Kupata kazi au kuomba kazi USA unahitaji vitu viwili, 1: Kitambulisho cha state (sawa na kitambulisho cha taifa Tanzania) na 2: Social security number (sawa na Tax ID number ya mtu binafsi kwa tanzania).
Ukiwa na student visa, unaweza kwenda kwa mamlaka husika ukapata hivyo vitu viwili. Ukioa raia wa USA pia unapata residency card hivyo unapata hivyo vitu viwili kiurahisi. Ila kwa visitor visa, HAKUNA JINSI YA KUPATA HIZO cards 2 ya SSN na ID card. Kwa hio ndio maana kuliko mtu uje USA na visitor visa kama unakuja kutafta maisha, BORA UBAKIE AFRICA TU hadi uweze pata visa nyingine. Wengi huwa wanateseka sana sana.