Safari ya Miaka 60: Kitabu Cha Picha Historia ya Tanzania

Safari ya Miaka 60: Kitabu Cha Picha Historia ya Tanzania

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SAFARI YA MIAKA 60 NDANI YA CHAPISHO LA PICHA ZA HISTORIA YA TANZANIA

Leo Maktaba imebahatika kutembelewa na mwandishi wa kujitegemea ambae ameandika na anaendelea kuandika sasa kwa miaka na magazeti maarufu ya Ulaya.

Ally Sultan.

Ally Sultan hakuja mikono mitupu amekuja na kitabu na jarida na vyote amehusika kuchapa kwake akishirikiana na Kumail Jafferji.

Kazi hizi mbili zinatosha kuwaeleza Ally Sultanna Kumail Jaffreji ni nani katika tasnia ya uandishi na uchapaji.

Chapisho la kwanza hapo: ''Photographic Journey 60 Years of the United Republic of Tanzania The Union of Tanganyika and Zanzibar 1964 - 2024.''

Utangulizi wa kitabu hiki cha picha umeandikwa na Dr. Samia Suluhu Hassan.
Chapisho la pili ni jarida Zanzibar Investment and Insights (ZIBI).

Ally Sultan ameitunuku Maktaba machapisho yote mawili.
Niseme nini kuhusu machapisho haya?

Wazanzibari ni hulka yao wakawepo lakini ikawa usiwaone hadi uwatafute.
Ikiwa hujawatafuta basi maisha watakuwa kwako wewe hawapo mfano wa nyota mchana.

Nyota zipo nyakati zote angani lakini huwezi kuziona hadi usiku uingie.
Katika kitabu hiki cha picha hakika ni safari ndefu ya zaidi ya miaka 60 iliyotajwa kitabuni.

Picha kitabuni zimeandikiwa maelezo ya kina ambayo yatamwekea mwanafunzi yeyote wa historia ya Tanzania yote yaliyo muhimu katika muungano wa nchi hizi mbili, Tanganyika na Zanzibar.

Karibu tufunge safari.

1733545498548.png

1733545554523.png

Ally Sultan​
 
Back
Top Bottom