Safari ya Lissu kuelekea Nairobi ilikuwa ni mateso na vilio, Spika Ndugai usitoneshe vidonda

Mnaleta "urasimu" wa taratibu za matibabu nje ya nchi kwa mwili wa binadamu uliopigwa na kulowa risasi zaidi ya 10?Ebooo!!HIZO PESA ZA MAMA ZENU?
Umegonga ndipo- hii mijitu hovyo.
 
Wanatukamata mkuu tukifanya hivyo.

Jana wamekamata watu Hospitali ya Temeke waliokuwa wanachangia damu
 
Asante sana mkuu barafu kwa kuweka mambo sawa...

Asante Mungu Baba kwa miujiza uliyotenda tangu siku ya kadhia hii.
Endelea kujidhihirisha juu ya Afya ya Mpendwa wetu Lissu!

Wajaze aibu, majuto na uendelee kuwanyima amani ya roho watesi wake wote siku zote kama ulivyomtenda "Yuda msaliti"

Sisi tutakupigia magoti ewe Mungu wetu Uishie, wao waendelee kumsujudu shetani aliyetupwa kuzimu.

Amen!
 
IPO siku ukawa wakishika nchi, wengine watakunya kwenye ndio subirini hakuna marefu yasiyo Na ncha

Hawawezi kushika nchi bila ya tume huru ya uchaguzi na Katiba kubadilishwa, na wa kushinikiza haya kufanyika ni mimi na wewe si mwingine.
Hakuna wa kutoka taifa lingine kuja kusisitiza hilo mkuu, ni mimi na wewe tu.
Wanasiasa hufanya mambo kulingana na wananchi wao walivyo, Mzee wa kazi kila analofanya anajua 2020 atapita tu sababu kila kitu chake, katiba yao na tume ya uchaguzi yao pia.
Na usishangae 2025 akataka kubadilisha katiba aendelee.
 
Ndungai anatafuta umaarufu wa siasa kupitia uhai wa Lissu amesahau kuwa uhai wa mtu ni zawadi kutoka kwa Mungu leo kwangu kesho kwako.
 
Unapokuwa kiongozi,kauli zako inabidi zisiache ukakasi nyuma.
Naongea ninachokielewa,sina tabia ya kutunga...Unaposema ndege ya NHIF mwananchi wa kawaida atajua kuwa kumbe mfuko wetu wa bima una ndege yake binafsi kama ilivyo AMREF na bima nyingine,ondoa utata na mgogoro wa kijami kuwa "ndege ya kukodiwa na NHIF",maana kuna watu wataona michango yao imenunuan ndege wakati wao bima zao zina-limit baadhi ya magonjwa kutibiwa na hiyohiyo NHIF.

Baada ya CHADEMA kutaka kwenda Nairobi,bunge lilijitoa kugharamia,mzigo ukawa kwa CHADEMA na kina Mbowe,hili ndio Ndugai analipotosha.Tunaojua mahusiano ya Turky na Muna (mmiliki wa Flight Link) tunajuakwanini Mbowe aliamua kumtumia Turky na si Ndugai wala bunge kudhamini.

Hivi hufikirii hata kidogo,kwamba Turky anadhamini ndege yeye binafsi tena kwa mali kauli kuliko Spika?yaani kwanini isiwe bunge ndio liwadhamini kina Mbowe kumsafirisha Lissu na badala yake akawa Turky?Kwamba mpaka mwenye ndege imani yake ni kwa Turky na sio Spika wa Bunge(nje ya jina Ndugai?)

Bunge hata kama halilipi,ndio lilipaswa kudhamini hata kwa mali kauli kuokoa afya ya mmoja wa wabunge wake,maana linaaaminika zaidi kama taasisi kuliko mtu binafsi.Yaani mnataka mpaka dharula ya afya ya mtu ifuate urasimu?Mbona bungeni huwa mnaleta muswaada kwa hati ya Dharura kukwepa mlolongo na urasimu,halafu uhai wa mtu mnakuwa hamna dharula?Ebooo!!!
 

Tatizo la hapo bongo ni moja tuu wajinga ni wengi kuliko werevu
 
Kuna wakat napatwa na hasira sna ..huyu ndugai anakera sana..akili zake ameziacha kule india au ubongo wake umepatwa na fungus ?.. Anaongopa mchana kweupe mbuzi wanakula majani..hii ni aibi sna..
Sampuli of G[emoji23]G[emoji23]
Society
 
Mkuu barafu naona leo umeamua kutoa povu....sisi tuliambiwa kuwa TL kapelekwa Nairobi kwa sababu za kiusalama sio kwamba muhimbili matibabu hayatoshi.

Cha kushangaza sasa kama sababu ni za kiusalama kwa nini mulazimishe safari ili hali mazingira ya usafiri hayakuwa rafiki?

Kulikuwa na haja gani ya kusafiri kwa mazingira hayo ya kumshikia madrip TL je hamkuweza kuona kuwa mngemsababishia mauti??

Kiukweli tukio la TL kila mtu mpenda amani analipinga ila nyinyi wenzetu mmeamua kulichukulia kisiasa na ndo mana na ndo mana wengine wanashindwa kukaa kimya mana kwenye siasa hakuna anayekubali kuonekana kushindwa.

Jaribuni kutumia busara,tangu mwanzo mmepotoka mno jinsi mlivyolishughulikia hili swala kisiasa kwa kukosa kuwa na Iman na serikali na hata kupoteza ile hali ya utu na ubinadamu kwa kutambua tuna mwenzetu yupo hospitalini na anahitaji maombi yetu watanzania ili aweze kupambania afya yake.
 
Alitedhamini ndege hakupenda hata kujulikana,zimepita siku ngapi tangu adhamini?

Ubaguz wa BUNGENI unaonekana na kusikika daily.
 
Kuna vitu vilikuwa havijawahi kutokea hapa Tanzania navyo Ni majibizano yasiyokuwa Na tija. Hakuna haja ya kuongelea mambo usiyoyajua. Tujitahidi kuombeana.
 
Si sahihi kumkashifu kiongozi mkubwa kama Ndugai . Barafu uwe na hekima na busara, Tabia kama hizi ndio zimesababisha Lissu akakosa msaada wa pesa.
Kwani amekosa matibabu?
Kukosa msaada wa kipesa kumemuondolea uhai?
Kabla ya kuwa mbunge alikuwa anatibiwa kwa msaada wa nani?
Wewe utakuwa ni MGOGO WA CONGWA[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
 
Kaa kimya unajiaibisha.
 
Nina historia ya kujadiliana kwa staha mimi na wewe humu jamvini,nataka kuidumisha historia hiyo,nisaidie kuidumisha pia...Asante!!
 
Dah kwa mara ya kwanza nimetoa machozi Ndugai na wote waliohusika kuna siku Mungu atawalipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…