha ndege kuruka usiku hata kama ina injini moja kwa sharti la kuwa na marubani wawili,Ukawa ni mtihani mwingine wa kuanza kutafuta ndege nyingine usiku uleule.
Ndege nyingine ya Safari Air Link aina ya Citation(Jet Engines) siku hiyo ilikuwa imeenda Pemba ya Mozambique kama si Zambia,Fox akawa hana option,sbb pia hiyo ndege isingeweza kubeba abiria wengi ambao CHADEMA walikusudia wasafiri na Lissu.
Ndege kubwa ya kuwatosha mgojwa,daktari pamoja na wasindikizaji akiwemo mkewe, ikawa ni hiyo Citation ya Flight Link,5H-ETG.Ambayo ilipaswa kutoka Dsm kuja Dodoma usiku uleule,ili inyanyuke kwenda Nairobi.
Jambo hili likawezekana,lakini ilipaswa pesa iwe juu ya meza kwa mlipo ya dola,Dodoma hakukuwa na Mbunge wala waziri mwenye dhamana ya dola,Turky wa Mpendae akachukua dhamana hiyo ya mali kauli,sababu mmiliki wa kampuni ya Flight-Link(Mhindi) wana ushirika naye.Ndege ilinyanyuka Dsm-Dodoma na baadae Nairobi
Siri ya safari ile wakiwa angani,naamini ipo siku Mbowe na Msigwa wataiandikia kitabu(A Day to Remember in a Dark Political Arena),Ilikuwa ni safari ngumu iliyojaa machozi na uchungu mkubwa,walisafiri kwa shida sana,kitanda kilikuwa kinacheza na pia dripu ilibidi Dokta asafiri akiwa ameishika mkononi kaining'iniza juu sababu ya "height" ya ndege,ilikuwa ni safari ya mateso na experience mbaya sana kwa kina Msigwa na Mbowe pamoja na mke wa Lissu.Mungu aliyemponya Danieli katikati ya Simba wenye njaa,alitenda miujiza.
Sijaelewa huu upotoshaji wa huyu Ndugai ameutoa wapi,kwamba kuna ndege ilikodiwa toka Nairobi?Hiyo ndege ni ipi?kwamba aliomba itumie "airspace" ya Tanzania kinyume na sheria za nchi?Kwani sheria za nchi zinavunjwaje kwa ndege iliyoomba kibali kutua Tanzania na ikaruhusiwa?
Huu uwongo ni wa nini?hiyo ndege mliyokodi toka Kenya ni ipi?Maana kila mtu hata siyekuwa Dodoma aliona ndege iliyoondoka na Lissu ni 5H-ETG mali ya kampuni ya FlightLink.
Hii ni kampuni ya Tanzania,ndio maana usajili wa ndege umeanza na "5H",ndege zote zilizosajiliwa Tanzania huanza na "5H",zile za Kenya huanza na "5Y" na majirani Uganda ni "5X"...Wewe Ndugai hiyo ndege ya Kenya mliyoiombea kibali cha kutumia "airspace" yetu tena kinyume cha sheria ni ipi?Na sheria zipi mlizovunja?
Sasa unaona mtu anakuja humu anasema eti Lissu alitoka na ndege Dodoma hadi Dsm then ndio akaenda Nairobi.Huu uwongo mnauzalisha toka wapi??Wacheni upumbavu katika uhai na maisha ya watu sbb ya siasa!!Eboooo!!!!
Nimemsikiliza Ndugai hapa Jf kwenye video,ameongea kwa uchungu na huzuni,sababu maneno ya Lema yamemuingia sana,amefikia hatua ya kusema kama CHADEMA wanataka kumpeleka Lissu India,bunge lipo tayari endapo Waziri atakubali.Maneno ya Lema yamegusa mfupa,Job anajua aliondoka na hali gani hapa nyumbani kwenda India,amekaa miezi kibao akiugua.
Kila aliyekuwa anasimama bungeni,kabla ya kuchangia,alimuombea Spika afya njema na arudi mzima nyumbani.Watu walisali...Kuna siku Bulaya aliongoza sala ya kuomba afya ya spika katika Canteen ya Bunge.
Malumbano yanayoanzishwa na Spika ndani ya bunge juu ya afya ya Lissu si afya kwa ubinadamu na utu.Kuanzia lile la kutofautiana idadi ya risasi na Kubenea mpaka kamati ya maadili,na lile la kusema Turky ndio kachangia.Turky ni muislam safi,sadaka isiyo na mawaa na yenye thawabu haitangazwi.
Palipo na tendo jema,Mungu hufungua riziki...Kuitangaza sadaka ya Turky bungeni ni kumuondolea neema na thawabu kubwakubwa na ndogondogo mja wake aliyetoa sadaka.Mh.Spika,tumia busara kufunga malumbano ya afya ya Lissu Bungeni,wakati upo India,watu walijibiidisha kukuombea na si kujadili na kulumbana juu ya afya yako na matibabu yako.FUNGA MJADALA WA KUSIMANGANA BUNGENI KUHUSU AFYA NA HALI YA TUNDU LISSU...HUU SI UBINADAMU.
Kuna kijana sijui ni msemaji wa chama naye katoka kabisa na "Press Release" kupongeza hali ya Mbunge Turky,kutoa "mali kauli" ya safari ya ndege.Jamani mnaharibu sadaka za wenzenu.Turky mwenyewe amenukuliwa akisema;
" Mbowe akaniomba kwa kuwa nafahamiana nao (wenye ndege) niwadhamini wamuwahishe Lissu halafu wao watalipa. Na ndicho nilichofanya (kuwadhamini kwa mali kauli) na pesa hiyo imelipwa jana. Tunamshukuru Mungu nia njema hufungua milango yake” .Watu mnaharibu sadaka za watu bila kujua,nia njema ya Turky ipo katika hayo maneno yake ya mwisho yenye "bold".
Msaidieni Lissu kama nyie mlivyosaidiwa kwa kofia za ubunge na uspika wenu,wacheni masimango,tendeni kama vile mlivyotendewa,wengine mlikwenda India miguu haingii hata katika viatu,mlivaa suti na sandozi.Mungu amewaponya...Lipeni wema juu ya wema!!Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu uliopigwa na kulowa risasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?
barafu wa JF
We Live Once,but Legacy Lives forever!!
View attachment 588456
Juu ni ndege ya kampuni ya FlightLink(Tanzania) iliyompeleka Lissu Nairobi
View attachment 588458
Hii ni ndege ya Safari Air Link iliyokusudiwa kumleta Dsm ikashindikana
Hizo Hospitali unazozisifia kuwa zinatoa huduma bora kuliko zote East Africa kuna kiongozi yeyote anayekwenda kutibiwa hapo? nafikiri usilete ujinga wa kuchukulia lile tukie la yule mama kulazwa pale Muhimbili kwa kuugua Mafua na kupigwa picha ikawa kama kigezo cha kuwaaminisha watu eti huduma ni bora. Kama tuna huduma bora za magonjwa ya Moyo na Cancer inakuwaje hao akina Ndugai wanakwenda kutibiwa India na Ufaransa? kama tuna huduma bora ilikuwa wale watoto wa ile ajali ya shule ya Luck Vincent wakaenda kutibiwa nje? na tena Baadhi ya kauli za Serikali walijigamba kuwa wao ndio waliofanikisha hilo?NInawasiwasi na uelewa wako, nitaendelea kukuelimisha bure bila malipo yoyote, kwa sasa Tanzania tunaongoza katika kutoa huduma za specialized medicine katika ukanda wote huu, ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo haipeleki tena wagonjwa wa moyo nje ya nchi, badala yake inapokea wageni toka nje ya nchi za jirani ikiwemo Kenya kuja kutibiwa mwgonjwa ya Moyo pale JKCI, Hospital kubwa yenye vifaa vya kisasa vya kutibu cancer katika ukanda huu ni Ocean road, nenda ujionee wakenywa, warundi, na waganda walivyojazana pale. Mloganzila ndiyo itakuwa hosptal ya kisasa zaidi kusini mashariki na kusini mwa Afrika ukiondoa Afrika ya kusini, wewe endelea kuchapa usingizi.
Kwanza usilete matusi kuita watu ni wajinga, kama ni ujinga wewe ni wakwanza kabisa. Pili sema ukweli tangu awamu ya tano imeingia madarakani ni watu wachache sana wanapelekwa nje baada ya sisi hapa nchini kushindwa, sio kwamba tunaweza kila kitu, hata huko India wanashindwa na watu wanakufa, ila kiukweli huduma zimeboreka sana, mawaziri, wakuu wa mikoa na viongozi mbalimbali wamekuwa wakitibiwa Muhimbili kwa sasa, unamkumbuka Martin Shigela alivyotibiwa Muhimbili kwa zaidi ya mwezi alilzwa pale, unamkumbuka yule mbunge wa viti maalumu wa kike aliyegongwa na pikipiki akitoka bungeni pale Dodoma alikua na hali mbaya sana akapelekwa Muhimbili kwa ndege?, unakumbuka mzee kawawa alivyokua akitibiwa nchini hadi kifo chake?, unamkumbuka mtoto wa Magufuli apivyotibiwa Muhimbili hadi alipofariki mwaka 2010?, Hao ni baadhi tu ya watu wanaojulikana ila mawaziri na wabunge wengi sana wanatibiwa nchini, ikishindikana ndiyo hupelekwa njeHizo Hospitali unazozisifia kuwa zinatoa huduma bora kuliko zote East Africa kuna kiongozi yeyote anayekwenda kutibiwa hapo? nafikiri usilete ujinga wa kuchukulia lile tukie la yule mama kulazwa pale Muhimbili kwa kuugua Mafua na kupigwa picha ikawa kama kigezo cha kuwaaminisha watu eti huduma ni bora. Kama tuna huduma bora za magonjwa ya Moyo na Cancer inakuwaje hao akina Ndugai wanakwenda kutibiwa India na Ufaransa? kama tuna huduma bora ilikuwa wale watoto wa ile ajali ya shule ya Luck Vincent wakaenda kutibiwa nje? na tena Baadhi ya kauli za Serikali walijigamba kuwa wao ndio waliofanikisha hilo?
Majibu mnayoyatoa sasa ni wazi yanaendana na chuki na aibu juu ya hiki mlichokifanya ambacho kwa mapenzi ya Mungu dhamira yenu haijatimia. na nina uhakika adhabu mtakayoipata hamtakuja kuisahau kamwe kwani siku zote Mungu ulipa hapahapa duniani.
Umetaja MOI, nitakuomba upite pale MOI ukaangalie jinsi ilivyo kwa upande wa vifaa, dawa na wataalamu na kazi wanazofanya, ukitoka hapo uende Kenya Jommo Kenyatta Hospital utembelee kitengo kama MOI, uende Uganda, Rwanda na nchi zingine, kisha urudi nchini, ninakuhakikishia hutokuja kuandika lolote kuhusu huduma zw tiba Tanzania zaidi ya kukaa kimya au kusifia tu.Naona unatolea mfano kwa ugonjwa wa moyo, na mambo ya cancer Ocean road, je Lisu alikuwa anaumwa ugonjwa wa Moyo? Cancer?
Mbona huizungumzii MOI?
Tuje kwenye hali aliyokuwa nayo Lisu, japo tulihofia usalama wake ambapo dhamira ya wasiojulikana ilikuwa bado inaendelea mioyoni mwao, kwa haraka angeweza kusaidiwa japo kwa usiku mmoja?
Muhimbili nilikosa ALU nikaenda kununua mwenyewe, mambo mengine tuwe serious bana
Mkuu,kuna viumbe wanaishi kwa kazi moja tuu,kukwaza wenzao basi.inasikitisha sanaaHebu toka hapa bana!