Safari ya Matumaini ya Simba Sport Club . Yaliyo Mbele na Nyuma ya SSC —Part 2

Mk54

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2016
Posts
1,996
Reaction score
3,950
—Kwanza napenda kumpongeza sana Muhammad D. Ni moja ya watu ambao wanamchango mkubwa kwa Simba kufika ilipofika. Huyu ni mmoja wa wamiliki wa Simba mwenye hisa kubwa kuliko yeyote as per individual.

—Muhammad anamiliki 49% ya hisa zote baada ya kukataliwa kumiliki zaidi ya 50% na Serikali ya TZ.

MICHUANO YA KLABU BINGWA AFRICA..
---------------------
— SSC imeonesha ukomavu kwenye soka na kikosi chake chenye gharama chini ya bil 3.

Tout Puissant Mazembe ni moja ya klabu tajiri barani Africa yenye historia nzuri ikiwa ni pamoja na kuchukua makombe hayo zaidi ya mara 4.

Kikosi chake Kina kadiriwa kuwa na gharama zaid ya bil 40 TZS.

—SSC imeweza kucheza mpira mzuri sana leo na pongezi za dhati ziende kwa Medie Kagere ambaye alionesha jitihada za dhati ni mchezaji akili nyingi anapokuwa maeneo ya 18, ile tikitaka aliyoruka hakika mungu anakuona Medie bahati haikuwa kwako tu.

— Kocha bado anatakiwa kusoma game kama hizi kimapana zaidi,Chama sio mchezaji wa kutoka kabisa, Chama ni moja ya wachezaji wanaoweza kuleta athari in no time hasa Kwenye game kama hizi. Aidha, kiwango cha Okwi kwakweli hakiridhishi japo bado ni mchezaji mzuri.

— I have no personal interest kuhusu Bocco, lakini hili nitalisema.

Kati ya wachezaji wa SSC ambao sio wa kutegemea na hawajawahi kuwa makini and not to trust basi ni Bocco.

—Bocco hata akiwa yeye na kipa hajawahi kuwa makini wala Creative. Nilistuka sana kuona kocha kumpa Bocco kupiga Penalty. Kuna jumla ya magoli mengi sana ambayo bocco anabaki yeye na kipa lakini still anakosa, na leo pia alipata position 2 yeye na kipa lakini ni totally disappointment .

—Akaja kuwa discourage wachezaji wote kwenye kukosa penalty. Tunajua hata Ronaldo huwa anakosa penalty, 'Isooke' lakini kwa Bocco ni muendelezo wa failure ambao amekuwa akionesha many times. Mpira sasa hivi ni biashara, ikiwa huwezi kuwa makini na creative kwakweli unaitia timu hasara na taifa zima. Mfano Samatta sio mchezaji mzuri sana but one of the thing ambayo sammata anayo ni kuweza kumalizia magoli vizuri. Wa TZ tuna vichwa vizito sana, wachezaji wa nje ndio wanaonekana kuwa makini mara nyingi sana. Seme wazi kuwa sijawahi kuwa na imani na Bocco tangu zamani. Bocco ni mchezaji ambaye mpaka ashinde ndio ushangilie hata kama yupo yeye na kipa, hate it or what but he has never been serious this dude.

—Goli la chama kati ya As Vita na Simba, kwa nafasi ile Bocco anapaisha, ni mchezaji asiye makini kabisa bila hata kujua umuhimu wa mechi anayocheza. Lakini pamoja na hayo ona kuwa haya yote tanatokana kwasababu kocha ameshindwa kusoma wachezaji wake vyema. Moja ya sifa ya kocha mzuri ni kujua wachezaji wako hasa kwenye game kubwa.

—Ni wazi kuwa mazingira ya Simba kusonga hatua ya nusu fainali ni madogo yaani chini ya asilimia 40, ni ukweli mchungu, face it.

—Lakni pamoja na hayo ni lazima watoke 4 kwenye hii Round na tumeshaona Al ahly ilivyochezea mvua leo, it is no Joke kuwa round hii ni ngumu.

—Simba imefikia hatua nzuri na ni fursa kwake na yafuatayo ni miongoni Muhammad anatakiwa kuyafanya,

1. Shauri atafutwe kocha mwingine mzuri zaidi na SSC iongeze bajeti kwa ajili ya kupata kocha bora

2. Muhammad alisema kuna wachezaji ambao SSC haitoendelea nao, basi Bocco na E.Okwi ni wachezaji wanaopaswa kuwa kwenye hiyo list especially Bocco, wamuuze right now. Maisha ya sasa ni ushindani, kama Huwezi kuonesha utofauti then hufai. Wa TZ hatujui kujiongeza wala kutumia fursa sijui tunashida gani lakini. Sammata alitokea Simba just kwa kuonesha utofauti, ni miongoni mwa wa TZ wachache wenye IO nzuri.

3. Usajili uzingatie wachezaji waliowahi kushiriki michuano ya kimataifa ambayo mchezaji âmeshiriki.

4.Usajili unapaswa kuzingatia nafasi ya beki, kiungo na safu ya ushambuliaji, pande zote hizi zinapwaya pwaya sana.

5. SSC inapaswa kuunda kamati itakayokuwa inafanya kazi ya kuleta proposal za namna gani timu inaweza kuongeza vyanzo vya fedha, mtaji mkubwa kwenye mpira ni pesa.

Pamoja na yote, SSC itambue kwamba nafasi ya kuvuka bado ipo kwenye mikono yao. Na hili litawezekana kama itaweza kucheza huko Congo kama ilivyocheza leo taifa, a die hard game. Inawezekana, ni Mind set tu. Tumewaona Tout Puissant, wala hawatishi kiivo, SSC wakichange Mind zao basi yanawezekana.

Mwisho, hili la Bocco lifanyiwe kazi.

Saturday 6, April 2019.
--------------------

Tunaomba na Yanga yetu apatikane Mdhamini wa dhati maana hali ni tete.
 
Nakubaliana na wewe katika yote hasa hasa kuhusu Bocco. Huyu jamaa ni mtu wa mismati na sio malengo. Mie alipochukua mpira tu nikazima na tv. Hata penati yake ya mwisho na mbao ilikua ni kubahatisha tu.

Bocco asiwe mchazaji tegemezi, awe sub inamtosha. Pale mbele itafutwe mashine nyingine ya kusaidiana na Kagere tu. Sijui Tuyisenge wameishia wapi. Tukienda congo na haya masihara ya Bocco tutavuna mabua.
 

Bocco ni Mtu wa wasiwasi sana. Hajiamini.
 
Umeongea point mkuu, kwa kweli Bocco so tu kwa kukosa penalty leo lakn amekuwa hana umakini kwenye ku score, anaweza pata nafasi 10 akapata 2, au akose zote.
Ndiyo ana mchango mkubwa sana kwa kutoa assists lakn so mchezaji wa kutegemea ku score, nadhan kuna haja ya kuanzia sub.
Lakini pia kuna kitu huwa nakiona kwenye Dimba la kati, Mkude na Kotei binafsi huwa sioni kama n watu sahihi kucheza pamoja kwan wote ni defensive midfielders, hakuna wa kupandisha timu, ushauri wangu awe anaanza mmoja then akae namba 8 mzuri wa kupandisha timu, mfano mzuri mechi ya Simba na As Vita Taifa hatukuwa na mkude ila Timu ilicheza kwa kushambulia sana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh! Soka la bongo bwana,juzi tu Boko alikuwa anasifiwa leo kukosa penati eti hafai! Bado tuna safari ndefu sana na sijui tutafika lini?
 
Duh! Soka la bongo bwana,juzi tu Boko alikuwa anasifiwa leo kukosa penati eti hafai! Bado tuna safari ndefu sana na sijui tutafika lini?
Boco hafai kweli....inatakiwa acheze mechi za Katavi huko....Chai Iringa Mecco ya Mbeya Bandari Mtwara Ridiko ya Lindi kama zipo....hizo timu ndio saizi yake apangwe
...sio kupangwa mechi kubwa kama ya leo....yupo kama Hashim Thabiti
..njemba kama hizi hazinaga hamu ya mafanikio makubwa wapo wapo tu ...
 
Boko amekosa akili yakufunga magori na kufunga magor c jukumu lakocha kukufundisha, alaf machezaji kama yakina boko makocha uwaga yana yapenda kuwapag, tukilud nyuma enzi za Maximo alikuwa anapenda kumpaga mwaikimba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bocco na Wachezaji warefu wapo mbali na Ardhi , huku wachezaj wafupi wakiwa karibu na Ardhi nahata Center of gravity yao inakua ndogo.

Sasa kwa kupiga mipira ya Penati, Faulo, au mashuti... NILAZIMA wachezaji hawa warefu wainame kidogo ili kuwa karibu na Ardhi na hiyo inawaongezea Stamina na kufanya Mpira ukandamizwe kushuka chin nasio kupaa juu.


Ikiwa wachezaji warefu kama boko wataendelea kupiga mipira wakiwa wamisimama, kuangua minazi itabaki kua ka mazoea.


But jamaa ni Mzuri. Anakaba, anakasi, sio mchoyo...... Kikubwa kocha Amuelekeze namna ya Kupiga mipira hiii ....


Na akifanikisha hilo. Basi jamaa atakua mzuri.


The Devil puts a spoonful of honey into neighbor's Wife
 
Mbona siku zote tunashinda huwa hamuandiki haya kuwalaumu wachezaji....chamsingi hapa ni kuwatia moyo wachezaji wajiandae vizuri kwa gemu inayokuja

Wewe tumia akili kabda hujanena.
 
Duh! Soka la bongo bwana,juzi tu Boko alikuwa anasifiwa leo kukosa penati eti hafai! Bado tuna safari ndefu sana na sijui tutafika lini?

Wewe tumia akili kabda hujanena
 
Ushauri mzuri sana.Ila kwa maoni yangu huyu kocha bado ni mzuri tu,la msingi ayafanyie kazi yale mapungufu.Kwa upande wa Boco nadhani pia kiwewe kilimzonga,la msingi kama mchezaji match kama hiyo unahitaji kujisikilizia,kama unahisi hujatulia unamwachia mwingine.
Kama mtoa mada alivyomalizia,TP Mazembe siyo timu ya kutisha,kama kiwango ndo hiki msishangae Simba inaandika historia maana haijaruhusu goal.

Tuwape moto Simba,tusilete ushabiki wa Kamwene kwenye mambo serious.
 
Kichuya ni mfupi, lakini mipira yote anayopiga lazima apaishe, na ili afunge goli, inabidi awe mbali na goli ili mpira uliopaa uanze kushukia golini
 
Kila mtu baada ya matokeo huwa anakuwa makocha. Kukosa penalti ni jambo linalotokea.Bocco ndio mpiga penalti wa Simba. Kama ni kukosa sijui mara ya mwisho ilikuwa lini?
Okwi alikosa na Kagera mwaka jana tukapoteza rekodi yetu ya kutokufungwa.
Mpira wakati mwingine una matokeo katili.Sio wakati wa kutafuta mchawi.
Nani alijua Al Ahly anapigwa goli 5 leo? Kwa mujibu wa tovuti yao ni moja ya matokeo mabaya waliyoyopata kwenye mashindano ya CAF.
Football ndio ilivyo.
 
Kuna siku niliona uzi ukimsifu Boco kwamba ni mchezaji anayekuwa kiwango kila kukicha.

Nikasema kwa sababu mimi ni Simba damu, ngoja nitunze mawazo yangu nisitofautiane na washabiki wenzangu.
 
Kiuhalisia kikosi hiki cha Simba ni kikosi kilichosukwa kwa malengo ya muda mfupi (short run), na moja ya lengo kubwa ilikuwa ni kushiriki makundi, swala la kuvuka ni bonus.

Ili kumudu ushindani, ni wakati wa Simba kuhakikisha inakuwa na academy ambayo ni classic, yenye kujumuisha vipaji kutoka sehemu mbalimbali za Africa, hapo tutakuwa tunajihakikishia wachezaji ambao wanajua culture ya timu na wanakuwa na competitive mind.

Age ni kitu cha kuangalia kwenye hili pia, maana unapounda timu ya kukaa muda mrefu lazima nguzo kubwa iwe umri, veterans kadhaa watatakiwa kuwepo ili kuwa-mentor madogo.

Nina uhakika Mo ana team ambayo ina uwezo huo, ni kuongeza scouts tu kwa ajili ya kutambua vipaji all of Africa.

Hapo Simba itakuwa ya kimataifa na uwekezaji wa jamaa utamlipa sana.
 
Simba wamejitahidi wenzenu mliokua kundi moja wamepigwa hamsa huko bora ninyi mmejitahidi sana wacongo walikuja kuzuia sare au wafungwe magori machache ndio maana mfumo wao wa kuzuia ulikua na wachezaji karibu nane wanarudi kushambulia ni wawili tuu...na wamefanikiwa na wachezaji wa Simba wamejitahidi kadri ya uwezo wao matokeo leo hayakua upande wenu ndio maana umeona magori ya wazi yakikoswa wakati mechi ya Vita au Nkana magori magumu yalifungwa hayo yote kwenye soka yanayotokea...
 
Mkuu kuna kamati maalum inayoshughulikia masuala yote ya kujenga timu.Kuna wachezaji wameshakuwa marked kwa usajili.
Mmoja yupo Dar muda mrefu. Wataachwa wachezaji kadhaa na wengine watasajiliwa ili,kuendelea kujenga timu ya kushindana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…